Shambulio la Kigaidi Urusi vifo vyafikia 93

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Idadi ya Watu waliouawa kwenye shambulizi katika eneo la Crocus City Hall Nchini Urusi imefikia 93 huku majeruhi wakiwa ni zaidi ya 140.

Shambulizi hilo la kigaidi ambalo Kikundi cha Kigaidi cha ISIS kimedai kuhusika nalo, limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo Vijana walioficha sura zao waliwashambulia Watu kwa risasi na kulipua jengo hilo.

Mamlaka za usalama Nchini Urusi zimemfahamisha Rais wa Nchi hiyo Vladimir Putin kwamba hadi mchana huu zimewakamata Watu 11 wakiwemo wanne ambao wamehusika moja kwa moja na shambulizi hilo.

Urusi imesema Watu hao wamekamatwa wakiwa wanavuka mpaka wa Urusi na Ukraine na walikuwa na mawasiliano na upande wa Ukraine.
 
Back
Top Bottom