Mimi kama kijana msomi wa elimu zote mbili za kiimani na kidunia,uelewa wangu unatosha kabisa kupaza sauti yangu kukekema vitendo vya ajabu kabisa kabisa alivyofanya kiongozi huyu, sijajua anawawakilisha waislam wa kundi lipi kwa nafasi yake hiyo?
Kitendo cha juzi kuhudhuria msiba wa aliyekua kiongozi wa jumuiya ya Freemason Afrika Mashariki na kati Sir Andy Chande huko jijini Dar es salaam na kumuombea sala ama dua, kitendo hiki kimetufedhehesha sana waumini wa dini ya kiislam nchini! ni kitendo cha aibu kutokea na kiongozi huyu anatakiwa kuwajibishwa kwa mujibu wa taratibu na sheria za dini ya kiislamu.Staki unafiki ni kweli tumedhalilishwa sana tena sana.
Ifahamike kua huyu sheikh ameshiriki kile ninachoitwa "SHIRKI". Anatambua kabisa kiongozi huyo wa Freemason anaabudu mungu wake tofauti na Mungu tunayemwabudu sisi,haabudu Mungu huyu aliyemtuma kipenzi chetu mtume Muhammad S.A.w, Sio Mwenyezi Mungu S.W aliyetuumba sisi wanadam pamoja na Mbingu na dunia/Ardhi.
Uislamu hauna hulka ya kuwalea watu wa aina hii, inatia hasira sana na kusikitisha sana kuona mtu anafika mahali flani tena kwa kuwakilisha waumini huku akijua ni kinyume ni mafundisho yetu anashiriki matendo kuikana imani yake. Kamwe waislam wa kweli hatutakivumilia kitendo hiki, labda aseme alienda kuliwakilisha kundi lake alijuaye yeye na sio waislam wote! " NO!NO!" I said NO to this.
Kwa taratibu tu za kawaida hakuna mahali desturi za imani flani zikatumika katika kufanikisha sala ya mazishi ya mtu kutoka imani nyingine, hili haipo otherwise mhusika awe amebadili imani yake kabla ya kufariki dunia.Hapa ndio inapodhihiri kua ajenda ya kiongozi huyo huenda ni tofauti na hatuijui.
Kuna mahali alinukuliwa akisema kua eti yeye alisema kua alimwomba mwenyeziMungu amuweke Mahali panapohusika, hivi kiongozi huyu ni hatambui kua hata kukanyaga eneo lile ni makosa? Kunywa tu hata maji aliyopewa kwenye tukio hilo ni kosa, kuonesha tu sura ya kununa tu kwenye msiba huo lilikua kosa, kula ubwabwa ulioandaliwa kwenye tukio hilo ni kosa kwa mujibu wa mafundisho ya mtume wetu na maamrisho ya kitabu kitukufu cha Qur-an.Kushiriki kwa dua hiyo huyo sheikh anatakiwa kujivua kilemba cha ushakhe,akatubu upya.
Alitakiwa kusimamama na kutolea ufafanuzi jinsi ambavyo imani yetu inatukataza kabisa Kushiriki sala ya mtu kama alifariki akiwa amemkana Mwenyezi Mungu S.W na mtume Muhammad S.W. Kwa imani yetu ni imekatazwa hata Kushiriki sala ya mtu wa dini nyingine mpaka awe ameshahadia au amesilimu.Alitakiwa kuukataa mwaliko kama huo kama yeye ni kiongozi wa waislam wote wanaoiamini Qu-an tukufu.
Nitoe wito kwa waislam wote popote walipo wajitokeze kukemea tabia za aina hii, kunyamaza kimya ni kuonesha kuridhia vitendo vya aina hii na tufahamu kua siku ya mwisho tutajibu.