Shambulio la damu

Shambulio la damu

NYEMO CHILONGANI
SHAMBULIO LA DAMU
0718069269

Sehemu ya Kumi na Tatu.

“Did you find his name?” (umelipata jina lake?)
“Yes sir!” (ndiyo mkuu)
“Who is he?” (ni nani?)
“Kennedy Edward!”
“Very nice. I want to know where he lives, his family too, just give me everything I want, right?” (safi sana! Ninahitaji kujua anapoishi, familia yake pia, nipe kila kitu ninachohitaji, sawa?)
“Yes sir,” (ndiyo mkuu)
Hayo yalikuwa ni mazungumzo baina ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nchini Uingereza, MI6 aliyeitwa Pegg Burn ambaye alikuwa akizungumza na kijana wake, mtaalamu katika masuala ya kompyuta aliyeitwa Baines Cole.
Walipewa taarifa za chini kabisa kwamba wapinzani wao wakubwa, Marekani walikuwa wamepeleka mtu nchini Iraq kwa ajili ya kuhakikisha wanapata formula iliyotumika kutengeneza mabomu ya nyuklia ambayo alikuwa akijivunia Rais Hamis.
Japokuwa alikuwa ameaminiwa sana lakini Backnon ndiye ambaye alitoa taarifa hiyo kwa watu hao na kuwaambia kuhusu Kennedy. Ulikuwa usaliti mkubwa kufanywa na mtu kama yeye lakini hakuonekana kujali, kwake, kitu alichokuwa akikiangalia ni pesa tu kutoka kwa Waingereza ambao walikuwa wakimlipa vizuri sana mtu ambaye aliwapa siri kuhusu Marekani waliokuwa wakipambana nao kisiri.
Hizo zilikuwa taarifa zilizowaumiza sana, walilifahamu taifa hilo, halikuwahi kushindwa kitu, walikuwa na watalaamu, wajanja ambao kama kweli walikuwa wakihitaji kitu chochote kile ilikuwa ni lazima wakipate hata kama wangechukua muda gani.
Backnon aliwapa taarifa aliwaeleza kwa kifupi sana na kuwataka wao wafuatilie ili wapate zaidi kile walichotakiwa kukipata. Hilo halikuwa tatizo, haraka sana Cole akaanza kutumiwa na hatimaye kumpata mwanaume huyo aliyeitwa kwa jina la Kennedy Edward.
Ilikuwa ni lazima waipate formula hiyo, walijua kabisa kwamba kama wangezungumza naye na kumuomba lingekuwa jambo gumu sana hivyo walitakiwa kufanya kitu fulani ambacho kingemfanya mwanaume huyo afanye kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba anawapelekea formula hiyo.
Kitu ambacho walifikiria ni kuiteka familia yake. Waliamini kwamba alikuwa na mke na watoto ama mtoto hivyo ilikuwa ni lazima wafanye juu chini mpaka kuhakikisha wanaipata familia yake.
Hawakujua alipokuwa akiishi nchini Marekani lakini baada ya kufuatilia katika kompyuta zao, wakagundua mpaka mahali alipokuwa akiishi na familia yake, yaani mkewe na mtoto wake aliyeitwa Nicole.
“Ana mke na mtoto mmoja,” alisema Cole.
“Safi! Anaishi wapi?”
“Jijini New York kwenye mtaa wa Shakespeare W56 nyumba namba 1709 karibu na Barabara ya St. Victoria,” alijibu Cole.
“Nahitaji kujua kuhusu familia yake!”
“Mtoto wake anasoma katika shule ya Prince Richard ambayo si mbali sana na mahali wanapoishi,” alijibu.
“Sawa. Naihitaji familia yake, watume vijana waende huko haraka sana,” alisema Burn.
Siku hiyo ilikuwa ni kivumbi, kila kona ndani ya makao makuu ya MI6 ilikuwa balaa, kila mmoja alikuwa bize kuhakikisha familia ya Kennedy inatekwa haraka iwezekanavyo.
Kulikuwa na mpango mzito ambao ulikuwepo katika kuhakikisha wanaipata formula hiyo, wao kama wao walijaribu kwa nguvu zote kuingia nchini Iraq lakini ilishindikana hivyo kama Marekani walifanikiwa basi ilikuwa ni lazima wahakikishe wanaipata hata kama hawakifanyia kazi hata kidogo.
Vijana waliokuwa nchini Marekani wakapigiwa simu na kuambiwa kilichokuwa kikiendelea, wao, walitakiwa kufanya kila liwezekanalo mpaka familia hiyo itekwe na kupelekwa mahali fulani kufichwa.
Hilo halikuwa tatizo, vijana hao wakaondoka na kuelekea katika Mtaa wa Shakespears ambapo huko wakaelekea karibu na nyumba hiyo na kutulia. Siku hiyo, kwa kuwa waliwahi asubuhi na mapema, wakamuwahi mke wa Kennedy, Eve ambaye alikuwa akimtoa mtoto wake na kumpeleka shule.
Walimwangalia, hawakutaka kwenda kumteka, siku hiyo ilikuwa ni maalumu ya kuangalia ni kitu gani alikuwa akikifanya, yaani akitoka shuleni anakwenda wapi mpaka kukamilisha mizunguko yake.
Baadaye aliondoka na kuelekea kazini ambapo jioni akamfuata mtoto wake na kurudi nyumbani. Mpaka hapo wakajua kwamba alikuwa na sehemu tatu za kwenda, yaani shuleni, kazini na nyumbani hivyo kama kweli walitaka kumteka walitakiwa kufanya hivyo wakati akirudi kutoka shuleni.
Wakawasiliana na wenzao kutoka nchini Uingereza na kuwaambia kuhusu kile kilichotokea, haraka sana wakawaambia kwamba walitakiwa kufanya utekaji jioni kwa sababu kusingekuwa na magari mengi kama asubuhi.
Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, siku iliyofuata wakafuatilia na mwisho wa siku, majira ya jioni wakati Eve akitoka shuleni na mtoto wake kurudi nyumbani ndiyo wakatumia nafasi hiyohiyo kwenda kulisimamisha gari lao mbele ya gari la mwanamke huyo wakati akiwa kwenye barabara ya mtaani kwao kwenda nyumbani kwake, wanaume hao wakateremka na kumfuata kisha kuwatoa wote wawili ndani ya gari.
“Twende huku,” alisema mwanaume mmoja, usoni mwake alikuwa na kinyago, mkononi alishika bastola, yaani alikuwa na muonekano wa mtu hatari.
