Shaka Hamdu Shaka atuma neno kwa Freeman Mbowe amsifu Rais Samia

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
May 27, 2020
1,450
799
IMG-20220305-WA0012.jpg


"Ibara ya 118 ya ilani ya uchaguzi ya CCM inaeleza Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuheshimu na kulinda misingi ya demokrasia na haki za binadamu kwa ajili ya kudumisha umoja, amani na ustawi wa Taifa kwa kuzingatia Katiba ya Nchi"

"Namshkuru Mhe Freeman Mbowe kwa kuonesha uungwana kwa sababu amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujali na amemuahidi kumpa ushirikiano kwa ustawi wa Tanzania.

Hiyo ndio siasa safi na hiyo ndio Tanzania tunayojivunia"

"Chama Cha Mapinduzi kinawahakikishia watanzania kuwa kitaendelea kuisimamia Serikali izidi kuimarisha Uhuru wa maoni, misingi ya haki na demokrasia ili kujenga taifa lenye upendo, umoja, amani na mshikamano wakati wote."

"Siasa safi inahusisha uzalendo, utu, heshima na kuweka mbele maslahi ya Taifa kuliko chochote.

Rais Samia ni kielelezo katika hili na ameendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuijenga Tanzania moja yenye ustawi kwa wananchi wote. Tumpe ushirikiano."

" Lengo la CCM katika kipindi hiki ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata haki kwa mtu mmoja mmoja na makundi
mbalimbali.

Tunampongeza Rais Samia kwa kuendelea kutekeleza maelekezo haya ya ilani kikamilifu hakika Kazi inaendelea vyema."

Hakika kwa sasa ccm-tanzania ina msemaji anayezungumza kwa hekima,akili,busara,Utu na Utulivu na anazungumza vitu vinavyoeleweka kama Msemaji Wa Chama Tawala, Heko Mhe Shaka Hamdu Shaka kwa kukibeba na kukiheshimisha vema Chama Chetu


05 Machi 2022
Gymkana, Dar Es Salama
#366zaSamia
#KaziKubwaImefanyika
#KaziIendelee

<<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
 
CHADEMA ni kunguru hafugiki, Hongera Sana Rais Samia,

Wewe ni zaidi ya Rais, Wewe ni mtumishi wa Mungu,
 
Kwani kwa mujibu wa kesi ya Mbowe anayemfanyia fujo mwingine ni nani!

Ili tuheshimike ndani na nje ya nchi vijana viongozi wa baadaye mjifunze na kuzoea kutafuta na kusema ukweli.

Ukweli ndiyo utawaweka huru,utawapa amani na maisha marefuu!!
 
Mbowe kwani wakati anatungiwa kesi ya mchongo,hiyo ilani yenu ilikuwa haijaandikwa?

Hamjamuachia Mbowe kwa sababu mnafata haki za binadamu,mmeona aibu,

Dunia nzima inawacheka,sasa hv mtajikosha tu,lakini wenye akili tunajua,hapa mta justfy kila kitu kwa hayo makaratasi yenu,lakini jiulizeni hiyo ilani mlikuwa hamjaisoma Wala mlikuwa hamuifati wakati mnatunga hiyo kesi?

Sasa malaika kawashukia ndio mnaifata?!!
 
Lile shetani lililokufa mwaka jana si lilikuwepo wakati hiyo Iran ipo?
MBowe kwani wakati anatungiwa kesi ya mchongo,hiyo ilani yenu ilikuwa haijaandikwa?
Hamjamuachia Mbowe kwa sababu mnafata haki za binadamu,mmeona aibu,Dunia nzima inawacheka,sasa hv mtajikosha tu,lakini wenye akili tunajua,hapa mta justfy kila kitu kwa hayo makaratasi yenu,lakini jiulizeni hiyo ilani mlikuwa hamjaisoma Wala mlikuwa hamuifati wakati mnatunga hiyo kesi??
Sasa malaika kawashukia ndio mnaifata?!!ccm na akili za makalio
Wasitufanye mazuzu, mnamuweka mtu ndani muda wote huo anakosq opportunities halafu leo mnamuambia hizo ndio siasa?

Mnadhani yeye fala?

Subirini calculated reactions.
 
Kujipendekeza kwingine hadi wanaharibu.

Kukaa kimya nayo ni busara.
 
NUKUU ZA KATIBU WA NEC - ITIKADI NA UENEZI WA CCM TAIFA NDG. SHAKA HAMDU AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA BENKI YA CRDB JIJINI DAR ES SALAAM, LEO MACHI 05,2022 .

#ChamaImara
#KaziIendelee
IMG-20220305-WA0024.jpeg
IMG-20220305-WA0023.jpeg
IMG-20220305-WA0022.jpeg
IMG-20220305-WA0021.jpeg
IMG-20220305-WA0020.jpeg
 
NUKUU ZA KATIBU WA NEC - ITIKADI NA UENEZI WA CCM TAIFA NDG. SHAKA HAMDU AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUZINDUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA BENKI YA CRDB JIJINI DAR ES SALAAM, LEO MACHI 05,2022 .

#ChamaImara
#KaziIendeleeView attachment 2140435View attachment 2140438View attachment 2140440View attachment 2140441View attachment 2140442
Kwa hiyo yeye ndiye aliyeratibu maongezi ya Rais na Mwenyekiti FAM jana au basi ndio walewale wanaona wawahi siti ya mbele kabisa kabla hajaongea mhusika akatema madini yote.

Shaka njaa nyingi ridhika ulipo.
 
Shaka huna mahali ccm ,nyi ndo mlikuwa mnamdharau mama na mwenzio yule (ushaelewa) waomba msamaha mlikosa sana mlikosa ninyi bro kalime ccm hatukutaki na waitara
 
Hivi hawa watu walitaka Mbowe aendelee kukaa jela?

Ametolewa kelele, akikaa ndani kelele...Hivi watu wapo sawa sawa kweli.

Mbowe mwenyewe ameridhia kukutana na Rais, sasa hao wanaoongea ongea ovyo wanataka nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom