Sheikh Mkuu Dsm aibua utata Freemason

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,950




Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salumu mwishoni mwa wiki iliyopita alizua utata katika kona mbalimbali za kijamii kufuatia kufanya dua maalumu ya kumwombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Freemason Afrika Mashariki, marehemu Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy Chande’ (pichani).

Tukio hilo lilifanyika Aprili 21, mwaka huu katika Shule ya Sekondari ya Shabani Robert na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi, akiwemo Rais Msaatafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa sanjari na wanafunzi wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo.



Sir Andy Chande alifariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nchini Kenya kwa maradhi ya presha na kuzikwa katika Makaburi ya Baniani, Makumbusho jijini hapa kwa kuchomwa moto.

Katika enzi za uhai wake, Sir Andy Chande aliwahi kuweka wazi kuwa yeye ni mfuasi na kuhani mkuu wa Jumuiya ya Freemason, jumuiya ambayo inaaminika na baadhi ya watu kwamba iko kinyume na mafundisho ya dini za Kiislamu na Kikristo. Katika tukio hilo la kuwakumbuka waasisi wa shule hiyo, Shehe Alhadi aliongoza dua maalumu kwa upande wa dini ya Kiislamu kwa ajili ya kumwombea marehemu Chande jambo lililoibua mjadala mkubwa.

MSIKIE HUYU

Baadhi ya watu walihoji kuwepo kwa shehe mkuu wa Dar kwenye dua hiyo wakati marehemu alijulikana kuwa ni Freemason ambayo wengi hawaiamini kama ina sera za Mungu. Msikie huyu:

“Mimi binafsi sidhani kama ni sahihi kumfanyia dua mtu ambaye aliwahi kuweka wazi kwamba yeye yupo upande wa kushoto, tena akiwa mwenyekiti na kuhani mkuu wa jumuiya ambayo inaaminika inakwenda kinyume na maadili ya Kimungu,” alisema Kimashi John katika ukurasa wake wa Facebook.

Mbali na mtu huyo, mijadala mingi siku hiyo ilikuwa kuhudhuria kwa shehe mkuu kwenye shughuli hiyo.

Gazeti la Uwazi, baada ya kuyasikia hayo, liliamua kumtafuta Shehe Alhadi mwenyewe ili kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Shehe Alhadi alikuwa na haya ya kusema:

“Katika dua niliyoiomba siku ile hakuna neno nililosema kwamba Mungu aiweke roho ya marehemu Chande mahali pema peponi. Unaweza kusikiliza tena rekodi za ile dua, nilichokifanya ni kumwombea kwa Mwenyezi Mungu amlipe kwa mambo yote aliyoyafanya duniani maana yeye ndiye hakimu wa mwisho.”

Aidha, katika hatua nyingine Uwazi lilipotaka kujua kama alishawahi kumpa elimu ya dini ya Kiislamu, marehemu Sir Chande ikiwa ni pamoja na kumtaka asilimu, Shehe Alhadi hakuwa tayari kulizungumzia hilo zaidi ya kukiri kwamba amekuwa akifahamiana na marehemu kwa muda
mrefu.
 
Ninaamini ni jukumu la wazazi kuwafundisha watoto maadili ya dini na ninauhakika wazazi wa Sir Andy Chande walimfundisha mtoto wao yale waliyoamini. Uamuzi wake alioufanya ninaona alikuwa huru kama binadamu kuchagua dini ya kuabudu pia alisimama imara katika kile alichoamini. Apumzike kwa amani.
 
Ninaamini ni jukumu la wazazi kuwafundisha watoto maadili ya dini na ninauhakika wazazi wa Sir Andy Chande walimfundisha mtoto wao yale waliyoamini. Uamuzi wake alioufanya ninaona alikuwa huru kama binadamu kuchagua dini ya kuabudu pia alisimama imara katika kile alichoamini. Apumzike kwa amani.

Freemasonry sio dini..Acheni kupotoka
 
UISLAM UNA MISINGI MADHUBUTI NA HAITETEREKI.
KTK UISLAM NI TWO WAY TRAFFIC;
1. IMMA SHAKILLAH
2. WA IMMA KAFURAH
Mtu anafahamika Ana amini mashweitan kwanini husitumie nafasi hiyo kuwaeleza jamii kuwa Allah hakuelekeza vile huyu marehem alivyokuwa anaabudu.
Mtu mpaka anachomwa moto, unaweza kusema ulikuwa hufaham kuwa alikuwa anaabutu vitu tofauti na vile alivyoamrisha Allah!?

BAL 'LINSANA 'ALA NAFSII BASWIRA.
 
Aliyekwambia Freemason wanaamini nguvu za shetani amekudanganya......tatizo hampendi kujishughulisha kuelewa mambo
Ww sasa naona kichwa chako ni kizito hivyo kwa kwel ni unafaa kwao maan umekuwa tofali zuri linalofaa kujengea na kudhibitisha uimara wao. Sor km sijaelewek
 
UNAWEZA KUTUAMBIA WANAAMINI NGUVU ZA NINI WEWE UNAYEJISHUGHURISHA KUELEWA MAMBO?
Freemasonry sio dini...Kila mtu ndani ya Freemason ana ruhusa ya kuwa na dini yake anayoamini yeye..ila Wote kwa pamoja katika masonry kuna imani ya kuwa kuna Mungu mmoja na watu mbalimbali wanatumia namna anuwai kuelezea jinsi gani wanamfahamu Mungu...Kiufupi ni Brotherhood inayoamini katika "Supreme Being" in other words "God"
 
Heri nikajiunge huko niwaachie hata watoto wangu pesa nitakapokufa;
Mkiwaona wanaoandikisha wapeni jina langu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom