Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,719
- 114,063
- Thread starter
- #781
Kwanza nakushukuru kwa kuniheshimu kutumia verified name. Licha ya kutumia verified name pia mimi ni mwana habari, jukumu kuu la waandishi wa habari ni tell nothing but the truth. Hivyo mimi ni mkweli daima na yote niandikayo humu ni kweli tupu.Nakuheshimu kitu kimoja, unatumia verified ID, lakini ukweli unaujua. Tuishie hapa
- Ina maana hujui nani kaamuru kuawa Ben Saanane?
- Hujui nani kaamuru Tundu Lissu ashambuliwe?
- Hujui nani alikuwa nyuma ya utekaji wa Mo Dewji ?
Kuamini ni jambo moja na kuwa na hakika ni jambo jingine. Nakuomba mambo ya imani, tuyaache kwenye dini, hapa tuzungumzie vitu vyenye uhakika na sio masuala ya imani.
- Ina maana hujui nani kaamuru kuawa Ben Saanane?. Kwanza sina uhakika kama Ben Saanane ameuwawa, wewe ndio unanieleza sasa. Nijuavyo mimi ni Ben Saanane ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, mpaka sasa hakuna ajuaye kilichomkuta. Kumbe mwenzetu unajua kuwa kauwawa na una mjua hadi aliyeamuru Ben Saanane kuuwawa!. Una uhakika wa hili?.
- Hujui nani kaamuru Tundu Lissu ashambuliwe?. Pia simjui aliyeamuru Tundu Lissu ashambuliwe, kwenye hili la Tundu Lissu, mimi naungana na mamlaka rasmi kuwa Tundu Lissu ameshambuliwa na watu wasiojulikana, na nimeisha andika mabandiko mengi kuhusu shambulio la Tundu Lissu. Vipi wewe mwenzetu unamjua aliyeamrisha Tundu Lissu ashambuliwe, una uhakika?.
- Hujui nani alikuwa nyuma ya utekaji wa Mo Dewji ?. Hata aliye nyuma ya shambulio hili mimi simjui, wewe mwenzetu unamjua?. Una uhakika?.