Sheikh Ponda: Sherehe za Mapinduzi zichunguzwe

Sep 19, 2019
43
383
SHEREHE ZA MAPINDUZI ZICHUNGUZWE

Na Sheikh Ponda Issa Ponda

IFIKAPO Januari 12, 2022, tutashuhudi watu wakisherehekea Mapinduzi yaliyofanywa visiwani Zanzibar mwaka 1964. Ni vizuri tujadili japo kwa ufupi tukio hilo.

Zanzibar ilifanya uchaguzi wa nne wa kidemokrasia (wa vyama vingi), Julai 1963. Chama kilichoshinda uchaguzi huo kilikuwa Zanzibar Nationalist Part (ZNP-ZPPP).

Uchaguzi huo ulihusisha vyama kadhhaa kikiwemo chama kikubwa cha Afroshiraz Part (ASP).

Tarehe 10, Desemba 1963, Waingereza kwa idhini ya Umoja wa Matafa, walitoa Uhuru wa Zanzibar kwa chama kilichoshinda uchaguzi huo (ZNP-ZPPP)

Siku 30 baada ya Uhuru huo, yalifanyika Mapinduzi yakidaiwa kuongozwa na chama kilichoshindwa katika uchaguzi (ASP).

Waandishi nguli wa historia, na watu mashuhuri wameeleza kuwa siku ya Mapinduzi hayo, dawati la ufundi lilishikwa na Watanganyika pamoja na Waingereza.

Wahandisi wa pande hizo mbili wakiwa Unguja, upande wa Tanganyika uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Bwana Emil Mzena na upande wa Waingereza uliwakilishwa na Balozi wao T. S. Crossthwit.

Pia wamethibitisha mipango, silaha (bunduki, mapanga) na majeshi ya Mapinduzi viliandaliwa na kuingizwa Zanzibar kutoka Tanganyika. Pia majeshi (ya majini), ya Waingereza yalionekana yakishiriki moja kwa moja katika Mapinduzi Zanzibar.

Kwa namna hiyo, Tanganyika na Uingereza walishiriki Mapinduzi hayo ya kuiondoa madarakani serikali halali ya taifa huru la Zanzibar (1964).

Aidha mwaka huohuo (1964), Jeshi la Wananchi Tanganyika lilipanga na kutekeleza Mapinduzi yaliyomuondoa Ikulu Rais Julius Kambarage Nyerere kwa zaidi ya siku mbili kabla ya kurejeshwa tena.

Mwalim Nyerere akihutubia mkutano wa hadhara Januari 25, 1964, jijini Dar es Salaam, alieleza namna alivyorudishwa madarakani:

“Nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Kikosi kikawasili sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti Waigereza wamerudi Tanganyika.”

Kwa muktadha huo, mwaka 1964, Waingereza walishiriki kupindua serikali ya Zanzibar na kuzuia Mapinduzi dhidi ya Serikali ya Tanganyika.

Mapinduzi ya Zanzibar yamehusisha mambo mengi mazito yakiwemo haya:-

Moja: Kuondolewa madarakani serikali iliyochaguliwa na wananchi.

Pili: Kuondoshwa kiti cha Taifa hilo (Zanzibar) katika Umoja wa Mataifa (UN).

Tatu: Kuonfolewa Uhuru wa Wazanzibari kujiamulia mambo yao wenyewe.

Nne: Mauaji ya kinyama, makubwa, yaliyowaathiri wataalamu wa taifa hilo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Maulamaa wakubwa wa Kiislamu.

Tano: Ufisadi wa ubakaji wa mabinti, wake za watu na dhulma ya ardhi, mashamba, majumba na mali nyingine mbalimbali za raia.

Mmoja wa mamluki wa Mapinduzi hayo kutoka nchini Uganda, John Okelo anasema, katika Mapinduzi hayo waliwauwa Wazanzibari wapatao 11,995.

Izingatiwe kwamba, Zanzibar kabla na baada ya Uhuru palikuwa na utawala wa kikatiba na vyombo vya maamuzi ya kisheria na kisiasa kama vile Mahakama, Tume ya Uchaguzi na vingine vilikuwepo.

Serikali ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte (ZNP-ZPPP), iliyopinduliwa na Wazanzibari waliouliwa, hawakuwa na tuhuma wala hatia yoyote iliyowasilishwa na kuthibitishwa katika mamlaka hizo za serikali.

Sasa kwanini katika Twitter yangu ya tarehe 23, 2021, nilihoji Je ni nani aliyeruhusu Mapinduzi Zanzibar na kuzuia Mapinduzi Tanganyika? Pia nikauliza “alifanya hivyo kwa idhini na maslahi ya nani?

Nilihoji hayo kwa sababu mwezi ujao Januari 12, 2022, waliofanya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kusheherekea Mapinduzi yao.

Na wanahamasisha wakitaraji kuungwa mkono na watu mbalimbali wakiwemo Waislamu na Wakristo.

