Sheikh Ponda: Sherehe za Mapinduzi zichunguzwe

Mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na wachache waliokuwa na uroho wa Madaraka, kwasababu wananchi wenyewe kwa ridhaa yao walishamchagua Sultan aongoze nchi.... Nadhani Wazanzibari kwa sasa wanachukia haya Mapinduzi yanayoshikiwa bango na sisi wabara... Hivi SULTANI angekuwepo kwa miaka 58 kweli Zanzibar ingekuwa kama hii ya sasa?
 
Kwa kifupi unajaribu kusema utawala wa kiarabu urudishwe?..

Nikujuze Tu bwana mkubwa huo utawala hautorudi kamwe.. kwasababu ulivunja kila Haki ya binadamu ambayo wewe umewahi kuisikia, kama Kweli wanawapenda hao unaojupendekeza kwao kwanini mkienda Oman wanaishia kuwaua na kuwabaka Dada zetu na mbaya zaidi wakienda kushtaki hata polisi hakuna Haki wanayopata mpaka wanapofika kwenye ubalozi wetu ndo wanasaidiwa yani!!..

Hizi Dini walizotuletea ndo zimetudanganya Sana yani kama Kweli zilikuwa ni Dini wasingezitumia Dini kufanya biashara ya utumwa yani..

Namalizia Kwa kusema Bila Mapinduzi Zanzibar Leo isingetoa Raisi Mwanamke amah kiongozi yeyote mwanamke sasa wewe wadanganye wajinga ujifanye umetumwa na watu wa Oman[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
Aliyeleta biashara ya utumwa ni kanisa na mreno
 
Huu mjadala kama una ubongo mdongo na mvivu wa kusoma huwez kuchangia kitu,issue ni historia iandikwe upya,mapinduz yalikuwa haramu,ndo maana waliopindua hadi leo hawajaweza kukaa kwa amani,hawaminiani wenyewe kwa wenyewe!!
 
Kwenye siasa hakunaga kuaminiana popote ulimwenguni sio zenji tu hata kwa mabwana zenu waarabu.
 
Kati yako na ponda nan mjinga? Huo utumwa kwann hadi saii tukiwatafuta hao walochukuliwa utumwa hatuwakuti uarabuni bali wapo america na ulaya? Waarabu walikuja africa miaka elfu kabla mzungu hajaja kwann huo utumwa uje utokee baada ya mzungu kuja? Fikra yako mgando unaona kutawaliwa na mwanamke ndo maendeleo?
Walihasiwa
 
Mapinduzi ya Zanzibar yalifanywa na wachache waliokuwa na uroho wa Madaraka, kwasababu wananchi wenyewe kwa ridhaa yao walishamchagua Sultan aongoze nchi.... Nadhani Wazanzibari kwa sasa wanachukia haya Mapinduzi yanayoshikiwa bango na sisi wabara... Hivi SULTANI angekuwepo kwa miaka 58 kweli Zanzibar ingekuwa kama hii ya sasa?
Kumbe walikuwa wanawapenda waarabu ?
 
SHEREHE ZA MAPINDUZI ZICHUNGUZWE

Na Sheikh Ponda Issa Ponda

IFIKAPO Januari 12, 2022, tutashuhudi watu wakisherehekea Mapinduzi yaliyofanywa visiwani Zanzibar mwaka 1964. Ni vizuri tujadili japo kwa ufupi tukio hilo.

Zanzibar ilifanya uchaguzi wa nne wa kidemokrasia (wa vyama vingi), Julai 1963. Chama kilichoshinda uchaguzi huo kilikuwa Zanzibar Nationalist Part (ZNP-ZPPP).

Uchaguzi huo ulihusisha vyama kadhhaa kikiwemo chama kikubwa cha Afroshiraz Part (ASP).

Tarehe 10, Desemba 1963, Waingereza kwa idhini ya Umoja wa Matafa, walitoa Uhuru wa Zanzibar kwa chama kilichoshinda uchaguzi huo (ZNP-ZPPP)

Siku 30 baada ya Uhuru huo, yalifanyika Mapinduzi yakidaiwa kuongozwa na chama kilichoshindwa katika uchaguzi (ASP).

