Sheikh Mkuu wa Dsm ahudhuria ibada Kanisa la Ufunuo, asisitiza umoja na mshikamano kwa Watanzania

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,816
image.jpeg image.jpeg image.jpeg



Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dsm amehudhuria ibada katika kanisa la Ufufuo. Akiongea na waumini wa kanisa hilo Sheikh amesema yeye kama mdau wa kamati ya Amani ya Mkoa wa Dsm anayofuraha kuona Tanzania inazidi kuwa nchi ya amani licha ya utofauti wa dini.

Amepongeza utii wa waumini wa Kikristo kwa viongozi wao, juhudi za kanisa katika kutoa huduma za jamii kama elimu na afya.

Amewataka waumini wote kuishi kwa umoja na upendo na wenzao Waislam na baadae kudumisha amani na mshikamano wa Taifa.
 
Sasa hii mie ndio naona maana ya kuhubiri amani kwa vitendo.
Linapokuja suala la amani mnaweka tofauti zenu za imani pembeni na kushirikiana kuzungumzia kitu kimoja kwa waumini wenu.

Nimeipenda sana hii na nampongeza sana sheikh.....hakika kwa mfano huu na wengine wakaiga, itakua ngumu sana kuwatenganisha watanzania maana huku mtaani tunachanganyika kwa kila kitu mpaka ndoa.

Tuachane nao hao WAPIGA ZUMALI ambao matendo yao hayaendani na matamko yao, twaambiwa ni wa wote lakini anafanya yake kwaajili ya upande wake wengine anawatenga na kuwatisha...kisa tu ni watoto wa mama wa kambo ilhali Baba ni huyo huyo mmoja na urithi ni kwa watoto wote.

Asanteni viongozi wetu wa kiroho....hakika Mungu atabariki kazi nzuri ya mikono yenu.
 
Ubinadamu mbele ya mambo yote. Safi sana sheikh!
Ubaguzi wa aina yeyote si jambo zuri
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom