Sasa hii mie ndio naona maana ya kuhubiri amani kwa vitendo.
Linapokuja suala la amani mnaweka tofauti zenu za imani pembeni na kushirikiana kuzungumzia kitu kimoja kwa waumini wenu.
Nimeipenda sana hii na nampongeza sana sheikh.....hakika kwa mfano huu na wengine wakaiga, itakua ngumu sana kuwatenganisha watanzania maana huku mtaani tunachanganyika kwa kila kitu mpaka ndoa.
Tuachane nao hao WAPIGA ZUMALI ambao matendo yao hayaendani na matamko yao, twaambiwa ni wa wote lakini anafanya yake kwaajili ya upande wake wengine anawatenga na kuwatisha...kisa tu ni watoto wa mama wa kambo ilhali Baba ni huyo huyo mmoja na urithi ni kwa watoto wote.
Asanteni viongozi wetu wa kiroho....hakika Mungu atabariki kazi nzuri ya mikono yenu.