Wakawachukua, wakawaingiza ndani ya gari na kuondoka zao. Hakukuwa na mtu aliyeliona tukio hilo, katika mtaa waliokuwa wakiishi hakukuwa na watu nje, kila nyumba ilikuwa na geti lake, watu waliokuwa wakiishi huko wengi walikuwa wafanyakazi wa serikali ambao walijengewa nyumba hizo na serikali.
Ndani ya gari Eve alikuwa akitetemeka, alikuwa na hofu, kwa jinsi alivyowaangalia watu hao, kwa jinsi walivyoonekana ilionyesha walikuwa watu hatari ambao wangeweza kuwafanya jambo lolote baya kama tu wangeleta ubishi ndani ya gari hilo.
“Don’t kill us, pleaseee....” (tafadhali msituue...) alisema Eve huku akionekana kuwa na hofu.
Wanaume wale walimwangalia, hawakujibu kitu zaidi ya kumtaka kunyamaza kwani kama angeendelea kuomba kutokuuliwa, basi wangemuua.
***
Wataalamu wanne wa kutengeneza mabomu ya nyuklia walirudiwa katika hali yao ya kawaida na kushangaa kujiona ndani ya nyumba moja huku wakiwa wamefungwa kamba na kuwekwa kwenye viti.
Hawakuwa na nguo zozote zile, miilini mwao kulikuwa na nyaya za umeme ambazo zilipitishwa kwenye swichi zilizokuwa humo ndani.
Hawakujua walikuwa mahali gani, walishangazwa kwani walichokumbuka ni kwamba walikuwa ndani ya nyumba yao ambayo ndiyo walikuwa wakiitumia kwa ajili ya kufanyia mambo yao mengine, kwenye nyumba waliyokuwa kipindi hicho, haikuonekana kuwa sehemu salama hata kidogo.
Wakabaki wakiangalia, ghafla mlango ukafunguliwa na wanaume wawili kuingia ndani. Walishangaa, mmoja walimfahamu, alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakipeleka matunda ndani ya nyumba yao ile.
Walishangaa! Kwa nini walikuwa mahali hapo? Walifanya nini? Kila walichojiuliza walikosa majibu. Walitamani kuzungumza kitu lakini midomo yao iliwekwa gundi, haikufumbuka, hivyo walitakiwa kubaki kama walivyokuwa.
“Karibuni sana! Tunasikitika kwa sababu mmechukua muda mrefu mpaka kurudiwa na fahamu, ila msijali, natumaini kila kitu kitakwenda kama kinavyotakiwa,” alisema Kennedy huku akiwaangalia, wanaume hao walibaki kimya tu.
“Tuna dakika chache sana!” alisema Backnon.
“Usijali! Ngoja tuanze kazi yetu,” alisema Kennedy na kuanza kuwafafanulia kuhusu zile nyaya alizokuwa amewawekea.
Aliwaambia kwamba zilikuwa ni nyaya ambazo zingewapa mateso makubwa mno, zilikuwa na nguvu za kupitisha umeme kwa kiwango cha 150W ambacho kilikuwa kikubwa mno na kingeifanya miili yao kubadilika na kuwa kama mkaa ndani ya kipindi kifupi kabisa.
Yote hayo wangewafanyia kama tu wasingeonyesha ushirikiano wa kile walichokuwa wakikihitaji mahali hapo.
Wataalamu hao walikuwa wakimsikiliza tu, maneno aliyowaambia yaliwatisha na kuona kabisa kulikuwa na hatari kubwa mbele yao.
“Tunahitaji kitu kimoja kutoka kwenu. Nyie ndiyo mliotengeneza formula ya mabomu ya nyuklia, kwa hiyo tunahitaji hiyo formula. Ooh! Samahani kumbe sijatoa gundi, atakayepiga kelele, tutamlipua,” alisema Kennedy huku akiwaangalia.
Akawapa karatasi, alihitaji kujua formula ambayo ilitumika kutengeneza mabomu yale. Kuitoa formula hiyo ilikuwa kazi kubwa, ni siri ambayo kama wangemwambia mtu yeyote yule basi kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kumdhoofisha Rais Hamis kitu ambacho hawakutaka kabisa kuona kikitokea.
Walifunguliwa mikono ya kulia na kuambiwa kuandika lakini kila mmoja alionekana kusita kufanya hivyo. Hivyo alichokifanya Backnon ni kuzichukua karatasi zile, akachukua ndoo ya maji na kuwamwagia.
Hawakupenda kabisa ubishi, kwao, kitu walichohitaji kilikuwa ni kufanya kile walichowaambia, hilo lilikuwa kosa, hawakutaka kushindwa hivyo baada ya kuwamwagia maji wakawasha umeme ambao ulikwenda kwenye chombo kilichokuwa na nguvu ya kupunguza na kuongeza halafu kwenda moja kwa moja kwenye miili yao.
Walipigwa shoti, walitetemeka, nywele ziliwasimama. Ulikuwa umeme mwingi hivyo ukapunguzwa kidogo lakini maumivu hayakupungua, kwa jinsi shoti ilivyokuwa ikiwapiga, hata kupiga kelele walishindwa kabisa. Baada ya sekunde thelathini tu, wakazima umeme.
“Huwa ninawapenda wanaume jeuri kama nyie, yaani mnaifanya siku yangu kuwa nzuri kabisa,” alisema Kennedy huku akionyesha tabasamu, yaani kama alifurahia kuona wale watu wakikataa kufanya kile alichotaka wakifanye.
Wataalamu hao wakawa hoi, walijua kabisa walikuwa katika mikono ya watu hatari ambao wangeweza kuwamaliza kama tu wasingefanya kile walichokuwa wakikihitaji mahali hapo.
Walishindwa kuvumilia, umri wao ulikuwa mkubwa, hawakuwa imara kwenda sawa na maumivu yale hivyo wakakubali kuwaambia juu ya hiyo formula waliyokuwa wakiitaka.
Wakaandika kwenye karatasi, zilikuwa ndefu mno, kila mtu na yake kisha kuzichukua karatasi zote nne na kuangalia kama zilikuwa zinafanana, kweli zilikuwa sawa. Wakaridhika kwani kitendo cha kuwapa hizo formula tu ilionyesha wangefanikiwa kwa kile walichohitaji kipindi hicho.
Walipomaliza, wakawaambia hawakuwa na muda, ilikuwa ni lazima waondoke mahali hapo na kuwahakikishia kwamba wangewasiliana na watu ambao wangekuja mahali hapo na kuwafungua.
Wakaondoka! Walipokaribia nje, Kennedy akaitoa sura ya bandia aliyokuwa ameivaa na kuitupa humo kisha yeye kuondoka na Backnon.
“Hakikisha hizo karatasi unazishika wewe,” alisema mwanaume kutoka upande wa pili kutoka Marekani, hawakuwa wakimwamini sana Backnon.
“Sawa. Haina shida!” alisema.

