Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
wenzenu wanajenga shule nyinyi mnajenga madrasa na kufundishana ngumi km vile tuko somalia! pia tambueni kuwahao wakristo wazungu ndio walizitawala nchi za kiarabu na uislamu kwa ujumla hivyo wakristo kutawala wameanza enzi na enzi na hakutakuja kuwa na usawa hapa duniani.
sasa we unatoka nje ya mada,hata hivyo waarabu ndo walianza kutawala wazungu,miaka 3000 iliyopita kabla warumi hawaokoa jahazi miaka 500 iliyopita,kabla waturuki hawajawatala tena mpaka muingereza akaja kuwakomboa,hata hivyo hii haihusiana na topic ilkiyopo hapa
 
[emoji814] Daah...HUWA NAJIULIZA HILI:

■ Awamu iliyopita,

[emoji666]RAIS= Muislam.

[emoji666]MAKAMU WA RAIS= Muislam

[emoji666]RAIS WA ZANZIBAR = Muislam

■ Awamu hii

[emoji666]RAIS= Mkristo

[emoji666]MAKAMU WA RAIS = Muislam

[emoji666]WAZIRI MKUU= Muislam

[emoji666] JAJI MKUU= Muislam

[emoji666] RAIS WA ZANZIBAR= Muislam

Sijui kama ingekuwa ni wakristo wameshikilia nafasi hizo ingekuaje kama sasahv lawama haziishi.

- Hata kwenye all 3 National pillars wangekuwa waislam wote bado kuna watu wangelaumu tu.
Lini rais wa Zanzibar au makamu wa rais alikuwa mkristo? Unafahamu ni kwa nini?
 
Rais Kikwete alipokuwa madarakani walisema anatumiwa na Wakristo na hawajali waislam wenzie.
Hiyo labda uliisema wewe mkuu.nakumbuka kikwete aliitwa mdini sana.wakristo walilalamika sana kwamba anawapendelea waislam. Tena mpaka kashfa wakati wa mwezi mtukufu pale ikulu rais akipata iftar ilikuwa ni kelele mtindo mmoja.labda kama umesahau.sisi tu nakumbuka sana.
 
Huo si uchochezi?
Hilo sikosa la jinai?
kwa nini polisi wasimkamate na kufunguliwa mashtaka huyo SHEIKH kama walivofunguliwa mashtaka Akina lema, lissu na wengine?
 
Hata tukiangalia idadi ya watz wakirsto na waislam wapi wako wengi zaid ya wengine? Ukishajibu utajua kuwa hata kwny teuz lazma wawe wengi pia
Sasa awamu iliyopita mlivyokuwa mnalalamika kikwete anawapendelea waislam hilo la idadi ya watu mlikuwa hamlioni.? Hopeless
 
Hiyo labda uliisema wewe mkuu.nakumbuka kikwete aliitwa mdini sana.wakristo walilalamika sana kwamba anawapendelea waislam. Tena mpaka kashfa wakati wa mwezi mtukufu pale ikulu rais akipata iftar ilikuwa ni kelele mtindo mmoja.labda kama umesahau.sisi tu nakumbuka sana.
Mkuu ni sawa ila to be honest, wakristo hawakuwahi kulalamikua seriously hilo na kama walilalamika sio suala lililochukua hata mwezi mmoja.

Ila ndugu zetu waislam walishamlaumu kuwa amekuwa agent wa wakristo na hawajali waislam wenzie na kipindi hicho Lowassa ndio alikuwa very close na waislam

Leave alone hizo issues, imekuwa ni kawaida ndg zetu waislam kucomplain kwenye kiiila kitu kuwa wanaonewa.

Research yourself utagundua.
 
Facts gani?
Tanzania ina mikoa 135? Huoni kama ameandika andika tu?
Au wewe ndio yeye kwa ile ID yako ya 7?
Karudie tena kuaoma kusoma usipepese macho uelewe content ya jamaa. Uje apa na +ve idea alizitoa, ukipata -ve kama sasa, rudia tu kusoma tena mungu atakusaidia utaelewa taratbu tu.....
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
Wewe ni mnafiki! Tupe takwimu za safu ya uongozi Zanzibar ndipo ulete fyokox2 zako huku JF. Badala ya kuhubiri dini unaendesha siasa? Usichezee AMANI ya nchi yetu tumetoka mbali. We are very serious! Mod naomba upeleke huu uzi face book tujitokeze hadharani kuchangia hizi ni ID tunazifahamu wengine walianzisha uzi wa uliza ujibiwe!
 
Dau pekee ndo mwenye akili ktk waislamu wote Tanzania,maana aliweza kuiba na kujenga taswira ya lidini Nssf,big up dau
Siku hizi huna jipya tena. Dr.Dau ndio balozi wako huko Malaysia, wale watu wako pale wakina magori wote wapo kikaangoni.goma limegeuka.uliyekuwa unamuombea mabaya yupo ughaibuni anachapa kazi. Magori na wenzie lazima wafungwe kwa wizi waloufanya.
 
Hii ni sumu inatengenezwa,madhara yake huyaoni leo,baada ya miaka kadhaa,ndo madhara yanakuja kuonekana unakuta kuna west Tanganyika na east Tanganyika kimchezo mchezo tu,kipindi hicho kina pengo au malasusa walishaondoka zamani na hakuna wa kumuuliza tumefikaje hapa..
Yote haya kwasababu ya tamaa za kidunia,ambazo utakufa utaziacha
 
huyu sheikh akamatwe na atiwe ndani ni mchochezi, mdini na dhaifu kiakili.
Kigodoro,
Mimi si sheikh wala si mchochezi.

Kitabu changu cha historia ya TANU nä uhuru wa Tanganyika kinauzwa nchini toka mwaka 1998.

Kimependwa sana na tunakwenda to leo la nne.

Kitabu kimepitiwa na mabingwa wa historia ya Afrika na review kuchapwa katika majarida ya Ulaya na Marekani.

Hakuna popote nimeitwa dhaifu wa fikra au mchochezi au mdini.

Zaidi wananialika katika vyuo vyao kufanya mhadhara.
 
tuache kuwa na mtazamo hasi,serikali imejitenga namaswala ya dini toka zamani,raisi hawezi akazingatia huyu dini gani katika uteuzi wake,bali yeye ataangalia yupi ni mtendaji bora,mchapakafi,mbunifu ambaye ataleta maendeleo.
 
Sidhani kama Rais huteua watu kwa kuhoji dini zao. Pia kuna ukweli kuwa taasisi za elimu za Kikristo zimekuwa zikijitahidi sana kuendeleza watoto kielimu tofauti na taasisi nyingi za Kiislamu ambazo zimekuwa zikihimiza zaidi elimu ya Madrassa na lugha ya Kiarabu.

Hizi ni propaganda za kuwanyamazisha waislamu.. Hili jambo lina siri nzito sana ambayo siku muslim wakiamka itakuwa shughuli hapa
 
Wewe ni mnafiki! Tupe takwimu za safu ya uongozi Zanzibar ndipo ulete fyokox2 zako huku JF. Badala ya kuhubiri dini unaendesha siasa? Usichezee AMANI ya nchi yetu tumetoka mbali. We are very serious! Mod naomba upeleke huu uzi face book tujitokeze hadharani kuchangia hizi ni ID tunazifahamu wengine walianzisha uzi wa uliza ujibiwe!
sawa sawa mkuu hao wanataka uchochezi tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom