Sheikh Ponda apandishwa kizimbani Morogoro

Sheikh Ponda apandishwa kizimbani Morogoro

1800

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Posts
2,215
Reaction score
611
Nipo katika viunga vya mahakama ya mkoa wa Morogoro, nimeona ulinzi mkali umeimarishwa na helicopter ya polisi kutoka Dar es salaam ikiwasili mnamo mida ya saa tano.

Habari ni kuwa helicopter hiyo ilimleta Sheikh Ponda kuja kusomewa mashtaka yake, mashtaka ambayo hayakuzidi hata nusu saa kusomwa, na mnamo saa sita na dakika 28 mchana helicopter hiyo iliondoka na kurejea D.s.m.

Bado haijajulikana kama imeondoka na Sheikh Ponda au vipi.

Hivi kweli Ponda amekua threat kiasi hiki?
Ktk mahakama ya Mkoa wa Morogoro ameletwa Sheikh Ponda kuja kusomewa shitaka la uchochezi.

Nimeshangaa kuona umati wa askari kanzu, FFU na wale wa Usalama barabarani. Pesa ya walipa kodi inateketea kwa mambo ya kijinga kama haya inatia uchungu sana.

Kwa sasa chopa inawashwa na sheikh anarudishwa Dar.




DSC03292.JPG



Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo
Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ''Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ''katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilikaa Dhamana Imefungwa na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.




DSC03303.JPG



Sheikh Ponda akiondoka Mahakamani Mpaka Aug 28 2013


DSC03308.JPG



Ulinzi wa POLISI
 
Ktk mahakama ya Mkoa wa Morogoro ameletwa Sheikh Ponda kuja kusomewa shitaka la uchochezi.

Nimeshangaa kuona umati wa askari kanzu, FFU na wale wa Usalama barabarani. Pesa ya walipa kodi inateketea kwa mambo ya kijinga kama haya inatia uchungu sana.

Kwa sasa chopa inawashwa na sheikh anarudishwa Dar.
 
Mkubwa kwa kuwa hukohuko jaribu kutafuta data kamili na urudi kutujuza kilichokuwa kinajiri. Ni ombi tu mkubwa.
 
Takbir.......Takbir... kiama chao chaja muda si mrefu.
 
Kweli ponda ni tishio,,,ila sisi walala hoi tutazidi kuletewa kodi zisizo na kichwa wala miguu ili kufanikisha utatara wa design hii,,hii ndio tz
 
Mi nilidhani kabla ya kumpeleka mahakamani angecharazwa viboko makalioni ili akamuineshe mke na watoto wake
 
Havi Dar hakuna Mahakama sasa ?
Abood Bus, Hood zimejaa tele

Ila Ponda anatakiwa kuwa makini sana
wakati mwingine lazima aondoke
 
Shekhe Issa ponda Issa amefikishwa mahakamani mkoani morogoro leo na kusomewa mastaka ma tatu.. Staka la kwanza ni kuchochea uvunjifu wa sheria, pili ni maneno ya kukashifu na kudharau dini nyingine, tatu ni kuandaa machafuko ambayo yamepigwa marufuku.. Aliletwa na helkopta ya polisi na kurudishwa Dar es salaam na gari ya polisi..

Serce😀w bony..
 
kwahiyo wanampandisha na helkopta sio!!!!! Mwisho wa siku unasikia hana kesi ya kujibu na yuko huru. kuna siku tutaanza kudai kodi zetu.
 
Dhu, hayo mashitaka mbona hayajakaa vizuri .............. especially hilo la tatu la kuandaa machafuko??
 
Aliletwa na chopa kisha karudishwa na gari!!!

Kwa hiyo yale ya Dsm ni mashitaka feki??
 
Back
Top Bottom