Sheikh Ponda: Sherehe za Mapinduzi zichunguzwe

Sasa tukiungana malkia anafaidika na nini?
Muwekezaji mkubwa na mkopeshaji mkuu wa Tanzania ni Uingereza.Hata mifumo ya serikali na mabunge yetu lazima yafanane na ya Uingereza.Usisahau kanisa la Anglikana ndo kanisa la malkia na Lina mali nyingi Zanzibar.Ukimuuliza Yeriko Nyerere Kuna barua serikali ya Tanzania iko chini ya ulezi wa Maria mama wa Yesu.
 
Mleta nada kaandika uongo eti waingereza walihusika kumpindua Shamte kiongozi wa Zanzibar

Swali ni Kwa nini Shamte aliamua kukimbilia uingereza kuishi maisha yake kule?

Haiingii akilini SI angekimbilia nchi za kiarabu kwa nini aliona nchi bora ni uingereza?
Shamte alikimbilia Uingereza kweli? Hebu muulize mtoto wake Taga mwenzako Baraka Shamte.
 
Sheikh bora wa muda wote💪💪💪
dj6.jpg
 
Kila Mara uwa nasema humu.
MUUNGANO NI MALI YA MALKIA WA UINGEREZA.
Yeyote atakayejaribu kuugusa huu muungano ataadhibiwa na kupotezwa na hakuna mtu yeyote ndani au nje ya Tanzania atakayeongea.
Ndo maana masheikh wa uamsho sijawahi kusikia watu wa haki za binadamu wakipiga kelele au mabeberu wakipiga kelele
Hata mimi nilishaushtukia huu muungano. Huu ni muungano wa lazima! Hakuna kuvunja muungano kwa njia za amani!

Ukiungalia muungano una kero kibao tangu uanzishwe, lakini haziishi.

Kama kweli Wazanzibari na Watanganyika waliungana kwa hiyari, je, ni kwa nini tusiwe na nchi na serikali moja, halafu Zanzibar kukawa na mikoa tu?

Pia, kama Wazanzibar na Watanganyika wameamua kuungana, kwa nini tusiwe kitu kimoja tu, mfano, Mtanganyika aende akamiliki ardhi Zanzibar?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mleta nada kaandika uongo eti waingereza walihusika kumpindua Shamte kiongozi wa Zanzibar

Swali ni Kwa nini Shamte aliamua kukimbilia uingereza kuishi maisha yake kule?

Haiingii akilini SI angekimbilia nchi za kiarabu kwa nini aliona nchi bora ni uingereza?

Shamte hakukimbilia Uingeraza mkuu, Shamte alikaa gerezani kwa miaka 10,alikimbia baada ya kutoka gerezani.
 
Muwekezaji mkubwa na mkopeshaji mkuu wa Tanzania ni Uingereza.Hata mifumo ya serikali na mabunge yetu lazima yafanane na ya Uingereza.Usisahau kanisa la Anglikana ndo kanisa la malkia na Lina mali nyingi Zanzibar.Ukimuuliza Yeriko Nyerere Kuna barua serikali ya Tanzania iko chini ya ulezi wa Maria mama wa Yesu.

Yeriko ni mtu ambae anajiona anajua mengine kumbe hajui kitu, ni aibu kwenye Chama kwa kweli
 
SHEREHE ZA MAPINDUZI ZICHUNGUZWE

Na Sheikh Ponda Issa Ponda

IFIKAPO Januari 12, 2022, tutashuhudi watu wakisherehekea Mapinduzi yaliyofanywa visiwani Zanzibar mwaka 1964. Ni vizuri tujadili japo kwa ufupi tukio hilo.

Zanzibar ilifanya uchaguzi wa nne wa kidemokrasia (wa vyama vingi), Julai 1963. Chama kilichoshinda uchaguzi huo kilikuwa Zanzibar Nationalist Part (ZNP-ZPPP).

Uchaguzi huo ulihusisha vyama kadhhaa kikiwemo chama kikubwa cha Afroshiraz Part (ASP).

Tarehe 10, Desemba 1963, Waingereza kwa idhini ya Umoja wa Matafa, walitoa Uhuru wa Zanzibar kwa chama kilichoshinda uchaguzi huo (ZNP-ZPPP)

Siku 30 baada ya Uhuru huo, yalifanyika Mapinduzi yakidaiwa kuongozwa na chama kilichoshindwa katika uchaguzi (ASP).