Mimi kama kiongozi wa dini nalazimika kuangalia matukio na sherehe hizo katika mizani ya haki, uadilifu na ubinadamu.

Katika mizani hiyo, sioni haki yoyote wala busara ya mtu anayejali hisia za utu na umoja wa umma kujifaharisha kwa Mapinduzi ya namna hiyo.

Nadhani busara ni kufanya kama waliyofanya Kanisa Katoliki nchini Rwanda kujuta na kuwaonba radhi Wanyarwanda kwa maovu yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wake katika mauwaji ya kimbari mwaka (1994).

Waingereza, Watanganyika (na Wazanzibari-ASP), hawakuwa na uhalali wowote kwa yale waliyowafanyia Wazanzibari na taifa lao mwaka (1964).

Ndio maana tunasema “Mapinduzi yachunguzwe”.
 
Kwa kifupi unajaribu kusema utawala wa kiarabu urudishwe?..

Nikujuze Tu bwana mkubwa huo utawala hautorudi kamwe.. kwasababu ulivunja kila Haki ya binadamu ambayo wewe umewahi kuisikia, kama Kweli wanawapenda hao unaojupendekeza kwao kwanini mkienda Oman wanaishia kuwaua na kuwabaka Dada zetu na mbaya zaidi wakienda kushtaki hata polisi hakuna Haki wanayopata mpaka wanapofika kwenye ubalozi wetu ndo wanasaidiwa yani!!..

Hizi Dini walizotuletea ndo zimetudanganya Sana yani kama Kweli zilikuwa ni Dini wasingezitumia Dini kufanya biashara ya utumwa yani..

Namalizia Kwa kusema Bila Mapinduzi Zanzibar Leo isingetoa Raisi Mwanamke amah kiongozi yeyote mwanamke sasa wewe wadanganye wajinga ujifanye umetumwa na watu wa Oman

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 
  • Zanzibar mmezidi sana unyoronyoro. Mmepigana vita dakika 45 mkanyoosha mikono juu. Yaani dunia iliwashangaeni sana 1896
  • Hamkutoa kabisa resistance kwa wavamizi wanardhi yenu mkaruhusu hadi mapinduzi yafanyike mwaka 1963

Tumetoka mbali na bado!

IMG_20211225_093056_062.jpg

“Nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Kikosi kikawasili sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti Waigereza wamerudi Tanganyika.”
 
Kila Mara uwa nasema humu.
MUUNGANO NI MALI YA MALKIA WA UINGEREZA.
Yeyote atakayejaribu kuugusa huu muungano ataadhibiwa na kupotezwa na hakuna mtu yeyote ndani au nje ya Tanzania atakayeongea.
Ndo maana masheikh wa uamsho sijawahi kusikia watu wa haki za binadamu wakipiga kelele au mabeberu wakipiga kelele
 
Kwa kifupi unajaribu kusema utawala wa kiarabu urudishwe?..

Nikujuze Tu bwana mkubwa huo utawala hautorudi kamwe.. kwasababu ulivunja kila Haki ya binadamu ambayo wewe umewahi kuisikia, kama Kweli wanawapenda hao unaojupendekeza kwao kwanini mkienda Oman wanaishia kuwaua na kuwabaka Dada zetu na mbaya zaidi wakienda kushtaki hata polisi hakuna Haki wanayopata mpaka wanapofika kwenye ubalozi wetu ndo wanasaidiwa yani!!..

Hizi Dini walizotuletea ndo zimetudanganya Sana yani kama Kweli zilikuwa ni Dini wasingezitumia Dini kufanya biashara ya utumwa yani..

Namalizia Kwa kusema Bila Mapinduzi Zanzibar Leo isingetoa Raisi Mwanamke amah kiongozi yeyote mwanamke sasa wewe wadanganye wajinga ujifanye umetumwa na watu wa Oman

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
Unatumia kichwa kufuga makamasi kwa uwezo wako ulionao usijaribu kuvuka barabara ukiwa peke yako...
 
Huyu shekh ponda anataka kuzidi Sasa.. Siyo wa kumchekea huyu...
 
Historia ya muungano inahitaji kupitiwa upya.

Mwandishi wa kitabu cha ''Kwaheri ukoloni,kwaheri uhuru, Zanzibar na mapinduzi ya Afrabia' amejaribu kuandika yaliyofichwa ni vizuri mkisome hichi kitabu.
 
Kuna watu wako tayari kuwa wafuasi wa waarabu au wazungu kuumiza WaAfrica wenzao wakijiona nao Waarabu au Wazungu kwasababu tu ni wafuasi wa dini walizoletewa na hao mabwana...
 
Ni bahati mbaya tu viongozi waliokuwepo kipindi hicho na kushika madaraka makubwa, hawataki kuandika UKWELI juu ya safakasi za Muungano!

Mohamed Said unalakutia jambo hapa?
 
Back
Top Bottom