Waandishi nguli wa historia, na watu mashuhuri wameeleza kuwa siku ya Mapinduzi hayo, dawati la ufundi lilishikwa na Watanganyika pamoja na Waingereza.

Wahandisi wa pande hizo mbili wakiwa Unguja, upande wa Tanganyika uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Bwana Emil Mzena na upande wa Waingereza uliwakilishwa na Balozi wao T. S. Crossthwit.

Pia wamethibitisha mipango, silaha (bunduki, mapanga) na majeshi ya Mapinduzi viliandaliwa na kuingizwa Zanzibar kutoka Tanganyika. Pia majeshi (ya majini), ya Waingereza yalionekana yakishiriki moja kwa moja katika Mapinduzi Zanzibar.

Kwa namna hiyo, Tanganyika na Uingereza walishiriki Mapinduzi hayo ya kuiondoa madarakani serikali halali ya taifa huru la Zanzibar (1964).

Aidha mwaka huohuo (1964), Jeshi la Wananchi Tanganyika lilipanga na kutekeleza Mapinduzi yaliyomuondoa Ikulu Rais Julius Kambarage Nyerere kwa zaidi ya siku mbili kabla ya kurejeshwa tena.

Mwalim Nyerere akihutubia mkutano wa hadhara Januari 25, 1964, jijini Dar es Salaam, alieleza namna alivyorudishwa madarakani:

“Nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Kikosi kikawasili sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti Waigereza wamerudi Tanganyika.”

Kwa muktadha huo, mwaka 1964, Waingereza walishiriki kupindua serikali ya Zanzibar na kuzuia Mapinduzi dhidi ya Serikali ya Tanganyika.

Mapinduzi ya Zanzibar yamehusisha mambo mengi mazito yakiwemo haya:-

Moja: Kuondolewa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi.

Pili: Kuondoshwa kiti cha Taifa hilo (Zanzibar) katika Umoja wa Mataifa (UN).

Tatu: Kuonfolewa Uhuru wa Wazanzibari kujiamulia mambo yao wenyewe.

Nne: Mauaji ya kinyama, makubwa, yaliyowaathiri wataalamu wa taifa hilo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Maulamaa wakubwa wa Kiislamu.

Tano: Ufisadi wa ubakaji wa mabinti, wake za watu na dhulma ya ardhi, mashamba, majumba na mali nyingine mbalimbali za raia.

Mmoja wa mamluki wa Mapinduzi hayo kutoka nchini Uganda, John Okelo anasema, katika Mapinduzi hayo waliwauwa Wazanzibari wapatao 11,995.

Izingatiwe kwamba, Zanzibar kabla na baada ya Uhuru palikuwa na utawala wa kikatiba na vyombo vya maamuzi ya kisheria na kisiasa kama vile Mahakama, Tume ya Uchaguzi na vingine vilikuwepo.

Serikali ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte (ZNP-ZPPP), iliyopinduliwa na Wazanzibari waliouliwa, hawakuwa na tuhuma wala hatia yoyote iliyowasilishwa na kuthibitishwa katika mamlaka hizo za serikali.

Sasa kwanini katika Twitter yangu ya tarehe 23, 2021, nilihoji Je ni nani aliyeruhusu Mapinduzi Zanzibar na kuzuia Mapinduzi Tanganyika? Pia nikauliza “alifanya hivyo kwa idhini na maslahi ya nani?

Nilihoji hayo kwa sababu mwezi ujao Januari 12, 2022, waliofanya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kusheherekea Mapinduzi yao.

Na wanahamasisha wakitaraji kuungwa mkono na watu mbalimbali wakiwemo Waislamu na Wakristo.

Mimi kama kiongozi wa dini nalazimika kuangalia matukio na sherehe hizo katika mizani ya haki, uadilifu na ubinadamu.

Katika mizani hiyo, sioni haki yoyote wala busara ya mtu anayejali hisia za utu na umoja wa umma kujifaharisha kwa Mapinduzi ya namna hiyo.

