Sheikh Mkuu wa mkoa wa Tabora, Ibrahimu Mavumbi amewataka Waumini wa dini ya kiislamu mkoani Tabora kufuata maelekezo ya serikali na viongozi wa dini kuhusu kuilinda amani ya Taifa.
Sheikh Mavumbi ametoa rai hiyo wakati akifungua misikiti mitatu katika Wilaya za Igunga na Nzega mkoani Tabora akisema kila muumini na Mtanzania anawajibika kulilinda Taifa lake kwa kudumisha amani.
SHeikh Mavumbi amesema zipo athari mbalimbali zinazoweza kutokea endapo wananchi hawatalilinda Taifa ikiwemo kukwama kwa shughuli za kila siku zinazoweza kuwaingizia kipato.
Akiwa katika wilaya hizo,Sheikh amezindua misikiti ya AL RAHMAN uliopo kijiji cha IDUDUMO,msikiti wa AL RAHIM uliopo BUHEKELA A na msiti wa AL SHEIKH KHALID ambayo imejengwa na taasisi ya ALTIJARAH AL RABIHA.