Share nasi matukio yako ya ukuaji

We jamaa fala sana kwaiyo unasubiri upewe tuzo😂
 
Msanii Dully ndio katoka ni wimbo wake salome na ablam yake Historia ya kweli, nipo mkoa X shule boarding usiku tumetoroka tukaenda ukumbini, show imeisha tunatoka ukumbini tunakuta wahuni wanamzonga dada mmoja hivi kisa kavaa nusu uchi dada kujisalimisha akakimbilia kwa maskali waliokuwa lindo bank

Miye na jamaa tukapata wazo tukodi tax twende mchukua yule dada tuseme tunamjua ili tukampige mtungo,bwana wee sitosahau

Tax inapaki bank tu ile jamaa anashuka askari wakakoti bunduki mpo chini ya ulinzi lala chini jamaa akalala chini ikatolewa amri wote kwenye gari tushuke aisee tulicgezea kipigo kumbuka tumetoroka shule, tulipigwa nguo chanika magoti yamechubuka yani tupo hoi ndiotunambiwa ondokeni dereva wa tax alikimbia akasahau gari,

Tunarudi hostel tumeumia asubuhi kiongozi wa bwana akareport kwa uongozi wa shule, tukaitwa tunachezea kichapo tena, na suspension ikafuata mwezi mzima tukirudi tuje na wazazi

Hapo hapo shule mkoa huo huo imekuja imekuja timu ya Yanga kucheza si tukatoroka shule hao uwanjani vingilio hatuna ile kuzu guka zunguka uwanja tukakuta jamaa wamevunja eneo kwaiyo mnapita pale kwenye tundu mnaingia uwanjani bwana bwana acha tu

Kumbe ndani mule askari washatambua kwaiyo wamekaa ukiingia tu unaitwa kaa hapa so wazee hatujui tukaingia tukakuta watu kibao wamekamatwa tatizo siyo kukamatwa tatizo nimetoroka shule itakuwaje

Basi tumeingia hivi askari wakatuchukua kutupeleka kwenye karandinga tunapitishwa chini ya uwanja hivi jukwaani watu kibao hee kumbe walimu wapo umo na Head master si wakatuona wanafunzi wao, tupo kwenye karandika tukasikia wanafunzi wa shule X njooni tukatoka ebwana tukambiwa haraka sana rudini shule, tukarudi kesho yake sasa tulichezea fimbo na adhabu kali ikafuata


Ipo nyingine hiyo nipo form six na mwanangu mmoja kutoka Tanga uyo week end tunaenda club, tuna muhuri wetu kama wa club so tukifika tunakaa njee kingilio buku mbili tu enzi hizo kwaiyo siye tunagonga mhuri kwa buku buku tu unazama ndani ebwana kumbe wenye club wanafutilia inakuwaje watu ndani wengi arafu mapato madogo

bwana bwana si wakatuotea siku hiyo tuligongwa acha na polisi tukapelekwa uzuri form six nilikuwa day so nakaa gheto na wenzangu so wanafunzi we zangu wakajichanga wakaja nitoa

Hiyo ikapita club tunaenda ila deal hatuna ila tunaitaji bia inakuwaje tukaanza tabia za kishenzi ukijifanya unacheza mziki umeacha bia siye tunahamisha bia tunakunywa siku moja si tukahamisha bia kumbe mwenye bia katuona ebwana fujo zikaanza club ngumi ngumi, uongozi ukajuw wale wanfunzi tena aaah tukapigwa na marufuku kwenda hiyo club

Aisee story ni nyingi tunashukuru mungu utukutu wote tupo hai na maisha yana songa
 
Ulikuwa mnoko sana
 
Mimi kipindi cha ukuaji wakati wote nilikuwa mtu wa kusifiwa tu mkaka mzuri, handsome, kila mwanamke atatamani kuwa na ww utaleta sana shida lkn nimeishia kuwa mwanaume wa hovyo ndoto nyingi zikayeyuka nafikiri midomo ya sifa ikizidi wakati kutoka kwa watu wakati wa ukuaji wako hiyo ni sumu mbaya
 
Duh🤭 nikaju ulilala ukasinzia😂
 
We misomisondo
Umepigaje apoo😅😂
 

Attachments

  • IMG_0468.jpeg
    36.8 KB · Views: 22
Sikutambulishi wife😅
 
We misomisondo
Umepigaje apoo😅😂
Hapo hamna kitu mkuu. Hivi unaijua mizinga ya kienyeji wewe? We acha tu. Bora huyo jicho linaona moja. Mi yote yalivimba. Jiulize kwenye miaka kama 9 au 10. Kukimbia siwezi,acha tu
 
Hapo hamna kitu mkuu. Hivi unaijua mizinga ya kienyeji wewe? We acha tu. Bora huyo jicho linaona moja. Mi yote yalivimba. Jiulize kwenye miaka kama 9 au 10. Kukimbia siwezi,acha tu
Hahah pole mkuu
 
Hahaaaa, ukimkumbusha anasemaje sasa? Utoto Raha sana mkuu.
 
Nikiwa Darasa La Sita Wakati Nywele Sehemu Nyeti Zikianza Chipuka Nilianza Tabia Ya Uzururaji Nakumbuka Kuna Cku Nilitoka Nyumbani Saa 9 Mchana Mm Na Rafk Yangu.Aisee Tulizurura Sana Ikafka Saa 2 Ucku Nikaenda Kwa Rafk Yangu Mwngne Alikuwa Na Laptop Nikaanza Chezea Laptop Yake Mpaka Saa 5 Ucku Huku Nyumbani Hali Si Shwari Natafutwa Na Viboko Vimechumwa Viko Ndani Aisee Niliporud Nilifungiwa Ndani Niliisoma Namba Kwa Kirumi Hyo Tabia Ilifika Ukomo Siku Hyo
 
Hahaaaaa nimecheka kwa sauti. Wazee wetu walikuwa makauzu sana.
 
Mama alikuwa anasema roho za uharibifu... Unakula fimbo then anakuambia soma mithali ngapi ngapi' inasema usimnyime mtoto fimbo/mapigo maana hatayasahu hata atakapokuwa Mzee' ukimaliza kúsoma zinaanzia stick za maana
Daah!!!hyo na sisi pia tumepitia mda wa kichapo unapewa kwanza bible usome hicho kifungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…