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Alhamisi
 
NYEMO CHILONGANI
SHAMBULIO LA DAMU
0718069269

Sehemu ya Kumi na Nne.

Rais Hamis wa Iraq alikuwa na uhakika wa kutamba kila siku na kutokufanywa kitu chochote kile, mkwara ambao aliwapiga Marekani na dunia kwa ujumla ulimfanya kila mmoja kunyamaza na wengi kupanga mikakati ya kuangalia ni kwa namna gani wangeweza kupambana na mwanaume huyo.
Hakujua kama katika jumba lile aliloagiza watalaamu wawekwe liliingiliwa na mwanaume hatari na hatimaye watalaamu hao kutekwa na kupelekwa kusikojulikana.
Wakati akionekana kuwa na furaha huku akipanga ni kwa namna gani angeweza kupambana na Wamarekani ndipo akapokea simu yake kutoka kule alipowahifadhi wataalamu wake.
Alipoiona simu hiyo tu, moyo wake ukawa na hofu, alihisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea hivyo kuipokea na kuita, sauti ya upande wa pili ikasikika.
Alichoambiwa ni kuvamiwa kwa jumba hilo, kulikuwa na mtu mmoja aliyekwenda humo akijifanya kuungana na muuzaji wa matunda na kuwateka wataalamu wote na kuondoka nao usiku huo.
Hakuamini kile alichokuwa akikisikia, alihisi kama alikuwa ndotoni na baada ya muda mfupi angejikuta akiamka kutoka kitandani. Alichanganyikiwa, mwili wake ulisisimka na kijasho chembamba kuanza kumtoka.
Ilikuwa usiku sana, alichoka, alisikia usingizi lakini ghafla usingizi ukatoweka. Hakutaka kubaki ikulu, haraka sana akaondoka na kuelekea katika jumba lile.
Kile alichoambiwa ndicho alichokutana nacho, aliwakuta walinzi wakiwa wameamka huku wakionekana kuchoka mno, akawauliza ni kitu gani kilitokea, wakamwambia kwamba walileweshwa madawa ya kulevya.
“Kivipi?” aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Kwenye matunda,” alijibu mwanaume mmoja.
“Yaani kivipi?” aliuliza tena.
Wakaanza kumwambia kila kitu kilichotokea, stori nzima ambayo aliambiwa hapo ilionekana kuwa kama ujinga, hakuamini kama wanajeshi waliokuwa na mbinu nyingi, mafunzo mengi wanyweshwe dawa za usingizi kilaini kama ilivyokuwa.
Aliambiwa kwamba chanzo cha yote alikuwa ni mzee Shabir aliyekuja na mtu ambaye walikuwa na uhakika kwamba ndiye alikuwa mtu aliyewalewesha na kuwateka watalaamu hao.
“Huyo mzee yupo wapi?”
“Ndani! Tumemfungia,” alijibu mlinzi mmoja.
Akaondoka na kuelekea katika chumba kile, alipofika, akamkuta mzee huyo akilia, alimuuliza maswali mengi, alimwambia kwamba mtu aliyekuwa amekuja naye alikuwa Ibrahim, yule mwanaume bilionea kutoka Afrika ambaye alitaka kuona ni kwa jinsi gani nilikuwa nikifanya biashara hii kwa kuwa alikuwa amenisaidia mno.
“Hebu subiri! Umesema nani?” aliuliza Rais Hussein.
“Ibrahim!”
Haraka sana rais huyo akachukua simu na kuwapigia vijana wake na kuwaambia waende hotelini kuona kama mwanaume huyo alikuwemo.
Vijana hao wakaondoka na kuelekea huko, walipofika na kumuulizia, wakaambiwa alikuwa ndani, wakaenda huko lakini kitu cha ajabu kabisa walikuta chumba kikiwa tupu.
Wakaanza kumtafuta kila kona, bafuni, kwenye kabati, chini ya kitanda lakini kote huko hawakufanikiwa kumuona mwanaume huyo.
Wakampigia simu rais na kumwambia kwamba mwanaume huyo hakuwepo na kulikuwa na dalili zote kwamba hakuwa amelala chumbani humo kwa usiku huo.
“Mna uhakika hayupo humo?” aliuliza rais.
“Ndiyo mkuu! Hayupo.”
Kwa kuwa alikuwa amechanganyikiwa, akaagiza vitu viwili, kwanza walinzi wake wote wauawe kwa kupigwa risasi kutokana na uzembe uliokuwa umetokea lakini pia polisi wajipange kila kona kuwatafuta wataalamu hao ambao mpaka muda huo haikujulikana walikuwa mahali gani.
Hayo mawili yakafanyika huku wakimwacha mzee Shabir hai. Polisi walihangaika usiku kucha kuwatafuta watu hao lakini hawakufanikiwa kitu kilichoonyesha inawezekana kabisa watu waliofanya tukio hilo walijipanga, walijua kilichokuwa kikiendelea kutokea, kwamba wangetafutwa sana na ndiyo maana nao walijificha na kuwaficha watu hao.
“Taarifa zozote zile?” aliuliza Rais Hamis, muda huo ilikuwa ni saa kumi na moja alfajiri, usiku mzima hakulala alikuwa akiwafikiria watu hao tu.
“Bado hatujawapata mkuu, ila tunahangaika kuhakikisha watu hao wanapatikana haraka iwezekanavyo,” alisikika mwanaume kutoka upande wa pili.
***
Mipango ilikuwa imekamilika, Waingereza walionekana kuwa makini kwa kila kitu walichokuwa wakikifanya, ilikuwa ni lazima wazipate hizo karatasi zilizokuwa na formula ya kutengenezea mabomu ya nyuklia ambayo waliitumia Waarabu na kuwatisha Marekani.
Walichukua namba yake ya simu aliyokuwa akiitumia Uarabuni, namba hiyo walipewa na Backnon ambaye alionekana kabisa kuisaliti nchi yake na kuanza kushirikiana na Waingereza kwa kuamini kwamba ilikuwa siri kumbe wenzake wote walikuwa wakimcheki tu.