Nadhani busara ni kufanya kama waliyofanya Kanisa Katoliki nchini Rwanda kujuta na kuwaonba radhi Wanyarwanda kwa maovu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wake katika mauwaji ya kimbari mwaka (1994).

Waingereza, Watanganyika (na Wazanzibari-ASP), hawakuwa na uhalali wowote kwa yale waliyowafanyia Wazanzibari na taifa lao mwaka (1964).

Ndio maana tunasema “Mapinduzi yachunguzwe”.
Na mapinduzi yanaendelea kila uchaguzi hadi nyakati hizi! ASP, TANu na sasa CCM havijawahi kukubalika visiwani, ni mapinduzi tu na madhila yake ndio vinawaweka madarakani! Wenzetu Wana msimamo sana, sema dola isyo na utu, ndio inawakandamiza.
Katiba mpya muhimu!
 
tatizo lako uelewa mdogo sana unao sukuwa na chuki hapa dini inaigiaje? hao walio shirikiana kumpindua surutani wakatawala walikuwa dini gani? mwenzako katoa maoni yake na wewe jibu kwa hoja sio kuja hapa kupakaza matapishi kwa watu
 
Historia imefichwa na kufungwa kama bidhaa haramu. Ukweli hauelezwi na uongo unafundishwa hadi darasani. Mapinduzi Zanzibar picha za watawala waliopo madarakani zimetamalaki kuliko picha za John Gideon Okello na wenzake. Abeid Karume aliyekuwa DSM siku ya mapinduzi anaitwa shujaa
20230116_042513.jpg
20230116_042518.jpg
 
SHEREHE ZA MAPINDUZI ZICHUNGUZWE

Na Sheikh Ponda Issa Ponda

IFIKAPO Januari 12, 2022, tutashuhudi watu wakisherehekea Mapinduzi yaliyofanywa visiwani Zanzibar mwaka 1964. Ni vizuri tujadili japo kwa ufupi tukio hilo.

Zanzibar ilifanya uchaguzi wa nne wa kidemokrasia (wa vyama vingi), Julai 1963. Chama kilichoshinda uchaguzi huo kilikuwa Zanzibar Nationalist Part (ZNP-ZPPP).

Uchaguzi huo ulihusisha vyama kadhhaa kikiwemo chama kikubwa cha Afroshiraz Part (ASP).

Tarehe 10, Desemba 1963, Waingereza kwa idhini ya Umoja wa Matafa, walitoa Uhuru wa Zanzibar kwa chama kilichoshinda uchaguzi huo (ZNP-ZPPP)

Siku 30 baada ya Uhuru huo, yalifanyika Mapinduzi yakidaiwa kuongozwa na chama kilichoshindwa katika uchaguzi (ASP).

Waandishi nguli wa historia, na watu mashuhuri wameeleza kuwa siku ya Mapinduzi hayo, dawati la ufundi lilishikwa na Watanganyika pamoja na Waingereza.

Wahandisi wa pande hizo mbili wakiwa Unguja, upande wa Tanganyika uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Bwana Emil Mzena na upande wa Waingereza uliwakilishwa na Balozi wao T. S. Crossthwit.

Pia wamethibitisha mipango, silaha (bunduki, mapanga) na majeshi ya Mapinduzi viliandaliwa na kuingizwa Zanzibar kutoka Tanganyika. Pia majeshi (ya majini), ya Waingereza yalionekana yakishiriki moja kwa moja katika Mapinduzi Zanzibar.

Kwa namna hiyo, Tanganyika na Uingereza walishiriki Mapinduzi hayo ya kuiondoa madarakani serikali halali ya taifa huru la Zanzibar (1964).

Aidha mwaka huohuo (1964), Jeshi la Wananchi Tanganyika lilipanga na kutekeleza Mapinduzi yaliyomuondoa Ikulu Rais Julius Kambarage Nyerere kwa zaidi ya siku mbili kabla ya kurejeshwa tena.

Mwalim Nyerere akihutubia mkutano wa hadhara Januari 25, 1964, jijini Dar es Salaam, alieleza namna alivyorudishwa madarakani:

“Nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Kikosi kikawasili sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti Waigereza wamerudi Tanganyika.”

Kwa muktadha huo, mwaka 1964, Waingereza walishiriki kupindua serikali ya Zanzibar na kuzuia Mapinduzi dhidi ya Serikali ya Tanganyika.

Mapinduzi ya Zanzibar yamehusisha mambo mengi mazito yakiwemo haya:-

Moja: Kuondolewa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi.

Pili: Kuondoshwa kiti cha Taifa hilo (Zanzibar) katika Umoja wa Mataifa (UN).

Tatu: Kuonfolewa Uhuru wa Wazanzibari kujiamulia mambo yao wenyewe.

Nne: Mauaji ya kinyama, makubwa, yaliyowaathiri wataalamu wa taifa hilo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Maulamaa wakubwa wa Kiislamu.

Tano: Ufisadi wa ubakaji wa mabinti, wake za watu na dhulma ya ardhi, mashamba, majumba na mali nyingine mbalimbali za raia.

Mmoja wa mamluki wa Mapinduzi hayo kutoka nchini Uganda, John Okelo anasema, katika Mapinduzi hayo waliwauwa Wazanzibari wapatao 11,995.

Izingatiwe kwamba, Zanzibar kabla na baada ya Uhuru palikuwa na utawala wa kikatiba na vyombo vya maamuzi ya kisheria na kisiasa kama vile Mahakama, Tume ya Uchaguzi na vingine vilikuwepo.

Serikali ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte (ZNP-ZPPP), iliyopinduliwa na Wazanzibari waliouliwa, hawakuwa na tuhuma wala hatia yoyote iliyowasilishwa na kuthibitishwa katika mamlaka hizo za serikali.

Sasa kwanini katika Twitter yangu ya tarehe 23, 2021, nilihoji Je ni nani aliyeruhusu Mapinduzi Zanzibar na kuzuia Mapinduzi Tanganyika? Pia nikauliza “alifanya hivyo kwa idhini na maslahi ya nani?

Nilihoji hayo kwa sababu mwezi ujao Januari 12, 2022, waliofanya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kusheherekea Mapinduzi yao.

Na wanahamasisha wakitaraji kuungwa mkono na watu mbalimbali wakiwemo Waislamu na Wakristo.

Mimi kama kiongozi wa dini nalazimika kuangalia matukio na sherehe hizo katika mizani ya haki, uadilifu na ubinadamu.

Katika mizani hiyo, sioni haki yoyote wala busara ya mtu anayejali hisia za utu na umoja wa umma kujifaharisha kwa Mapinduzi ya namna hiyo.

Nadhani busara ni kufanya kama waliyofanya Kanisa Katoliki nchini Rwanda kujuta na kuwaonba radhi Wanyarwanda kwa maovu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wake katika mauwaji ya kimbari mwaka (1994).

Waingereza, Watanganyika (na Wazanzibari-ASP), hawakuwa na uhalali wowote kwa yale waliyowafanyia Wazanzibari na taifa lao mwaka (1964).

Ndio maana tunasema “Mapinduzi yachunguzwe”.
Huyu mrundi si akayaseme haya huko kwao Burundi
 
Kila Mara uwa nasema humu.
MUUNGANO NI MALI YA MALKIA WA UINGEREZA.
Yeyote atakayejaribu kuugusa huu muungano ataadhibiwa na kupotezwa na hakuna mtu yeyote ndani au nje ya Tanzania atakayeongea.
Ndo maana masheikh wa uamsho sijawahi kusikia watu wa haki za binadamu wakipiga kelele au mabeberu wakipiga kelele
aijawai kutokea nchi yoyote hata wakiuwawa masheikh wote hakuna wa kulalamika wawe na makosa au kuonewa
 
Kuna watu wako tayari kuwa wafuasi wa waarabu au wazungu kuumiza WaAfrica wenzao wakijiona nao Waarabu au Wazungu kwasababu tu ni wafuasi wa dini walizoletewa na hao mabwana...
hapa hatuongelei dini kwani wanao tawala zanziba ni dini gani kama kigezo ni dini? hawa wanaofisadi nchi na kujitajirisha kwa jasho la watu masikini waarabu walio tawala zanzibar?
 
Back
Top Bottom