Ndugu zangu Watanzania,
Ni kweli vitendo vya uvunjifu wa amani hapa nchini vyatuudhi sote wenye busara bila kujali dini zetu. Vitendo hivi vina ajenda ya siri iliyojificha sana. bahati mbaya watanzania wengi wakiwemo hata viongozi wetu wa serikali na dola zake wanachukulia juu juu ghasia hizi. Chimbuko lake liko mbali sana zaidi ya dini zetu. Tuelewe kwamba baada ya kuanguka kwa dola la Soveat (USSR) ambayo ilikuwa inajaribu kuleta ahueni katika nchi zetu, sasa nchi kubwa (Wakubwa kama alivyokuwa anawita Mwalim Nyerere) wanaanza kugawana nchi zetu hizi changa lakini Mungu kazijalia kwa utajiri wake kama mafuta, madini na fursa zingine za uchumi. Wakubwa hawa wanataka kurudisha ukoloni lakini hasa ukoloni mambo leo. Wanataka kumiliki uchumi wa dunia kwa kuwa kwao uchumi unaanza kuyumba. Ghasia zote tunazoshuhudia nchi za kiarabu zinatokana na utajiri wao wa mafuta pamoja na viongozi wao kutokubali kuwa mifukoni mwa Wakubwa hawa. Angalia nchi kama Saudi Arabia na Kuwait kwanini hawana mgogoro huo wakati nao hawana demokrasia kama Libya, Iraq,Siria n.k. Nani asiyejua kuwa Saudia na Kuwait wamo mifukoni mwa Marekani na uchumi wao wote unamilikiwa na wamerekani. Visima vya Mafuta vimo mikononi mwao. Wanachota mafuta wanavyotaka. Ole wao watakapobadili msimamo.
Hawa Wakubwa wanaona nchi yetu inawachosha kwa kujivunia utulivu wa amani kwa muda mrefu na pia wanamezea mate utajiri wetu Madini n.k. Wanachora mipango ya kutuvuruga sisi ndugu kwa kupitia mgongo wa dini zetu mbili. Wanaelewa fika kuwa Ukabila hawawezi kufanikiwa kwa kuwa makabila ni mengi.Lakini dini ni mbili kubwa wanaweza kuigawa nchi yetu vipande viwili kwa kutuchonganisha kwa kutumia dini zetu na ujinga, umasikini na ulafi wa baadhi yetu.
Katika kufanikisha ajenda zao hizi wanatumia wajinga, maskini na walafi na wakati mwingine bila wao kujijua kuwa wanatumika hivyo. Fedha nyingi zinasafirishwa kutoka kwa wakubwa hawaletwa kwetu kwa kuzipitisha nchi za Kiarabu chi zingine rafiki. Zikifika kwetu hapa zinaonekana kuwa zimekuja kutoka arabuni kuhamasisha shughuli za dini.
Mara nyingi Wakubwa hawaatafuta uchochoro laini au dhaifu ambao una watu wanaoweza kushawishiwa kirahisi. Kwa bahati mbaya wapo baadhi ya Waisilam wachache walio dhaifu kwa kuwa na kasoro hizo kama ilivyo hata kwa baadhi ya Wakristo.
Wenzetu hawa wa mfano wa Issa Ponda (sijui ushekh aliupata wapi labda wa kujipa kama Mtikila), wanatumiwa wengine hawajijui kutokana na kasoro hizo hapo juu Ni wajinga kiasi cha kushindwa kujua athari wanazoiletea nchi yao. Hawana tofauti yoyote na majambazi walio jela. wanatujengea chuki kubwa sana wakati sisi ni ndugu kabisa.
viongozi wetu wanao udhaifu mkubwa sana kwa kutoshughuliakia hili jambo kwa uzito mkubwa sana. Nigetegemea Rais Kikwete angeitisha mkutano ukumbi wa Diamond Jublee kwa Wazee wa Dar, Viongozi wote wa serikali na amashirika ya umma na makampuni binafsi pamoja na wakuu wa vyombo vya habari na wahariri wao akafoka kwa nguvu zote akiwa amekunja uso kwa hasira akakemea uchafu huu wa aibu katika taifa letu. kuwasweka rumande wahalifu hawa tu haitoshi kuwaogopesha na kuwaelimisha wengine wenye mtizamo kama huo.