Alichokifanya Godson ni kuchukua simu yake na kumpigia Kennedy na kuanza kuzungumza naye. Alimwambia wazi kwamba walikuwa na familia yake, kama kweli alitamani kuiona ikiwa salama kabisa alitakiwa kusafiri kuelekea nchini Uingereza ili awakabidhi karatasi zile zilizokuwa na formula ile.
Kennedy alichokisikia kilimchanganya, kwanza akakata simu na kumpigia mke wake, simu haikuwa ikipatikana, alichanganyikiwa na kuhisi kwamba kweli inawezekana kweli watu hao walikuwa na familia yake.
Aliziangalia karatasi alizokuwanazo, zilikuwa muhimu sana ambazo hakutakiwa kuwa nazo mtu yeyote zaidi ya maofisa wa CIA waliokuwa nchini Marekani, ile simu ambayo alipigiwa ilimchanganya, simu ambayo ilimwambia achague kitu kimoja, kama ni familia ama nchi yake aliyozaliwa.
Backnon alijua kila kitu, hata alipomuona rafiki yake huyo amebadilika alijua tu sababu ilikuwa nini. Hakumwambia kitu zaidi ya kubaki kimya huku akiendelea kufuatilia kile kilichokuwa kikiendelea.
Safari yao hiyo iliishia uwanja wa ndege ambapo hapo wakapanda ndege na kuanza kurudi nchini Marekani. Hapakuwa na mtu aliyegundua kama yeye ndiye alikuwa yule Ibrahim ambaye aliheshimika, aliyepewa kila kitu alichokitaka huku Waarabu wakiona kama alikuwa Mungu.
Kama alivyokuwa kipindi cha mwisho wakati akizungumza kwa simu na Godson ndivyo alivyokuwa hata humo kwenye ndege. Aliifikiria sana familia yake, safari ya kwenda nchini Marekani iliingia doa japokuwa alifanikiwa kwa asilimia mia moja kwa kile alichokifuata Uarabuni.
Walichukua saa kadhaa, wakaingia Dubai. Hapo, wakateremka kwa lengo la kusikilizia ndege nyingine ambayo ingewachukua na kuwapeleka Ulaya ambapo huko wangeunganisha mpaka nchini Marekani.
Akiwa hapo wazo likamjia kumpigia simu mke wake kwa mara nyingine, kama ilivyokuwa alipokuwa Iraq ndivyo ilivyokuwa hata hapo kwamba simu haikuwa ikipatikana kitu kilichomfanya kuhisi kwamba inawezekana kabisa ilikuwa kweli, familia yake ilitekwa na watu hao walioonekana kuwa na uhitaji mkubwa wa kile alichokuwa amekwenda kukifuata nchini humo.
Alikaa na kuzungumza na Backnon mambo mengi mno, hakumwambia kuhusu simu aliyokuwa amepigiwa, maneno aliyoambiwa kuhusu familia yake, na hakumwambia kuhusu karatasi alizokuwanazo kwamba zilikuwa zikihitajika nchini Uingereza.
Baada ya saa mbili, wakaendelea na safari yao. Walipofika nchini Uingereza, akafikiria sana kuhusu kuteremka na kwenda kuzikabidhi karatasi hizo kwa kuwa familia yake ilikuwa muhimu sana.
Wakati akifikiria hilo, akahisi inawezekana kile alichoambiwa kilikuwa ni uongo na familia yake ilikuwa salama kabisa. Akaamua kusubiri mpaka muda ambao angefika nchini Marekani na kuangalia kama kweli familia yake ilitekwa ama la.
Huo ndiyo ukawa uamuzi wake wa mwisho na kuondoka zake. Akiwa njiani, akatumiwa barua pepe na kuambiwa hakutakiwa kumwamini Backnon, alikuwa mtu hatari na alishirikiana na Waingereza katika kuhakikisha wanapata kitu fulani kutoka kwake.
Alipoambiwa hivyo ndipo akakumbuka jinsi alivyopigiwa simu. Alikuwa na uhakika kabisa hakukuwa na mtu nje ya CIA na Backnon ambaye aliifahamu namba ya simu aliyokuwa akitumia huko, ilikuwaje apigiwe simu kutoka nchini Uingereza na kuambiwa familia yake ilikuwa mikononi mwao?
“Kwa hiyo huyu Backnon anahusika?” alijiuliza huku akishtuka kwani hakutegemea kuona mtu wake wa karibu, ambaye alishirikiana naye kwenye kila kitu angeamua kumchoma na kutakiwa kuzipeleka karatasi zile nchini Uingereza.
Kitu cha kwanza alichowaambia CIA ni kuhusu familia yake, alihitaji kuiona ikiwa salama kabisa, alitaka kujua kama watu hao walikuwa wazima ama la.
Kuhusu hilo aliambiwa lingefuatiliwa kwa kina na wangempa majibu ndani ya saa moja kama familia yake ilikuwa salama ama la. Alisubiri, alikuwa na hamu ya kutaka kufahamu kilichokuwa kimejiri huko.
Alizungumza na Backnon lakini moyo wake ulikuwa na hofu tele, mwanaume huyo hakuonekana kuwa rafiki yake tena, alikuwa mtu mbaya ambaye alikuwa radhi kuona akiingia kwenye matatizo lakini mwisho wa siku apate kile alichokuwa akikihitaji.
Baada ya saa moja akapigiwa simu kutoka nchini Marekani na kuambiwa familia yake ilikuwa salama na hakukuwa na lolote baya ambalo lilitokea.
“Wapo salama kabisa?” aliuliza huku akionekana kutokuamini alichokisikia.
“Ndiyo! Ipo salama! Kuna nini lakini?” aliuliza Bwana Gordon.
“Hakuna kitu! Nilihitaji kufahamu hilo!” alisema Kennedy.
“Usijali! Ipo salama kabisa!” alisikika Gordon.

