Sheikh Mkuu Dsm aibua utata Freemason

Naomba kujuzwa,

Kwa hiyo hata kwenye mazishi ya Wakristo, mnapoalikwa hamtakiwi kuhudhuria? Achana kusoma dua, je muislamu haruhusiwi kuhudhuria?

Je, kula vyakula pamoja na vinywaji vilivyoandaliwa pia ni kosa?
Inapaswa kuhudhuria na kula na kunywa vilivyoruhusiwa kisheria
Ila hairuhusiwi kushiriki ktk ibada na hata kumuombea dua
 
Kuheshimu maiti hata kwenda kuzika (kwa wanaume) haijakatazwa ila kumuombea duaa HAPANA, halafu ujue yule ni kiongozi kuna kundi la watu wanafata vile afanyavyo, kama anaingia hadi kanisani huyu anawekwa kwenye kundi la WANAFIKI,
WANAFIKI hawataingia peponi mpaka watubu.
 
Ni muda sasa waislam wa Tanzania kuamka na kutafuta ilmu sehemu mbali mbali kuliko kuwafata hawa mashekh ubwabwa a.k.a wachumia tumbo, a.k.a wanafki.
kila siku wanakuja na vioja vipya.
 
Una maanisha hata wezi wakiiba tuwaache?
 


Hakuna kosa alilofanya Al Hadi, kamuomba Mwenyezi Mungu amuweke Chandi atakapo kwa aliyoyatenda duniani.

Hata kama angeuombea pepo basi hilo ni ommbi tu na halina aana kuwa atapewa hiyo pepo au la. Hakimu wa mwisho ni Allah.

Mbona wapo "Waislam" wengi sana ma Free MMasons na tunawazika na kuwasalia na kuwaombea pepo, lakini mwisho wa siku? Ni Allah pekee.

Hata mimi nnamuombea kwa Allah Sir Andy Chande awekwe popote anapostahiki.
 
Alikua mtu ila alipinga uwepo wa MUNGU tunayemuabudu.


Hata Ammi yake, ndugu ya baba'ke Mtume wetu, kipenzi chetu, Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam, Abu Lahab, alimpinga Mtume na aliupinga Uislam kwa nguvu zake zote, lakini Mtume alikuwa akimuombea atoke kwenye udhalim huo, licha ya kuwa ilikuwa imeshashuka aya kuwa huyo makazi yake ni motoni, surat Al-Masad (Tabatiyada).

Alichofanya Hadi hakina makosa, kamuomba Allah amuweke popote anapostahili, hata mimi nnamuomba Allah amuweke Chande popote anapostahili.
 
Hii mada ni fitna tu ya kuwatenganisha Waislam.

Waislam tuwe makini katika mada kama hizi. Zinatutengenisha.

Tuungane wote na kuona kuwa Sheikh Hadi hana kosa alilolifanya.
 
Sikujua kua na wewe ni mnafki kiasi hiki, unajinasibu kuitetea dini humu kumbe hakuna kitu. Hivi hujui nini kua hairuhusuwi kabisa kunyanyua mikono yako kumwombea dua MTU aliyekana uwepo wa Mungu tunayemwabudu? Inategemea anaomba katika mazingira ya kukemia au kutoa support kwa washiriki wa msiba.

Yeye alipewa mwaliko kama kiongozi wa waislam wa mkoa wa Dar, alifika kwa mwaliko huo. Basi angetumia nafasi hiyo kukemea dini kama aliyokua Chande, usiwe mnafki sema alipewa nafasi kama Mani na kwa minajili ipi?
 
Hii mada ni fitna tu ya kuwatenganisha Waislam.

Waislam tuwe makini katika mada kama hizi. Zinatutengenisha.

Tuungane wote na kuona kuwa Sheikh Hadi hana kosa alilolifanya.
Bado na narudia kua unaleta unafki, moto mweusu tii unakuhusu mbele ya Allhah S.W.
 
Wabongo wengi hatuishi katika imani zetu dini uliyozaliwa nayo ndio hiyo hiyo unaing'ang'ania na kutoana macho sijui uelewa mdogo sijui tunakosea wapi, binafsi sir chande alisimamia alisimamia alichokiamini
 
Kumuombea mtu akiwa hai ni sawa kabisa huenda ipi siku Mola akamfumbua macho na kuelekea njia inayostahili, ila kumuombea akiwa amekufa hakuna kitu kama hicho,

Kumuomba Mungu amuweke mahala anapostahili sawa je kulikua na ulazima kwa Shekh mkubwa kama yeye kusema chochote kwenye yale mazishi??? analeta taswira gani kwa wanafunzi wake wanaomfuata.

Ni huyo huyo aliashaingia mpaka kanisani kwa kisingizio kua anahubiri amani,

Hatuwezi kufumbia macho jambo hili na kumpongeza, kuna siku atakuja kusema waislam twende kanisan tushiriki dua ya pamoja kuliombea taifa kwa kigezo cha uzalendo.
 


Ameombewa awekwe popote anapostahiki, kuna tatizo lipi hapo?
 
Bado na narudia kua unaleta unafki, moto mweusu tii unakuhusu mbele ya Allhah S.W.


Hahahaha, umekuwa na ujuzi wa "ghaib" ambao hata Mtume wetu, kipenzi chetu, Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam hakuwa nayo?

Jifunze kuandika vizuri.
 

Wacha porojo wewe, kamuombea awekwe popote anapostahiki kuna kosa lipi?
 
Hahahaha, umekuwa na ujuzi wa "ghaib" ambao hata Mtume wetu, kipenzi chetu, Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam hakuwa nayo?

Jifunze kuandika vizuri.
Unaelewa makosa uliyoyafanya kwa makusudi, rudi katubu. Unafki ulioonesha leo nimekusamehe bure tu.
 
Ameombewa awekwe popote anapostahiki, kuna tatizo lipi hapo?
Kwahiyo unataka kusema ndivyo vitabu visemavyo? Mbona huelewi kitu wewe? Huenda nawe ni muumini wa jamii hiyo unayejifichia koti la uislam nisikulazimishe.
 
Kuna mtu anawasema freemanson wakati kiunoni kwake ana hirizi na chale hadi makalioni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…