Sheikh Ponda: Sherehe za Mapinduzi zichunguzwe

Sheikh Ponda: Sherehe za Mapinduzi zichunguzwe

Kabisa yani.. hapo ndo utajua kuwa damu ya wale machifu waliotumiwa kuingiza wazungu kufanya utumwa bado Ipo miongoni mwetu yani pamoja na kufundishwa Sana watu bado hawaelewi yani.. wewe Kuoa Tu ngozi nyeupe kwenye ukoo wao wanaona umewaletea nuksi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hajiulizi kwanini Uarabuni hakuna Black Arabs wakati walipelekwa wengi kipindi cha utumwa sema walifanywa kuwa mahanithi yani.. MTU ambae hajawahi kutamani uzao wako uendelee kuishi ni hatari kuliko neno lenyewe.

Kwa kipindi hiku kufanywa hanithi sio mpaka ubanwe mangende.. kupitia vyakula Tu inatosha kuongeza idadi ya mahanithi

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
kwani hawa wanao tuminya makande kwa kujilimbikizia mali kisha kwenda kuficha kwa walami kisha watoto wao na ndugu zao wakaishi kama wafalume mimi na wewe tukaishia kumiywa kulipa madeni hayo mpaka mababu hao nao ni waarabu ???????
 
KWA ASILI TANGU MWANZO ZANZIBAR NA PEMBA NI NCHI YA WAAFRIKA(PURE AFRICANS)

Taabu ilianza tu baada ya waarab kuchovya chovya dada zetu damu yao tena karibia zote ni haramu,
na kusambaza machotara visiwani humo, mbaya visiwa ni vidogo sana..

Hapo sasa uhasama , ubaguzi, unyanyasaji, utumwa ukaanza dhidi ya wenye nchi wenyewe hadi kutaka wawatawale...

Tuwaombe tu hao waarabu wawachukue hizo damu zao walizotelekeza hapa wazipeleke huko kwao si wanayo nchi yao ? ? ili watuaachie nchi yetu kwa waafrika wenye nayo ! ! !


Uliona wapi mtoto wa nje na haramu akarithi mji na ukoo ?

Mbona huko Lamu, Mombasa hawayasemi haya ? na huko walichovya chovya hivyo hivyo
ubagusi sio kwa muarabu tu hata muzungu nae anatubagua kupitia vibaraka walio waandaa wanao tufanya tuishi kwa dhiki huku wao wakiishi kifalume kwa kodi zetu wao wakitibiwa hosipital nzuli na wtoto wao kusoma shele yenye wanafuzi 35 walimu wakutosha magali maziwa yakumwaga mpaka madakitali hiwapo mtoto wao akiugua watoto wetu wanakosoma kaangalie awa watala nao ni waarabu?
 
Okello wodwa jo-tz nepok oluongo nyingi ei Nyasi mora mora mar Mapinduzi to in emaniriembo Shamte...
 
SHEREHE ZA MAPINDUZI ZICHUNGUZWE

Na Sheikh Ponda Issa Ponda

IFIKAPO Januari 12, 2022, tutashuhudi watu wakisherehekea Mapinduzi yaliyofanywa visiwani Zanzibar mwaka 1964. Ni vizuri tujadili japo kwa ufupi tukio hilo.

Zanzibar ilifanya uchaguzi wa nne wa kidemokrasia (wa vyama vingi), Julai 1963. Chama kilichoshinda uchaguzi huo kilikuwa Zanzibar Nationalist Part (ZNP-ZPPP).

Uchaguzi huo ulihusisha vyama kadhhaa kikiwemo chama kikubwa cha Afroshiraz Part (ASP).

Tarehe 10, Desemba 1963, Waingereza kwa idhini ya Umoja wa Matafa, walitoa Uhuru wa Zanzibar kwa chama kilichoshinda uchaguzi huo (ZNP-ZPPP)

Siku 30 baada ya Uhuru huo, yalifanyika Mapinduzi yakidaiwa kuongozwa na chama kilichoshindwa katika uchaguzi (ASP).

Waandishi nguli wa historia, na watu mashuhuri wameeleza kuwa siku ya Mapinduzi hayo, dawati la ufundi lilishikwa na Watanganyika pamoja na Waingereza.

Wahandisi wa pande hizo mbili wakiwa Unguja, upande wa Tanganyika uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Bwana Emil Mzena na upande wa Waingereza uliwakilishwa na Balozi wao T. S. Crossthwit.

Pia wamethibitisha mipango, silaha (bunduki, mapanga) na majeshi ya Mapinduzi viliandaliwa na kuingizwa Zanzibar kutoka Tanganyika. Pia majeshi (ya majini), ya Waingereza yalionekana yakishiriki moja kwa moja katika Mapinduzi Zanzibar.

