Washukiwa wa shambulio la kigaidi la "Crocus" wanasema kwamba walikuwa wakisafiri kwenda Kiev kupokea zawadi waliyoahidiwa

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
47,620
33,370
Wanaukumbi.

MPYA: 🇷🇺🇺🇦 Washukiwa wa shambulio la kigaidi la "Crocus" wanasema walikuwa wakisafiri kwenda Kiev kupokea zawadi waliyoahidiwa - RIA

Washtakiwa katika kesi ya shambulio la kigaidi huko Crocus walisema wakati wa mahojiano kwamba baada ya shambulio hilo walikuwa wakielekea Kiev kwa tuzo, Kamati ya Uchunguzi iliripoti kwenye chaneli ya Telegraph.

"Kwa maagizo ya mratibu, baada ya kufanya uhalifu, magaidi waliendesha gari kuelekea mpaka wa Urusi na Kiukreni ili kuvuka na kufika Kyiv kupokea thawabu waliyoahidiwa," chapisho hilo linasema.

Watu waliohusika katika kesi hiyo waliripoti kwamba vitendo vyao katika hatua ya maandalizi na baada ya shambulio kwenye ukumbi wa tamasha viliratibiwa na mtu fulani kupitia ujumbe wa sauti kwenye Telegraph.

Uchunguzi unaendelea kubaini wawakilishi wa huduma maalum za Kiukreni zinazohusika katika kuandaa na kufadhili shambulio la kigaidi.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
NEW: 🇷🇺🇺🇦 The suspects in the "Crocus" terror attack say that they were traveling to Kiev to receive the promised reward - RIA

The defendants in the case of the terrorist attack in Crocus said during interrogations that after the attack they were heading to Kiev for a reward, the Investigative Committee reported on the Telegram channel .

“On the instructions of the coordinator, after committing the crime, the terrorists drove in a car towards the Russian-Ukrainian border to subsequently cross it and arrive in Kyiv to receive the reward they were promised,” the publication says.

The persons involved in the case reported that their actions both at the preparation stage and after the attack on the concert hall were coordinated by a certain man through voice messages on Telegram.

The investigation continues to identify representatives of the Ukrainian special services involved in organizing and financing the terrorist attack.View: https://x.com/megatron_ron/status/1773757744958382495?s=46&t=mTROWpaJUT8H393JMgWOvw
 
Hawa magaidi wa Kiislamu wakishafunguka zaidi mtakuja kusikia wamepigwa risasi walipotaka kutoroka, kumbe wamewekwa ndani wananyooshwa viungo ili wakifika peponi wajilie bikra kwa nguvu zote
 
Urusi inafanya "plot twisting" kwenye hii issue ya shambulizi la kigaidi.

Siku chache zilizopita, Putin alirudia yale madai yaliyokuwa yakisambaa awali kabisa kuwa magaidi walikuwa wakikimbilia Ukraine. Akatuachia swali tujiulize kwamba ni kwa nini walitaka kwenda Ukraine.

Saa kadhaa baadaye, mshirika wa karibu wa Putin, rais wa Belarus, Alexander Lukashenko, akadai kwamba magaidi walikuwa wakielekea Belarus kwanza ila walikutana na vizuizi (vituo vya ukaguzi ama checkpoints) ndipo wakabadili njia ili kuelekea Ukraine. Na akasema kuwa atatoa ushirikiano wa kiintelijensia kwa Urusi kuhusiana na hilo.

Hii statement ya Mzee Lukashenko inaonekana kuleta mkanganyiko mkubwa ukilinganisha na kauli za viongozi mbalimbali wa Urusi.

Pia, saa chache baadaye, mkurugenzi wa FSB (hili ni shirika la ujasusi la Urusi), akadai [bila uthibitisho] kuwa Marekani, Uingereza na Ukraine ndio walioratibu na kuwezesha shambulizi la Moscow huku Ukraine ikitajwa kama mhusika wa kutoa mafunzo kwa "magaidi" katika eneo lisilojulikana ndani ya Mashariki ya Kati.

Hiyo statement pekee inaonesha uzembe wa hali ya juu na ingetosha wakati uleule kumfuta kazi huyo mkurugenzi.

Hilo la watuhumiwa kwenda Ukraine "kupokea zawadi" ni jipya katika mtiririko wa matukio na huenda tukasikia mengine mengi zaidi ya haya.

Madai karibu yote kuhusu Ukraine kuhusika yanasemekana yametokana na kauli za wale watuhumiwa wa ugaidi mara baada ya kufanyiwa mahojiano. Tatizo ni kwamba, kauli zinazotokana na watuhumiwa waliopitia mateso wakati wanahojiwa huwa sio za kuaminika kwa namna yoyote ile.
 
Waongo hao,ila kipondo watachopata watasema tu data zote,na kule hawauliwi ni kiungo kimoja kimoja wanatambaa nacho.
 
Tangu shambulizi lilipofanyika urusi anaimba wimbo uleule tu wa kumtupia Ukraine lawama, ajabu hakuna chochote kimebadilika Ukraine,kama mashambulizi kwenye miundombinu na kwingineko yalikuwepo tangu mwanzoni mwa uvamizi!
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeiachia Urusi madhaifu mengi kwenye intelijensia yake ikiwemo kutengwa kimataifa katika masuala ya intelijensia.
 
Hakuna lolote .......wale jamaa wanateswa na wanaambiwa hili mateso yapungue kira kitu waseme ni Ukraine......maana hata passport zao walisema ni za Ukraine kumbe uongo mijamaa ni kutoka Tajikistan..........yaani kira wakitaka kufanya kitu kina goma ......ila wanahalalisha vita kwa sababu walikuwa kwenye smo iliyoipa urusi gharama kubwa sana tokea taifa lile liundwe sasa hivi mafuta anaagiza Belarusian kwake jamaa wamelipua karibia visima vyote
 
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umeiachia Urusi madhaifu mengi kwenye intelijensia yake ikiwemo kutengwa kimataifa katika masuala ya intelijensia.
Hivi ushawahi Kujiuliza kwanini walipokuwa wanafanya hilo tukio la Kigaidi walikuwa na confidence kabisa ila walipokamatwa walikua wanatetemeka Mwili mzima?

Kuna mambo mengi sana hatuyajui kuhusu haya mashambulizi ya Kigaidi, inakuwaje mtu anajitoa Mhanga yupo kawaida tu?

Urusi hawa unaowasema hawana kitu kwenye intelijensia wametupa jibu, hao magaidi walipewa dawa maalum ambayo inatoa hofu kabisa, wakati wanafanya tukio ile sio akili yao kabisa, akili imewarudia Walipokamatwa.

Uzuri wa hili tukio kila findings Wanazozipata zinawekwa online, tutajua tu ukweli muda si mrefu.
 
Tangu shambulizi lilipofanyika urusi anaimba wimbo uleule tu wa kumtupia Ukraine lawama, ajabu hakuna chochote kimebadilika Ukraine,kama mashambulizi kwenye miundombinu na kwingineko yalikuwepo tangu mwanzoni mwa uvamizi!
Sasa unakasirika nini, Putini kaishasema atatoa adhabu ya wazi.
 
Hawa magaidi wa Kiislamu wakishafunguka zaidi mtakuja kusikia wamepigwa risasi walipotaka kutoroka, kumbe wamewekwa ndani wananyooshwa viungo ili wakifika peponi wajilie bikra kwa nguvu zote
kwa hiyo wewe hauatki waliowatuma wachukuliwe hatua na Urusi 🤣
 
Hakuna lolote .......wale jamaa wanateswa na wanaambiwa hili mateso yapungue kira kitu waseme ni Ukraine......maana hata passport zao walisema ni za Ukraine kumbe uongo mijamaa ni kutoka Tajikistan..........yaani kira wakitaka kufanya kitu kina goma ......ila wanahalalisha vita kwa sababu walikuwa kwenye smo iliyoipa urusi gharama kubwa sana tokea taifa lile liundwe sasa hivi mafuta anaagiza Belarusian kwake jamaa wamelipua karibia visima vyote
Hizo ni fikra zako kutoka Chanika tuzikubali halafu za Putin tuziache.
 
Back
Top Bottom