Sheikh Musa Alhad akiwa katika misa kanisani

Sheikh Musa Alhad akiwa katika misa kanisani

Yeye kajumuisha kasahau hakuna ihsani kumsaidia mtu wa imani nyingne kwa ibada kinyume na imani ya kiislam. Yeye pia ni kiongozi, jamii inapata picha gani na kizazi cha wanetu twawafundisha nini, kesho watajaa sunday mass wakimfuata sheikh wao kuabudu
Ndo maana nimesema hakuna kolabo katika ibada

Hayo ni maamuzi yake binafsi
 
Ndg. hamisj usiaanze kunipa masharti na shinikizo MIND YOU... nipo nachambua na kutoa dalili stahiki.....
Sio shinikizo, huo ni ukumbusho tu katika imani ya kiislamu hutangulia elimu kisha huja amali (samahani kama umeisoma katika tone ya juu ukaona ni shinikizo), pia nmesema nasubiri huo uchambuzi wako nipate kuona inapothibiti kushiriki ibada na imani tofauti na ile ya dini ya kiislam
 
Ule ni utashi wake lakini hakuna sheria ya kiislaam inayoruhusu kushiriki misa kanisani ndani ya vitabu.

Ila kuna (muammalat) yaani kukaa kwa wema na watu wa dini nyingine mkasaidie mambo ya kijamii yenye kuleta maendeleo kwa wote katika Taifa..kwahivyo hakuna ihisani ya kumsadia mtu wa imani nyingine kwa ibada kinyume na imani ya kiislaam ijapo wote ni wamoja katika kuumbwa.

Nazungumzia sheria ya kiislaam.. ama sheria za imani zingine sina ujuzi.
kwa alivyosimama hiyo ni ibada hapo? anafanya ibada hapo ya dini nyingine? ....
 
Assalam Alleykum,

Watu wa kitabu mnalizunguamziaje hili?
]
Kaenda kufanya nini, Kaenda yeye binafsi ama kaenda kuwakilisha waislamu wengine... Tunaeza bishana hapa kumbe yeye anapendezwa na imani hiyo na anajifunza polepole. Ima kama kaenda kama kiongozi wa waislamu atakua ana mushkeli katika kichwa chake na waliomtuma
 
kwa alivyosimama hiyo ni ibada hapo? anafanya ibada hapo ya dini nyingine? ....
Angekuwa anabusu msalaba ndo ungeamini kuwa yuko katika ibada sio

Ww jiulize kaenda kufanya nini kanisani!?
 
Mbona papa John Paul II ameingia msikitini. Je huyu shehe amekufa kwani alipoingia kanisani. Vizuri sana kujifunza ya wenzio hutokaa kugombana. Shida yenu nyinyi mnafikiri wa kristo kwa negative tu. Jaribuni kubadilika
 
Wewe mkuu inaonyesha ni mbishi sana

Ninayo video yake kuzungumza zaidi ya dk 5 katika kanisa la ufufuo
weka hapa video ili tuamue, au ulikuja na mawazo binafsi? ukitaka kupata mawazo ya wadau usiweke habari nusunusu!!
 
Tatizo sio kuingia kanisani, tatizo ni huyu Sheikh mambo yako....

Kuna watu wanasema yuko payrol ya mfuko mkubwa akitumika kama wazee wa suti
 
Mleta thread ningekuwa nae karibu kuna lidude ningemsukumizia alikalie
 
mbona kama wengne wale anakoelekea Sheikh ni wa mlengo huo huo wa sheikh
 
mbona kama wengne wale anakoelekea Sheikh ni wa mlengo huo huo wa sheikh
I am not his fan lakini sijaona kama amekosea. Yeye hapo anasimama kwa heshima ya hayo yanayotokea. Hata Pope John aliepita aliingia msikiti mkuu wa Istanbul tena yeye alisali kabisa.
 
Back
Top Bottom