*Wadai damu, mate na nywele
WAKATI Katibu wa Jumuiyana Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiendelea kuuguza jeraha linalodaiwa kutokana na risasi katika mahabusu ya Segerea, jijini Dar es Salaam, wingu jingine la mashaka limeizunguka familia yake. Mashaka hayoyanatokana na kitendo chamakachero wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakiwemo wale wa Uhamiaji kudaiwa kuvamianyumbani kwa wazazi wake, Ujiji mkoani Kigoma,kwa nia ya kuilazimisha familia yake wachukuliwe damu kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA).
MTANZANIA Jumapili limedokezwa kuwa kabla na baada ya tukio la sasa la Sheikh Ponda kupigwa risasi, makachero hao wamejaribu kuifikia familiahiyo ya Ponda kwa takribani mara tano bila mafanikio yoyote.
Mmoja wa wanafamilia hao ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini akihofia usalama wake, amelidokeza MTANZANIA Jumapili kwamba makachero hao baada ya kushindwa kuwashawishi kutoa damu, wakataka wapatiwe mate au nywele kwa ajili ya kufanyia kipimo hicho iwa ajili ya kufanyia kipimo hicho ili kutambua kama Ponda ni ndugu yao na pia ni raia wa Tanzania.
"Tulikwisha shawishiwa sana, wakati fulani walitukatia hadi tiketi za ndege ili tuje Dar es Salaam kwa ajili ya kipimo hicho pamoja na kufanya mahojiano maalumu, lakinitulikataa, kwa sababu hawa jamaa wanaogopesha," alisema mwanafamilia huyo.
Alisema baada ya kukataa kutoa damu, ndipo walipofika kwa mara nyingine tena wakitaka kuchukua nywele za mamayake mzazi Ponda pamoja na za baadhi ya ndugu zake, lakini hilo nalo likashindikana baada ya wao kugoma.
"Tangu Sheikh Ponda aumizwe mama yake mzazi amekuwa mgonjwa,baada ya kupokea taarifa hizo kwa mshituko, hata hivyo familia kwa ujumla haina uhuru tena kwa sababu imekuwa ikifuatwafuatwana makachero hao pamoja na watu wa Uhamiaji.
"Kwa kweli hofu imetanda katika familia yetu na hatujui nini kinafuata kutokana na kuendelea kufuatiliwa na makachero, kwa mfano ile hatua ya kupewa tiketi ili kwenda Dar es Salaam ilitufanya tushituke kwa hofu ya kwamba labda kuna mpango wa kudhuru maisha yetu, wamekwisha kuja mara nyingi, wameomba mpaka kitabu wamekitoa mpaka nakala, alichoandika Sheikh Ponda,kinaitwa ‘Tanu mkoani Kigoma mwaka 1954'," alisema mwanafamilia huyo.
Wakati taarifa hizo zikiibuka sasa, kwa muda mrefu sasa kumekuwapo na habari za kukanganya juu ya asili ya Sheikh Ponda Issa Ponda, wengine wakidai kuwa ni raia wa nchini Burundi, taifa ambalo linapakana namkoa wa Kigoma, sehemu inayoelezwa ndiko alikozaliwa. Hata hivyo ndugu zake wanadai kuwawao ni raia halali wa Tanzania.
Wakati huo huo, chanzo kingine cha habari kimelidokezea gazeti hili jinsi Sheikh Ponda alivyofanikiwa kuwakwepa polisi Zanzibar, baada ya kudaiwa kutoa kauli za uchochezi katika mhadhara wa Kiislamu wakati wakiwa visiwani humo.
Inadaiwa kwamba Sheikh Ponda kabla ya kuhutubia mhadhara huo alipita gerezani kumuona kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed.
Kwamba baada ya kumaliza kuhutubia mhadhara huo, alianza safari ya kuelekea katika msikiti wa Mbuyuni.
Chanzo: Mtanzania.