PreGE2025 Sheikh Ponda: Viongozi wa dini waache tabia ya UCHAWA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,931
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema anakereka na tabia za baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa kidini kuwa na tabia za kusifia sana viongozi kupindukia(chawa) tabia ambayo pia imeingia hata kwa viongozi wa kidini.

Sheikh Ponda amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na JAMBO TV na kueleza kuwa tabia hiyo inatokana na baadhi ya watu kutokutaka kuwajibika katika maeneo yao.

Soma: Sheikh Nurdin Kishki: Uchawa unakatazwa katika Uislam

Sheikh Ponda pia amekemea wale wanaowaita watu majina mabaya kuwa sio jambo zuri.

“Nasaha zangu ni kwa hao watu kwamba wajenge heshima kuwa mtu ambaye umesimama vizuri unakuwa mwadilifu ukiwa hivyo huwezi kuitwa chawa ukifanya matendo ambayo yanakufanya uitwe chawa ni jambo baya sana na kwa bahati mbaya sana jambo la uchawa linakwenda mpaka kwa viongozi wa dini kuna viongozi wa dini wanaitwa machawa” amesema sheikh Ponda.

HAPA HAKUNA VIONGOZI WA DINI, NI TAKATAKA TUPU
 
Wakuu , hii taasisi inaitwa Bakwata imekuwa ikijihusisha na siasa za Ccm je hili ndo lengo lake ?
Bakwata ilianzishwa na Julius Nyerere akishirikiana na Paulo Bomani, sasa mengine jiongeze wewe
 
Back
Top Bottom