Waandishi nguli wa historia, na watu mashuhuri wameeleza kuwa siku ya Mapinduzi hayo, dawati la ufundi lilishikwa na Watanganyika pamoja na Waingereza.

Wahandisi wa pande hizo mbili wakiwa Unguja, upande wa Tanganyika uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Bwana Emil Mzena na upande wa Waingereza uliwakilishwa na Balozi wao T. S. Crossthwit.

Pia wamethibitisha mipango, silaha (bunduki, mapanga) na majeshi ya Mapinduzi viliandaliwa na kuingizwa Zanzibar kutoka Tanganyika. Pia majeshi (ya majini), ya Waingereza yalionekana yakishiriki moja kwa moja katika Mapinduzi Zanzibar.

Kwa namna hiyo, Tanganyika na Uingereza walishiriki Mapinduzi hayo ya kuiondoa madarakani serikali halali ya taifa huru la Zanzibar (1964).

Aidha mwaka huohuo (1964), Jeshi la Wananchi Tanganyika lilipanga na kutekeleza Mapinduzi yaliyomuondoa Ikulu Rais Julius Kambarage Nyerere kwa zaidi ya siku mbili kabla ya kurejeshwa tena.

Mwalim Nyerere akihutubia mkutano wa hadhara Januari 25, 1964, jijini Dar es Salaam, alieleza namna alivyorudishwa madarakani:

“Nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Kikosi kikawasili sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti Waigereza wamerudi Tanganyika.”

Kwa muktadha huo, mwaka 1964, Waingereza walishiriki kupindua serikali ya Zanzibar na kuzuia Mapinduzi dhidi ya Serikali ya Tanganyika.

Mapinduzi ya Zanzibar yamehusisha mambo mengi mazito yakiwemo haya:-

Moja: Kuondolewa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi.

Pili: Kuondoshwa kiti cha Taifa hilo (Zanzibar) katika Umoja wa Mataifa (UN).

Tatu: Kuonfolewa Uhuru wa Wazanzibari kujiamulia mambo yao wenyewe.

Nne: Mauaji ya kinyama, makubwa, yaliyowaathiri wataalamu wa taifa hilo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Maulamaa wakubwa wa Kiislamu.

Tano: Ufisadi wa ubakaji wa mabinti, wake za watu na dhulma ya ardhi, mashamba, majumba na mali nyingine mbalimbali za raia.

Mmoja wa mamluki wa Mapinduzi hayo kutoka nchini Uganda, John Okelo anasema, katika Mapinduzi hayo waliwauwa Wazanzibari wapatao 11,995.

Izingatiwe kwamba, Zanzibar kabla na baada ya Uhuru palikuwa na utawala wa kikatiba na vyombo vya maamuzi ya kisheria na kisiasa kama vile Mahakama, Tume ya Uchaguzi na vingine vilikuwepo.

Serikali ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte (ZNP-ZPPP), iliyopinduliwa na Wazanzibari waliouliwa, hawakuwa na tuhuma wala hatia yoyote iliyowasilishwa na kuthibitishwa katika mamlaka hizo za serikali.

Sasa kwanini katika Twitter yangu ya tarehe 23, 2021, nilihoji Je ni nani aliyeruhusu Mapinduzi Zanzibar na kuzuia Mapinduzi Tanganyika? Pia nikauliza “alifanya hivyo kwa idhini na maslahi ya nani?

Nilihoji hayo kwa sababu mwezi ujao Januari 12, 2022, waliofanya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kusheherekea Mapinduzi yao.

Na wanahamasisha wakitaraji kuungwa mkono na watu mbalimbali wakiwemo Waislamu na Wakristo.

Mimi kama kiongozi wa dini nalazimika kuangalia matukio na sherehe hizo katika mizani ya haki, uadilifu na ubinadamu.

Katika mizani hiyo, sioni haki yoyote wala busara ya mtu anayejali hisia za utu na umoja wa umma kujifaharisha kwa Mapinduzi ya namna hiyo.

Nadhani busara ni kufanya kama waliyofanya Kanisa Katoliki nchini Rwanda kujuta na kuwaonba radhi Wanyarwanda kwa maovu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wake katika mauwaji ya kimbari mwaka (1994).

Waingereza, Watanganyika (na Wazanzibari-ASP), hawakuwa na uhalali wowote kwa yale waliyowafanyia Wazanzibari na taifa lao mwaka (1964).

