Sheikh Ponda akosoa utendaji wa Rais Magufuli

Sheikh ameongea ukweli mtupu wenye akili tumemuelewa. Bahati mbaya huko kukurupuka na visasi ndio tabia za mkuu wa kaya. Binafsi alinichosha mwaka jana akiwa mbunge wa Chato alipoamua kugawa pesa za mfuko wa jimbo kwa vijiji walikoshinda wenyeviti wa CCM na kuvitenga vijiji walikoshinda wenyeviti wa CHADEMA ilikuwa ni uamuzi wa hovyo na wakibaguzi tena kwa pesa za serkali lakini hayo ndio yalitokea. Plz mnaomshauri mhe msaidieni.
 
yaaaani ponda namkubali sana japo mie mgalatia
 
Toeni upumbafu hapa mbona kuna maaskofu na masheikh wengne wamempongeza JPM na hamkuhoji wala kuwashutumu eti wameingilia siasa?? Huyo magu sio Mungu (labda ni mungu wenu) na anamapungufu yake na ni lazima akosolewe ili ikiwezekana akiona inafaa ajirekebishe. Viongozi wa dini wanao uhuru wa kupongeza na kukosoa kama raiya wengne wa nchi hii. Kama hamtaki akosolewe na viongozi wa kidini basi zuiyeni pia asipongezwe na viongozi wa kidini maana "these are two sides of the coin"
 
tunanavyo fahamu sisi wengine tunavyomfahamu bwana mkubwa yeye ni kiongozi wa dini iweje leo aanze kuingilia mambo ya siasa za nchi kama vipi aanzishe naye chama cha siasa.
 
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema ina kasoro za kiutawala.

Akizungumza leo, Sheikh Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.

“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:

“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.

Watanzania watafurahi zaidi kama serikali haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”

Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti.

Anasisitiza, “Jambo hili halipo sawa hata kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu serikalini ni nzuri na inahitajika sana, lakini namna ya utekelezaji wa dhamira yake hakuuanza vizuri.

“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kuepuka madhara kama yale ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani ya Dar es Salaam mwishowe serikali ikaingia gharama,” amesema Sheikh Ponda.
Ni vichaa tu ndiyo wanaoweza kupokea ushauri wa huyu Mzee, ni nilini na wapi Magufuli amefanya kazi bila kuwa na taarifa za huyo anayemchukulia hatua? Au yeye anafanya kazi IKULU? Ambako anapokea taarifa za utendaji wa Rais hata amkosoe au maisha ya jela kayakumbuka?? Issue ya meli ni wajinga tu ndiyo wanaoamini Magufuli alihusika lakini kwa wenye uelewa hata wa darasa la nne wanafahamu mchezo gani ulichezwa pale hivi Polisi akikukamata akakupeleka mahakamani ukahukumiwa kinyume cha sheria kosa litakuwa la mkamataji au mahakama iliyotoa hukumu wakati ikijua kuwa huna kosa?? Wangapi walishakamatwa na mahakama ikawaachia licha ya kukamatwa na vielelezo? hilo lilikuwa deal la watu ni vema asiyejua asikimbilie kulaumu asichokijua.
 
Kase
Kujua au kuyaeleza mapungufu ya magufuli hautaji hata elimu ya darasa la 7, Magufuli amesha shindwa wenye uwelewa tulisha lifamu hili
Kusema akishidwa haina haja ya kuitwa rais bora akalime CHATO
 
Sheikh ponda(gaidi)atuie alitakaa waendelee kuagiza sukari?wameshikwa pabaya
 
Amemmiss mkwere naona,maana mkwere alimueza ponda haswa, akinyanyua mdomo tu alikuwa kamata tia ndani.
 
Huo ndio ukweli tutaingia kwenye gharama za kuwalipa wahanga soon,
Kumbe na masheikh huwa wana akili.
Kati ya Sheikh Ponda na JPM nani atakuwa na riport kamili ya majipu?
 
Nani kakwambia mh, raisi John P Magufuli anatumbua majipu bila kuwa na ripoti zinazohusu wanaotumbuliwa? hiyo ni dhana tu,watu wanapenda kulaumu utendaji wa mh, jpm ili kupata free publicity, lakini mwisho wa siku pumba na ngano zitatenganishwa, mh, Magufuli anatekeleza kilichokuwa kilio cha watanzania walio wengi sasa kama kuna mtu anadiriki kupingana naye basi mtu huyo akimbiwe kama ukoma.
 
Busara na hekima vitawale jaman, kama mtu amehujumu uchumi wa nchi yetu atumbuliwe tuu maana Hamna namna eeeh...
Bibi na babu pamoja na mama wajawazito na watoto + walimu huku shamba wanakosa huduma bora za afya kwa ajili ya ufisadi wa wachache... Mi nazani Sheikh amuache Mh Rais awafyatue tuu....kama ni makosa yatarekebishwa mbele ya safari
 
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema ina kasoro za kiutawala.

Akizungumza leo, Sheikh Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.

“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:

“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.

Watanzania watafurahi zaidi kama serikali haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”

Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti.

Anasisitiza, “Jambo hili halipo sawa hata kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu serikalini ni nzuri na inahitajika sana, lakini namna ya utekelezaji wa dhamira yake hakuuanza vizuri.

“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kuepuka madhara kama yale ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani ya Dar es Salaam mwishowe serikali ikaingia gharama,” amesema Sheikh Ponda.

Nashauri angezidisha bidii kufundisha imani tu, haya mambo hayawezi, maana kila kukicha majipu yanayofumuka yatamuumbuwa sheikh wa watu...
 
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema ina kasoro za kiutawala.

Akizungumza leo, Sheikh Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.

“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:

“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.

Watanzania watafurahi zaidi kama serikali haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”

Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti.

Anasisitiza, “Jambo hili halipo sawa hata kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu serikalini ni nzuri na inahitajika sana, lakini namna ya utekelezaji wa dhamira yake hakuuanza vizuri.

“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kuepuka madhara kama yale ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani ya Dar es Salaam mwishowe serikali ikaingia gharama,” amesema Sheikh Ponda.

- Huyu naye angetulia kwanza maana na yeye ni jipu ajue kwamba zile enzi za kumbembeleza bembeleza zimefika mwisho sasa akileta za kuleta atatumbuliwa tu kama wenzake, Ponda kwa mwanasiasa toka lini? Yeye atulie asubiri zamu yake cause inakuja soon!!

le Mutuz
 
Back
Top Bottom