Je, nini kitaendelea?
 
Yaani huku nako kuna arosto tena? Hongera madam S. Ingawa sijajua hatima ya Gabriel na watawa!
 
Yaani huku nako kuna arosto tena? Hongera madam S. Ingawa sijajua hatima ya Gabriel na watawa!
NYEMO CHILONGANI
SHAMBULIO LA DAMU
0718069269

Sehemu ya Kumi na Tano.

Scott na maofisa wengine wa CIA walikuwa wakifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea, kwa Kennedy, mwanaume huyo alionekana kuwa muhimu kupita kawaida. Ilikuwa ni lazima wahakikishe kwamba anaingia nchini Marekani salana kabisa.
Muda ulizidi kwenda, siku ambayo waliwasiliana naye na kumwambia kwamba alikuwa njiani kwenda huko ndipo wakagundua kwamba kulikuwa na simu ambayo alipigiwa Kennedy kutoka nchini Uingereza. Hawakujua walizungumza nini lakini baada ya kuifuatilia sana kwagundua kwamba ilitoka katika Shirika la Kijasusi la MI6.
Mpaka kufikia hapo wakajua kabisa kulikuwa na mchezo. Kitu cha kwanza kabisa ambacho walijiuliza ni namna ambavyo MI6 walipata namba ya simu ya Kennedy, kwenye hilo hawakutaka kujiuliza sana kwani tayari waligundua kwamba Backnon alikuwa akifanya mawasiliano na watu hao hivyo kulikuwa na uhakika kwamba yeye ndiye aliyewapa watu hao namba hiyo.
Scott akaagiza watu hao wafuatiliwe kwani tayari alihisi kulikuwa na jambo kubwa ambalo lilitakiwa kutokea mahali hapo ambalo yeye kama yeye hakutaka kabisa kuona likitokea kwa sababu Kennedy alikuwa na karatasi ambazo zilikuwa muhimu mno.
Baada ya dakika kadhaa akaona akipigiwa simu na Kennedy na mwanaume huyo kuuliza kuhusu familia yake, alihitaji kujua kama ilikuwa salama au la. Hapo akapata kitu kwamba inawezekana kabisa kulikuwa na jambo kubwa lililokuwa likiendelea nyuma ya pazia.
Akawaagiza maofisa waende nyumbani kwake kuiangalia familia hiyo na walipofika huko, kitu ambacho waligundua ni kwamba familia hiyo haikuwepo. Wakampigia simu Scott na kumwambia kile kilichotokea, mwanaume huyo alichanganyikiwa, akahisi labda inawezekana mke wa Kennedy alimchukua mtoto wake na kuelekea kazini, akatuma watu huko, jibu walilolipata ni kwamba mwanamke huyo aliondoka muda mrefu sana.
Hilo likawachanganya kupita kawaida, hapo wakapata jibu kwamba inawezekana kabisa familia ya Kenney ilikuwa kwenye matatizo na ndiyo maana kitu cha kwanza kabisa ambacho mwanaume huyo alihitaji kufahamu ni kuhusu familia yake.
Hapo wakapata jibu kwamba inawezekana kabisa familia ya Kennedy ilitekwa na Waingereza na kumwambia kwamba alitakiwa kuhakikisha anapeleka karatasi hizo nchini humo. Ili kumuaminisha kwamba familia yake haikuwa imetekwa, Scott akazungumza naye na kumwambia kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile, familia yake ilikuwa salama kabisa.
Alijua kulikuwa na kosa kumwambia hivyo lakini hakuwa na jinsi, karatasi zile alizokuwanazo zilikuwa muhimu kwao kuliko kitu chochote kile. Wakati akiwa amemwambia hivyo, aliwaambia maofisa wake wahakikishe familia ya Kennedy inapatikana haraka iwezekanavyo kwani bila hivyo kusingekuwa na uhakika wa kuzipata karatasi hizo.
Maofisa hao wakaondoka kwa lengo la kufanya kazi hiyo lakini pia alimtumia ujumbe Kennedy kwamba alitakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha anamuua Backnon kwani tayari alionekana kuwa adui wao ambaye hakutakiwa kuishi kabisa.
Kennedy aliwaambia ugumu wa kufanya hivyo ila walitakiwa kumtumia mtu mwingine kabisa kwa ajili ya kufanya kazi hiyo. Kwa Scott hakukuwa na tatizo, Wamarekani walijipanga, kwenye kila ndege ambayo ilikuwa ikikanyaga ardhi ya Marekani ilikuwa na mhudumu ambaye aliwekwa na CIA, hiyo ilitokana na shambulio la kigaidi ambalo lilitokea Septemba 11/2001.
Kennedy akawaambia kabisa kwamba kwa mazingira yaliyokuwepo ndani ya ndege lingekuwa suala gumu kufanya hivyo, walitakiwa kumtuma mtu ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo kama mhudumu kwa ajili ya kumuua mwanaume huyo.
Wakati akiwasiliana na Scott, Backnon alijifanya amelala lakini muda mwingi alikuwa akimfuatilia Kennedy kwa kujaribu kuangalia simu yake lakini alishindwa kabisa kuyaona mazungumzo yao. Alijua kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea na ilikuwa ni lazima afanye kitu chochote kile, wakitua Marekani tu akimbie zake na kutokomea kusipojulikana.
Huo ndiyo ulikuwa mpango wake lakini kwa upande wa Kennedy, tayari alikuwa na wasiwasi kwamba familia yake haikuwa salama kama alivyokuwa ameambiwa. Alihisi kabisa kulikuwa na tatizo mahali fulani na bosi wake, Scott hakutaka kumwambia ukweli.
Kilichomjia kichwani mwake ni kuondoka na kuelekea nchini Uingereza kama tu angegundua kwamba familia yake haikuwa salama kama alivyokuwa ameambiwa. Haraka sana akakata tiketi kwenye mtandao wakati ndege ikiwa imetulia angani ikiendelea na safari zake, katika anga ambayo waliruhusiwa kutumia huduma ya internet ndani ya ndege hiyo.
Akapata tiketi ya ndege ambayo ilikuwa ikiondoka ndani ya dakika saa moja na nusu baada ya ndege hiyo kutua nchini Marekani. Akawa nayo kwenye barua pepe yake na kitu pekee alichokuwa akikisikilizia ni kwa ndege hiyo kutua nchini Marekani na kuondoka zake kurudi nchini Uingereza.
Baada ya nusu saa, mhudumu mmoja wa kike akawasogelea pale walipokuwa huku akiwa na vinywaji kwenye chombo chake na kumuuliza Kennedy alikuwa akitumia kinywaji gani. Akasema hatumii chochote kile, akamuuliza Backnon ambaye alikuwa wa kwanza kabisa kwenye kiti kile cha watu wawili na yeye kusema kwamba hatumii chochote.
“Sawa,” alisema msichana huyo na kuanza kuondoka, alipoona amesimama pembeni ya Backnon kwa nyuma, akachukua sindano aliyokuwa nayo na kwa haraka sana kumchoma mwanaume huyo shingoni kwa nyuma.
Backnon akashindwa hata kupiga kelele, alishtuka tu na hapohapo usingizi mzito kumpata. Kennedy hakushtuka, alijua kilichokuwa kikiendelea, hivyo akatulia lakini akiwa makini kabisa kuhakikisha kwamba mchezo kama ule hauchezwi kwake hata kidogo.
Ndege iliendelea na safari, aliona kabisa kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kuhusu familia yake hivyo ilikuwa ni lazima afanye kila liwezekanalo kuhakikisha anaiokoa familia hiyo popote pale ilipokuwa.
Wakati safari hiyo ikiendelea ndipo akakumbuka kwamba ni lazima afanye kitu kimoja kwa ajili ya kuondoka salama katika ndege hiyo kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, alihisi kabisa uwanja wa ndege kungekuwa na maofisa wa CIA ambao walikuwa wakimsubiri, wamchukue na kuelekea naye ofisini kwa ajili ya kuwakabidhi karatasi zilizokuwa na formula hiyo.
“Ni lazima nifanye kitu,” alisema Kennedy.
Hicho ndicho alichokifikiria, hakutaka kuona akishikiliwa na kupelekwa makao makuu na kukabidhi formula ile na wakati hakujua kuhusu familia yake.
Haraka sana akafungua begi lake dogo na kuchukua koti kubwa na kulivaa ambalo lilikwenda mpaka karibu na magoti yake, akaondoka na kuelekea chooni, huko ilikuwa ni lazima apange mipango mipya kuhakikisha hakuna mtu anayemshtukia kwa lolote lile. Kule chooni, akaufungua mlango kidogo na kuangalia upande mwingine, aliuona mlango ambao uliandikwa ‘Staff’ akajua tu humo kulikuwa na nini.
Akatoka chooni huku akiangalia huku na kule, akaufungua mlango huo na kuangalia ndani. Akakutana na nguo nyingi za wahudumu pamoja na za marubani. Kwa pembeni kabisa kulikuwa na sehemu ambayo ilitengwa kwa ajili ya mizigo ya abiria.
Haraka sana akaanza kuzifuata nguo za marubani, alipokaribia mahali zilipo, akamuona msichana mmoja akiendelea kupanga nguo nyingine, kwa kuwa hakuwa ameonekana na msichana yule alimpa mgongo, akamsogelea, alipomfikia, akamkaba kwa nyuma, si kwa lengo la kumuua bali kumzimisha kwa muda.
Ni ndani ya sekunde chache tu msichana huyo akatulia na kumuweka chini. Akachukua vazi moja la rubani, akalivaa, kwa juu akavaa na koti lake kama kulificha na kisha kutoka ndani ya chumba kile huku akiwa ameishika kofia yake kwa kificho.
Alifanikiwa, hakuonekana, alitulia kwenye kiti na wakati huo ndege iliondoka nchini Canada na kuelekea Marekani baada ya kumaliza kuvuka katika Bahari ya Atlantiki.
Baada ya nusu saa, wakaambiwa wafunge mikanda, haraka sana akafanya hivyo na ndege kuanza kutua. Iliposimama, abiria wakaanza kuteremka, hakutaka kuwa na presha, akatoka na kurudi chooni, humo alisubiri kwa dakika kadhaa, alipohakikisha kwamba abiria wote wametoka, akavua koti lake, akabaki na mavazi ya rubani, akavaa kofia na kuanza kuteremka.
Kwa kumwangalia ilikuwa ni vigumu kugundua kama hakuwa rubani, alifanana vya kutosha, alikuwa akitembea kwa mwendo wa kawaida na kwenda kwenye mlango maalumu na kupita.
Maofisa kadhaa wa CIA walikuwa hapo, walimwangalia kila abiria aliyekuwa akiteremka, ilikuwa ni lazima wamchukue Kennedy na kuondoka naye mahali hapo lakini kitu cha ajabu kabisa mpaka abiria wanamalizika, mwanaume huyo hakuonekana.
“Vipi?” aliuliza Scott kwenye simu, alikuwa akimuuliza Kennedy.
“Hayupo!”
“Hayupo? Unamaanisha nini kusema hayupo?” aliuliza huku akiwa amechanganyikiwa.
“Yaani hatujamuona!”
“Hamjamuona? Kivipi?”
Kila swali alilouliza na kupewa jibu, aliibuka na swali jingine. Kile alichoambiwa hakukiamini kabisa, alichojua ni kwamba Kennedy alitoka Dubai akiwa amepanda ndege hiyo baada ya kubadilishwa, sasa ilikuwaje mwanaume huyo asiwepo.
Akahitaji kupata taarifa kutoka ndani ya ndege. Akaambiwa kwamba kulikuwa na tatizo, kuna mwanaume ambaye alichukuliwa na kukabidhiwa kwao, alikuwa Backnon lakini pia kulikuwa na jingine.
“Lipi?”
“Kuna mtu alivamia kwenye chumba cha nguo na kumzimisha mhudumu kwa muda,” alisema mwanaume huyo.
“Huyo ni Kennedy,” alisema Scott huku akishusha pumzi ndefu.
Wakafuatilia na kugundua kwamba kulikuwa na nguo za rubani zilikosekana humo, ilipotea katika mazingira ya kutatanisha lakini wakajua kabisa kwamba ni Kennedy ndiye ambaye alihusika kuzichukua nguo hizo.
Wakaondoka hapo na kuelekea katika chumba kimoja kwa lengo la kuangalia kwenye kamera ndogo za CCTV ili kuona kilichotokea. Huko, wakamuona Kennedy akitoka kwa kupitia mlango wa marubani, hakuonekana kuwa na hofu, alijiamini na alitembea kwa kujiamini kana kwamba alikuwa rubani kweli.
Mpaka kufikia hapo wakakubaliana kwamba walimkosa hivyo ilikuwa ni lazima wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha anapatikana kwa sababu mtu huyo alikuwa muhimu mno.
Tayari maofisa wengine wa CIA walikuwa nyumbani kwake, waliizunguka kwa mbali kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kuonekana. Walikuwa wakimsubiria Kennedy ambaye waliamini ni lazima afike humo kwa lengo la kuangalia kama kulikuwa na familia yake ndani ya nyumba.
“Tuvamie?” aliuliza mwanaume mmoja.
“Hapana! Subirini mpaka atakapokuja,” alisikika Scott kutoka upande wa pili.
“Sawa. Tunasubiri! Tutakupa taarifa!” alisema mwanaume huyo huku kila mmoja akiwa na uhakika kwamba ni lazima Kennedy angefika nyumbani hapo kwa lengo la kuhakikisha kama familia yake ilikuwa humo kwani kila alipokuwa akimpigia simu mke wake, hakuwa akipatikana.