Hata hivyo kwa Waislam wema wasingewaeza kuvunja makanisa kwa kisingizio cha mtoto kukojorea kuruani. katika hadithi za mtume Muhammad (S.A.W) kitendo cha namna hiyo kilijitokeza na Mtume akakitolea mafundisho yake. Kuna mlevi aliingia msikitni alimokuwa Mtume na maswahiba wake wamepumzika na wakijadili mambo kadha ya kidini. mlevi huyo alikojoa mle msikitini . Maswahiba wa Mtume walitak kumpiga lakini Mtume aliwazuia kabisa akawataka wamuache amalize kukojoa. Alipomaliza kukojoa aliwachagua watu wakamsindikiza mpaka nyumbani kwa kuhofia kuwa angepata madhara njiani au asingeweza kufika nyumbani kwake kwa kuwa alikuwa mamelewa sana. Aliwaambia maswahiba wake kuwa isingekuwa vizuri kumuadhibu mlevi huyo. Kesho yake taarifa za mlevi huyo zilisambaa mji mzima wa Makka na wote walishangaa kwa mlevi huyo kutoadhibiwa. Marafiki wa mlevi huyo kesho yake walikwenda nyumbani kwake kumuuliza kulikoni kwa kitendo chake hicho cha uchokozi. Aliwashangaa kwa kuwa hakuwa na kumbukumbu kuwa alitenda kitendo hicho kabisa. alistuka sana na kushangaa aliponaje kutoadhibiwa. Pale pale aliamua kurudi mskitini kuomba radhi kwa Mtume na waumini wenzake. aliomba radhi kwao na kumwambia Mtume amsilimishe kwa kuwa aliridhika kuwa dini hiyo ya mtume ni ya amani na ya watu waungwana wenye subira. baada ya hapo famiali yake yote ilisilimu na akwashawishi marafiki wake wote wakasirimu. Mtume siku hiyo aliwageukia maswahiba wake akasema, "Je mgelimuadhibu huyu bwana si matokeo yake yangekuwa ni chiki na wala asingesilimu?" Zipo hadithi nyingi za namna hiyo ambazo Waislamu wanaelekezwa kuzichukulia kama mafundisho kwa matendo mema na ya uvumilivu katika kuishi katika jumuia yoyote ile.
Akina Ponda ni waganga njaa. tena njaa yoa wapo tayari kumwaga damu ya Watanzania bila kujali dini yoyote. kumbukeni anavyomsakama Shekh Mkuu. Anataka atoke kwenye kiti hicho ili akae yeye au mtu wake kwa madai kuwa yeye ni poa sana. Amekuwa anapanga hata kumteka na kumpoteza. Ponda sio Mtanzania bali ni Mrundi kabisa. Lakini kuwa Mtanzania hakumpi haki ya kuvuruga amani ya nchi kwa visingizio vya dini. Akamatwe awekwe kizuizini muone vile nchi itakavotulia. Yeye ndo kitovu cha michoro yote ya vurugu hapa nchini. akifa au akipelekwa kizuizini gerezala Kawetere nchi itatulia na huta ona makanisa yanachomwa moto wala Shekh Mkuu na waislam wema hawatabughudhiwa tena. Sote Watanzania bila kujali dini zetu tushirikiane kuibana serikali yetu imuhifadhi mpumbavu huyu kwa kuwa madhara yake ni kwetu wote. hatuwezi kusubiri serikali ijayo huenda nayo ikagwaya kwa kuwa ameanza ujinga huu muda mrefu kupitia serikali za awamu zote labda ya Mwalim Nyerere.