barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dsm amehudhuria ibada katika kanisa la Ufufuo. Akiongea na waumini wa kanisa hilo Sheikh amesema yeye kama mdau wa kamati ya Amani ya Mkoa wa Dsm anayofuraha kuona Tanzania inazidi kuwa nchi ya amani licha ya utofauti wa dini.
Amepongeza utii wa waumini wa Kikristo kwa viongozi wao, juhudi za kanisa katika kutoa huduma za jamii kama elimu na afya.
Amewataka waumini wote kuishi kwa umoja na upendo na wenzao Waislam na baadae kudumisha amani na mshikamano wa Taifa.