Je, nini kitaendelea?

Kwa sababu mambo ni mengi na muda mchache, naomba hadithi hii niitolee kitabu chake kwa sababu ni ndefu mnooooo.

Kitabu kitakuwa sh. 10,000 tu. Kuna watu wengine watatu....Boniface ambaye anawania urais Tanzania.

Kuna Diana ambaye alitumwa Uingereza kumpeleleza muuza madawa ya kulevya, Wayne.

Pia kuna Bianca ambaye alikuwa mpenzi wa bilionea wa Dubai aliyempa almasi iitwayo Waridi ambayo ilikuwa inakatazwa kuuzwa kwa kuwa ilihusika na kumwaga damu za watu huko Siera Leone.
 
Madame asantee kama naona mapovu ya uko fb
 
Kumbe kuna mambo mazuri huku nilikuwa sijaona.
 
Ndege kubwa ya shirika la ndege la Orange Airlines, Airbus A350-900 inapotea angani ikitokea nchini Marekani kuelekea Dubai kwa kupitia viwanja kadhaa barani Ulaya.

Hilo linaibua hofu nzito, Marekani na mataifa mengine wakiongozwa na shirika la anga duniani, NASA yanaanza harakati za kuitafuta ndege hiyo.

Wanakwenda baharini, kwenye milima ya Himalaya, Everest, kwenye Pembetatu ya Bermuda lakini kote huko hawafanikiwi kuipata ndege hiyo.

Mbali na abiria 550 waliokuwa humo, kati yao kuna abiria watano ambao ndiyo walipelekea kupotezwa kwa ndege hiyo.
Kuna Gabriel: Huyu alikuwa mwanaume aliyepewa picha za utupu ambazo zilionyesha watawa wakifanyishwa mapenzi kinguvu akiwemo dada yake. Picha hizo zilimuumiza mno lakini kabla ya kwenda huko, dada yake na marafiki zake wawili, wanauawa kuificha siri hiyo, hivyo anaamua kwenda huko kuzipeleka picha hizo, mbaya zaidi anagundulika hivyo kutakiwa kupotezwa kabla ya kutua Ubelgiji.
Boniface Ngumije: Huyu jamaa alikuwa akigombea urais nchini Tanzania. Alitakiwa kumtoa madarakani Rais Hussein Sanura. Wakati ikigundulika kwamba yupo ndani ya ndege hiyo, mipango inasukwa ili ipotezwe angani.
Bella: Huyu alikuwa mwanamitindo nchini Marekani ambaye alipewa zawadi ya Almasi ya Warda na mpenzi wake bilionea kutoka Dubai. Wakati imegudulika almasi hiyo imetokana na damu zilizomwagika Liberia, inabidi bilionea akamatwe na Bella kutakiwa kwenda Dubai kutoa ushahidi ili jamaa afungwe, hivyo mpango wa kuipoteza ndege unaanza kusukwa.
Diana: Msichana huyu naye alikuwa ndani ya ndege hiyo akipeleka ushahidi wa kumfunga muuza madawa ya kulevya, Wayne wa nchini Uingereza.
Kennedy: Huyu ni mpelelezi wa CIA ambaye alitumwa nchini Iraqi kuhakikisha anapata formula ya kutengeneza mabomu wanayoitumia Waarabu. Anaipata ila anapofika Marekani, familia yake inatekwa na hivyo kutakiwa kuwapa formula hiyo Waingereza. Anaingia ndani ya ndege hiyohiyo kwenda huko, bahati mbaya, ndege inapotezwa.
Vitabu hivi vitaanza kupatikana Jumamosi nchi nzima kwa bei ya shilingi 10,000/=.
Dar es Salaam.....0718069269.
Kona ya Riwaya, Kinondoni......0655228085
Posta....0713454152
Mwanza.....0762337673.
Mbeya... ....0625726640
Dodoma...0719422001
Zanzibar... 0674294643
Arusha, Moshi, Morogoro...kote vitapatikana.
 
Back
Top Bottom