Shaka: Wanaotaka Urais 2025 wasahau, ni Rais Samia bara ni Rais Mwinyi visiwani mpaka 2030

Mkuu, hapo umenena na nakubaliana na hoja yako kabisa vinginevyo wamekalili nguvu ya upinzani iko wapi lakini pia ni kikali kuwa ukishapitishwa na Chama, basi ushindi lazima vinginevyo nikujifariji tu.
Nami nasema nafasi hiyo igombewe na wanaohitaji badala ya kutaka kuminya nafasi hiyo.
 
2025 ccm tutatumia busara ya kuprint fomu moja kwa ajili ya Samia, na mkutano mkuu utampitisha Samia kwa kishindo.
 
Naona unampigia chapuo, binafsi nitamfanyia tathimini baadaya yakukaa madaraka miaka miwili,lakini hadi sasa,mm kama mdau,sioni kama anafaa kuendelea kupewa nafasi hiyo ya uraisi ifikapo 2025 vinginevyo kuwe na mwelekeo mpya.
Nasubili miaka miwili ifike.
2025 ccm tutatumia busara ya kuprint fomu moja kwa ajili ya Samia, na mkutano mkuu utampitisha Samia kwa kishindo.
 
Hata wakati wa mwendazake mlisema hivyo hivyo ila 2020 moto ukawaka mpaka akatumia polisi,tiss na tume kujitangazia ushindi wa kishindo.

Waamuzi wa kumuajiri rais ni wananchi lakini kwa makusudi watanzania wameporwa haki hiyo. Tutakuja kuelewana tu mbele ya safari.
 
2025 Mama hanampinzani amebeba matumaini ya wengi, ndani ya mwaka mmoja amejenga madarasa 15000, amejenga vituo vya afya vijijini na miji midogo, amefanya kazi ya miaka 5 ndani ya mwaka mmoja na anaendelea kufanya
 
Maneno yenye hekima na ndio ukweli huo.
 
Kweli umelambishwa. Huoni kinachoendelea hapo jirani uchaguzi uliopita.
Huu ujinga unafanya wenye tume wanyanyase sana wagombea wengine.
KATIBA MPYA na Tune huru tunataka Haki na ukweli.
 
Maneno yenye hekima na ndio ukweli huo.
Hata hayati JPM tulifanya hivo hivi hata wengine walidhiriki kumfananisha na Muumba na alikuwa atawale maisha ila mwenye haki alifanya aaliyoona yeye. ! Punguzeni sifa na kumpamba huwez kujua wako wanapata tabu na Muumba anawajali pia.
 
Comrade Shaka mwenyewe tunahisi ni moja ya watu wanaomhujumu Rais Samia asigombee 2025. Ona mfano Comrade Kinana anavyotoa kauli ili Rais Samia akose uungwaji mkono 2025. Juzi hapa kasema traffic wapungue na tangu hiyo kauli itoke watu wengi wanakufa, foleni mfano barabara ya Morogoro toka Bwawani mpaka mikese ilikuwa haipitiki. Kikubwa wanajikusanyia pointi kusema Rais Samia hawezi, ona watu wanakufa wengi kwa ajali, huku Makamba akihakikisha bei ya mafuta inapanda kila kukicha, huku waziri wa kilimo akihakikisha wananchi wanauzia chakula shambani lengo ni kutengeneza taharuki nchi iwe vibaya na mwisho alaumiwe Rais Samia.
 
Kuna watu wanatoa Maoni mpaka unaghabika kiasi cha kutamani umtwange mtu Risasi. Hivi kweli huyu Shaka angalikuwa anajua Uongozi unatolewa Kwa wananchi kuamua kupitia Sanduku la Kura huyo Shaka angalitamani huyo mama agombee kweli kupitiq Chama Chao? Hivi kweli Uongozi wa Nchi umeshafikishwa kwenye level hiyo ya kugawiana zamu hata kama uwezo wa mtu ni Zero. Leo nilikuwa naongea na Mzee mmoja alipigana Vita ya Kagera na ni Mwana-CCM lakini hataki kabisa kumsikia huyo mwanamama! Anasema anaibiwa sana na sababu ni kwamba hajui Hesabu.
 
Ndio maana kila wakati nasema huyu mama naye IQ yake ni Zero. Magufuli alikuwa huwezi kumsifia namna hiyo na asikueleze ukweli. Namkumbuka Kangi Lugora alimaliza kusifia lakini akamtumbua. Sasa huyu ukichanganya na Jinsia yake kuwa wanawake wanapendwa kusifiwa hapo ndio wamemfikisha kabisa. Utashangaa watu wamemwambia ukweli kuwa Turn out ya wananchi kwenye Mikutano yake haitishi yeye kaona huo sio ukweli. Anataka wamwambie anapata Nyomi. Bure kabisa!
 
Utamaduni huwa unabadilika kulingana na uhitaji wa nyakati. CCM inapigia debe utamaduni huu lakini ipo siku utawatokea puani.

Suppose wamechagua mgombea lakini kwenye angu yake ya kwanza akaonekana ameshindwa kazi, je atavumiliwa mpaka miaka 10 iishe?

Leo yupo SSH tunasifia kesho hatujui ataletwa nani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…