Kwa namna hiyo, Tanganyika na Uingereza walishiriki Mapinduzi hayo ya kuiondoa madarakani serikali halali ya taifa huru la Zanzibar (1964).

Aidha mwaka huohuo (1964), Jeshi la Wananchi Tanganyika lilipanga na kutekeleza Mapinduzi yaliyomuondoa Ikulu Rais Julius Kambarage Nyerere kwa zaidi ya siku mbili kabla ya kurejeshwa tena.

Mwalim Nyerere akihutubia mkutano wa hadhara Januari 25, 1964, jijini Dar es Salaam, alieleza namna alivyorudishwa madarakani:

“Nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Kikosi kikawasili sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti Waigereza wamerudi Tanganyika.”

Kwa muktadha huo, mwaka 1964, Waingereza walishiriki kupindua serikali ya Zanzibar na kuzuia Mapinduzi dhidi ya Serikali ya Tanganyika.

Mapinduzi ya Zanzibar yamehusisha mambo mengi mazito yakiwemo haya:-

Moja: Kuondolewa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi.

Pili: Kuondoshwa kiti cha Taifa hilo (Zanzibar) katika Umoja wa Mataifa (UN).

Tatu: Kuonfolewa Uhuru wa Wazanzibari kujiamulia mambo yao wenyewe.

Nne: Mauaji ya kinyama, makubwa, yaliyowaathiri wataalamu wa taifa hilo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Maulamaa wakubwa wa Kiislamu.

Tano: Ufisadi wa ubakaji wa mabinti, wake za watu na dhulma ya ardhi, mashamba, majumba na mali nyingine mbalimbali za raia.

Mmoja wa mamluki wa Mapinduzi hayo kutoka nchini Uganda, John Okelo anasema, katika Mapinduzi hayo waliwauwa Wazanzibari wapatao 11,995.

Izingatiwe kwamba, Zanzibar kabla na baada ya Uhuru palikuwa na utawala wa kikatiba na vyombo vya maamuzi ya kisheria na kisiasa kama vile Mahakama, Tume ya Uchaguzi na vingine vilikuwepo.

Serikali ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte (ZNP-ZPPP), iliyopinduliwa na Wazanzibari waliouliwa, hawakuwa na tuhuma wala hatia yoyote iliyowasilishwa na kuthibitishwa katika mamlaka hizo za serikali.

Sasa kwanini katika Twitter yangu ya tarehe 23, 2021, nilihoji Je ni nani aliyeruhusu Mapinduzi Zanzibar na kuzuia Mapinduzi Tanganyika? Pia nikauliza “alifanya hivyo kwa idhini na maslahi ya nani?

Nilihoji hayo kwa sababu mwezi ujao Januari 12, 2022, waliofanya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kusheherekea Mapinduzi yao.

Na wanahamasisha wakitaraji kuungwa mkono na watu mbalimbali wakiwemo Waislamu na Wakristo.

Mimi kama kiongozi wa dini nalazimika kuangalia matukio na sherehe hizo katika mizani ya haki, uadilifu na ubinadamu.

Katika mizani hiyo, sioni haki yoyote wala busara ya mtu anayejali hisia za utu na umoja wa umma kujifaharisha kwa Mapinduzi ya namna hiyo.

Nadhani busara ni kufanya kama waliyofanya Kanisa Katoliki nchini Rwanda kujuta na kuwaonba radhi Wanyarwanda kwa maovu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wake katika mauwaji ya kimbari mwaka (1994).

Waingereza, Watanganyika (na Wazanzibari-ASP), hawakuwa na uhalali wowote kwa yale waliyowafanyia Wazanzibari na taifa lao mwaka (1964).

Ndio maana tunasema “Mapinduzi yachunguzwe”.
Sio sherehe ya mapinduzi tu, hata vita ya Uganda inabidi ichunguzwe maana kuna tetesi za kuaondolewa kwa Iddi Amini kwa sababu ya kutaka kuifanya uganda kuwa nchi ya kiislamu
 
Sio sherehe ya mapinduzi tu, hata vita ya Uganda inabidi ichunguzwe maana kuna tetesi za kuaondolewa kwa Iddi Amini kwa sababu ya kutaka kuifanya uganda kuwa nchi ya kiislamu

Achana na upuuzi wa ponda,vita vya uganda ni halali kabisa na ni vya kisiasa mana nduli alianza chokochoko zake kule kagera ulitaka aachwe tu ajichukulie kagera kama yake. ?
 
Back
Top Bottom