Sheikh Ponda akosoa utendaji wa Rais Magufuli

Sheikh Ponda akosoa utendaji wa Rais Magufuli

Watu wengine unaweza kuwadhania ni watoto wadogo kwa comments zao.. Badala ya kulijadili tamko lake , watu wanaanza kumshambulia sheikh.sio vyema kabisa kwa kuwa kuna mafundisho nilipewa kuwa " kamwe usimdharau kichaa pale akupapo tahadhari "......

Hakuna atakaepinga kauli ya sheikh kuwa RAIS wetu (pamoja na viongozi wake wengine) wamekuwa wakikurupuka katika maamuzi ambayo mwisho wa siku , anguko lake huzimwa kimya kimya na hili halihitaji kurunzi kuliona

Rais asiwe na msukumo wa kutoa maamuzi on the spot katika vitu vinavyohitaji mawazo ya wataalamu..

**TANZANIA KWANZA**

Ethics na intellectual integrity ndio tatizo kuuubwa kwa watanzania, si busara kumuattack mtu personally katika kila anachokisema, wakati mwingine inapaswa kutulia na kuyapima yale anayoyasema kwa mtazamo wa 3D, maoni ya ponda haya ni ya kawaida mno!! Na yana logic sana!

Kuna mtu mmoja anasema magu anatumia ripoti za CAG za miaka iliyopita, kwa taarifa tu, ripoti ya mwaka jana ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ilionyesha kuwa wizara ya ujenzi ndio iliboronga kuliko zote na kuipa serikali hasara kubwa, mbona basi magu hajajitumbua yeye wala makatibu wakuu wa wizara yake?!😱

Kwahiyo ni ukweli kuwa magu anachokifanya ni aina flani ya ambush tu, ambayo kimsingi sio nzuri, maana kuna watu wameajiriwa ili kufichua maovu kama hayo ili yeye na serikali yake wayachukulie hatua, sasa kama yeye kageuka kuwa mfichuaji wa maovu (jambo hili si baya) aliowaajiri kufanya kazi hiyo nao si ni kama wanakula mishahara hewa tu🙄🙄

Sijawai kumuelewa mzee ponda ila katika hili nahisi yuko sahihi kwa asilimia zote.
 
Ameongea kama shekh Ponda na vilevile kama kiongozi wa Taasisi.
 
ni heri kuchukua hatua hata kama utakua unakisea potelea mbali.....tutalekebisha mbele kuliko kutochukua hatu...nchi hii ina mambo ya ajabu sana...ninaposema ya ajabu ni ya ajabu kweli....JPM
 
Ndugu zangu msiogope kwenda shimoni kwa kuogopa kusema ukweli hata yesu na Muhammad walipo an a kuitangaza haki walipata misukosuko ila hawakuogopa madhalimu sasa tukitaka kujikomboa tusiangalie nani kasema tuangalie nini kasema
 
Je kuna ambao wameondolewa hatujaambiwa sababu wala nini
Na silazima kilahatua atakayochukua kufukuza wezi eti aje kutuambia,nyingine afanye na jopo lake tumeshaamua kumpa kazi. Kilakitu aje kuripoti kwetu ili iweje,atakapojiskia kusema na aseme japo vingine Ni aibu hata kusema...mf mtummoja mishahara 17 inamaana serikali iliyopita ilikuwa na uzembe wa kuchezea kodi zetu alafu walimu wakiomba nyongeza za mishahara wanaambiwa wakatafute kazi nyingine za kuwalipa vizuri eti kasungura kadogo...
Kwanza huyo ponda anayeponda yeye kawahi kufanyia hii nchi jambo gani la maana zaidi ya udini??
 
sheikh Ponda ni mtetezi wa haki ambaye hatishiki
 
Andiko la shekhe ponda, halina uhalali wa kiuthibitisho ni ngonjera tu, Rais na yeye nani mwenye taarifa za watendaji pia mwanahalisi ndio wameandika , ha ha ha my foot
 
“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:
Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.
Ndio maana kila siku nasema JPM ana kazi ya ziada katika vita yake na rushwa na kwa hakika hataweza kuifanikisha akiwa ndani ya ccm.
Mfano mmoja suala la wizi wa makontena bandarini, yeye na PM walijua ukitumia mfumo wa intelijensia ya kawaida hawataweza kukupa ripoti sahihi kwa hiyo akaamua kutumia 'vijana' wao ambao waliwapa majina ya wezi wote, makontena yalikotolewa mpaka namba za magari yaliyoyapakia. Kwa hiyo PM Majaliwa alipoenda pale bandarini kwa kupitia body language akagundua kuwa watu aliotegemea wamsaidie wanaijua hiyo issue na possibly walikuwa kwenye 'mchakato' wa kuua so juu kwa juu. Ndio akaamrisha pale pale wakamatwe ...hapo alivunja sheria lakini ni njia ipi nyingine angeliweza kuitumia!?
Pia issue kama ya mita za mafuta, ukiuliza kwa 'kufuata sheria' wanakupa taarifa zisizo lakini ukishtukiza baada ya kupata taarifa za 'vijana wao' mtendaji mkuu anakudanganya hadharani, na wewe si unamfuta hadharani!
Haya, kuna issue ya wafanyakazi hewa. Katuma 'vijana wake' wakafanya case study ya mikoa miwili ...na hapo je!?
Nchi tumeiharibu wenyewe kwa woga wetu na bahati mbaya JPM ni Lionel Messi ndani ya Ndanda FC ikipambana na Beyern Munich.
 
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema ina kasoro za kiutawala.

Akizungumza leo, Sheikh Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.

“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:

“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.

Watanzania watafurahi zaidi kama serikali haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”

Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti.

Anasisitiza, “Jambo hili halipo sawa hata kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu serikalini ni nzuri na inahitajika sana, lakini namna ya utekelezaji wa dhamira yake hakuuanza vizuri.

“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kuepuka madhara kama yale ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani ya Dar es Salaam mwishowe serikali ikaingia gharama,” amesema Sheikh Ponda.
tatizo la ponda elimu yake ya kuungaunga sasa mtu wa aina hiyo upeo wa kumkosoa mtu kama JPM ni ndogo sana
 
Ethics na intellectual integrity ndio tatizo kuuubwa kwa watanzania, si busara kumuattack mtu personally katika kila anachokisema, wakati mwingine inapaswa kutulia na kuyapima yale anayoyasema kwa mtazamo wa 3D, maoni ya ponda haya ni ya kawaida mno!! Na yana logic sana!

Kuna mtu mmoja anasema magu anatumia ripoti za CAG za miaka iliyopita, kwa taarifa tu, ripoti ya mwaka jana ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ilionyesha kuwa wizara ya ujenzi ndio iliboronga kuliko zote na kuipa serikali hasara kubwa, mbona basi magu hajajitumbua yeye wala makatibu wakuu wa wizara yake?!😱

Kwahiyo ni ukweli kuwa magu anachokifanya ni aina flani ya ambush tu, ambayo kimsingi sio nzuri, maana kuna watu wameajiriwa ili kufichua maovu kama hayo ili yeye na serikali yake wayachukulie hatua, sasa kama yeye kageuka kuwa mfichuaji wa maovu (jambo hili si baya) aliowaajiri kufanya kazi hiyo nao si ni kama wanakula mishahara hewa tu🙄🙄

Sijawai kumuelewa mzee ponda ila katika hili nahisi yuko sahihi kwa asilimia zote.

Umesema ukweli kabisa ila tunatakiwa tu kukubaliana na hali halisi kuwa watu wanatumia smartphones zaidi kuliko akili zao.mtu anaona kuwa na limits ni ujinga ila husaidia sana kwa kuwa hata Mimi nikiiona mada ni heavy weight kwangu huwa nakaa kimya ili nijifunze kwa wajuzi ..

Sheikh ponda sijawahi kumuelewa yeye pamoja na wafuasi wake ila kwa tamko hili...siwezi Kumpinga kwa asilimia zote
 
Ahsante shekh kwa maoni mazuri....
 
Sheikh atakuwa amesoma sana vitabu magazeti kwa muda aliokaa ndani kazi ni kusoma tu na busara zimeanza kurejea! Nampongeza sana Sheikh! Ila ajue kuwa JPM anasoma report hizo hizo ndio anatoka nazo!
 
Nataka kujua CV ya Sheikh Ponda ni sawa tu na wale wachungaji wenye elimu ya dini tu bila elimu ya utawala alitakiwa kujua Urais na Uwaziri ni vitu tofauti kabisa. Rais vyombo vyote viko chini yake anajua kila mtanzania amelalaje na ameamkaje ndio Maana Majambazi wanachapwa risasi tu. Sasa anataka kufanya siasa elimu yenyewe ya kujua mambo ndogo Duh Waislamu wamuombee tu! Na uzuri waislamu wasomi hawawezi kumpinga wala hawawezi kumfuata atabakia na kakundi kadogo tu kanakomzunguka. Maana Hii elimu bure nawasiwasi Viongozi baadhi hasa wabunge wataachwa wenyewe kwenye Majukwaa

Back
Top Bottom