Ndio maana tunasema “Mapinduzi yachunguzwe”.
Nampinga Ponda kwa kweli.
Lakini hapa kuna hoja inayopaswa kusomwa kwa tafakuri kubwa kabla haijapingwa.

Dah
 
Kwa kifupi unajaribu kusema utawala wa kiarabu urudishwe?..

Nikujuze Tu bwana mkubwa huo utawala hautorudi kamwe.. kwasababu ulivunja kila Haki ya binadamu ambayo wewe umewahi kuisikia, kama Kweli wanawapenda hao unaojupendekeza kwao kwanini mkienda Oman wanaishia kuwaua na kuwabaka Dada zetu na mbaya zaidi wakienda kushtaki hata polisi hakuna Haki wanayopata mpaka wanapofika kwenye ubalozi wetu ndo wanasaidiwa yani!!..

Hizi Dini walizotuletea ndo zimetudanganya Sana yani kama Kweli zilikuwa ni Dini wasingezitumia Dini kufanya biashara ya utumwa yani..

Namalizia Kwa kusema Bila Mapinduzi Zanzibar Leo isingetoa Raisi Mwanamke amah kiongozi yeyote mwanamke sasa wewe wadanganye wajinga ujifanye umetumwa na watu wa Oman

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
Naona umepanic bure na kutoka nje ya mada. Mleta mada anahoji kuwa nani aliyataka mapinduzi, nani aliyafanya mapinduzi na mapinduzi yalikuwa yamelenga nini?

Kama ni Uhuru, Zanzibar ilikuwa huru kabla ya mapinduzi.

Kama ni utawala wa kiraia, wazanzibar walikuwa wameshafanya uchaguzi wao na kumpata mtawala wao wanamtaka.

Kwanini mapinduzi?
Kwanini damu za watu wasiokuwa na hatia zimwagike pasipo sababu?
 
Shamte alikuwa kibaraka muhafidhina. ASP ilikuwa na nguvu na ndio maana waliungana ZNP-ZPPP ili wawashinde wazanzibar watumwa na masikini ASP
 
Hapa ndipo huwa namkumbuka marehemu sheikh ilunga alikuwa na madini nyeti saana kuhusu muungano, ukisikiliza mada zake juu ya muungano alikuwa ana jambo yule mzee

Mohamed Said leta habari zaidi.
 
Kila Mara uwa nasema humu.
MUUNGANO NI MALI YA MALKIA WA UINGEREZA.
Yeyote atakayejaribu kuugusa huu muungano ataadhibiwa na kupotezwa na hakuna mtu yeyote ndani au nje ya Tanzania atakayeongea.
Ndo maana masheikh wa uamsho sijawahi kusikia watu wa haki za binadamu wakipiga kelele au mabeberu wakipiga kelele
Na wamepotea wengi tu, kisa kuhoji huu muungano.
 
Historia ya muungano inahitaji kupitiwa upya.

Mwandishi wa kitabu cha ''Kwaheri ukoloni,kwaheri uhuru, Zanzibar na mapinduzi ya Afrabia' amejaribu kuandika yaliyofichwa ni vizuri mkisome hichi kitabu.
Kama una soft copy kitupie hapa mkuu.
 
Watu wA kubisha kila kitu,watakabwa mavi badala ya kwenda kunya watailaumu Ccm na Magufuli.
 
Kwa kifupi unajaribu kusema utawala wa kiarabu urudishwe?..

Nikujuze Tu bwana mkubwa huo utawala hautorudi kamwe.. kwasababu ulivunja kila Haki ya binadamu ambayo wewe umewahi kuisikia, kama Kweli wanawapenda hao unaojupendekeza kwao kwanini mkienda Oman wanaishia kuwaua na kuwabaka Dada zetu na mbaya zaidi wakienda kushtaki hata polisi hakuna Haki wanayopata mpaka wanapofika kwenye ubalozi wetu ndo wanasaidiwa yani!!..

Hizi Dini walizotuletea ndo zimetudanganya Sana yani kama Kweli zilikuwa ni Dini wasingezitumia Dini kufanya biashara ya utumwa yani..

Namalizia Kwa kusema Bila Mapinduzi Zanzibar Leo isingetoa Raisi Mwanamke amah kiongozi yeyote mwanamke sasa wewe wadanganye wajinga ujifanye umetumwa na watu wa Oman

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
Mkuu kwani Mohamed Shamte alikua muarabu?

Aliepinduliwa hakuwa Muarabu, tusikariri. Iliyopinduliwa ni serikali huru iliyopatikana kwa kura moja mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom