Sheikh Ponda akosoa utendaji wa Rais Magufuli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema ina kasoro za kiutawala.

Akizungumza leo, Sheikh Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.

“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:

“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.

Watanzania watafurahi zaidi kama serikali haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”

Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti.

Anasisitiza, “Jambo hili halipo sawa hata kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu serikalini ni nzuri na inahitajika sana, lakini namna ya utekelezaji wa dhamira yake hakuuanza vizuri.

“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kuepuka madhara kama yale ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani ya Dar es Salaam mwishowe serikali ikaingia gharama,” amesema Sheikh Ponda.
 
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema ina kasoro za kiutawala, anaandika Happiness Lidwino.

Akizungumza na Mwanahalisi Online leo, Sheikh Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.

“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:
“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.

Watanzania watafurahi zaidi kama serikali haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”
Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti.

Anasisitiza, “jambo hili halipo sawa hata kidogo.”

Kwa vile sheikh Ponda kawagusa watawala basi watasema anachanganya dini na saisa! Lakini akisema yule shehe war dar kuisifia CCM na watawala basi ni sawa. Halafu serikali inadai "watanzania tuombeeni". Kwa vile wanafanya maovu na dhuluma kwa kukusudia si watanzania wote ambao tutawaombea. Wengine tutailaani serikali kila pale inapokusudia kufanya uovu kwa makusudi.

Sent from my SM-G920W8 using JamiiForums mobile app
 
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, amekosoa utendaji wa Rais John Magufuli, hasa dhana ya kutumbua majipu, akisema ina kasoro za kiutawala, anaandika Happiness Lidwino.

Akizungumza na Mwanahalisi Online leo, Sheikh Ponda amesema utendaji wa Rais Magufuli ni wa kulipualipua.

“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na matatizo mengi, lakini lazima utaratibu kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,” amesema na kuongeza:
“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya kazi kwa kulipuka.

Watanzania watafurahi zaidi kama serikali haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”
Amesema ingekuwa bora kwa Rais Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya kupata ripoti.

Anasisitiza, “jambo hili halipo sawa hata kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu serikalini ni nzuri na inahitajika sana, lakini namna ya utekelezaji wa dhamira yake hakuuanza vizuri.

“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ili kuepuka madhara kama yale ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani ya Dar es Salaam mwishowe serikali ikaingia gharama,” amesema Sheikh Ponda.
Nadhani ni maoni tu kama ya wana JF wengi hapa, hatuwezi kuyapa uzito sana!
Kama angekuwa specific kuwa jipu A na B hayapo sahihi, au angesema kuwa haya yanayotumbuliwa ana uhakika kuwa hakuna taarifa za kitaalam zilizokamilika uchunguzi wake hivyo raisi anakurupuka kuamua, lkn mwanzo mwisho wa kisa chake hakuna uthibitisho wowote wa madai yake!
Ni hofu tu ya wananchi kuwa huenda haya yanayotokea hayatafanikiwa na Mkuu atashindwa!
Nadhani Ponda we endelea kumuombea raisi ayafanye Yale yenye manufaa na dhamira njema kwa umakini na ukamilifu mkubwa! Nadhani pia raisi hawezi kupuuzia ushauri wako, ingawa ofisi ya mwendesha mashtaka, PCCB, polisi na TISS ndio wanapaswa kuyasimamia haya!
 
Lakini msije ongea lugha nyingine mdaa si mrefu
 
Watu wengine unaweza kuwadhania ni watoto wadogo kwa comments zao.. Badala ya kulijadili tamko lake , watu wanaanza kumshambulia sheikh.sio vyema kabisa kwa kuwa kuna mafundisho nilipewa kuwa " kamwe usimdharau kichaa pale akupapo tahadhari "......

Hakuna atakaepinga kauli ya sheikh kuwa RAIS wetu (pamoja na viongozi wake wengine) wamekuwa wakikurupuka katika maamuzi ambayo mwisho wa siku , anguko lake huzimwa kimya kimya na hili halihitaji kurunzi kuliona

Rais asiwe na msukumo wa kutoa maamuzi on the spot katika vitu vinavyohitaji mawazo ya wataalamu..

**TANZANIA KWANZA**
 
Watu wengine unaweza kuwadhania ni watoto wadogo kwa comments zao.. Badala ya kulijadili tamko lake , watu wanaanza kumshambulia sheikh.sio vyema kabisa kwa kuwa kuna mafundisho nilipewa kuwa " kamwe usimdharau kichaa pale akupapo tahadhari "......

Hakuna atakaepinga kauli ya sheikh kuwa RAIS wetu (pamoja na viongozi wake wengine). Amekuwa akikurupuka katika maamuzi ambayo mwisho wa siku huzimwa kimya kimya na halihitaji kurunzi kuliona hili

**TANZANIA KWANZA**
Naomba nijazie nyama kwenye comment yako na UKWELI UTATUWEKA HURU
 
Back
Top Bottom