Shaka aambiwe hata kukosolewa Rais Samia ni uhuru wa maoni binafsi

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
Huu upuuzi wa eti akikosolewa fulani ni kosa na hali ikiwa vilevile kwa mwingine eti ni uhuru wa maoni si sawasawa kabisa.

Jana amenukuliwa Shaka msemaji wa CCM akisema wale wote walio mshambulia Ndugai eti wametoa maoni yao binafsi na ni uhuru wao.

Ajabu kupitia huohuo uhuru wa maoni binafsi akikosolewa Rais Samia ni kosa!

Si sawasawa hata kidogo.
 
Tabia ya kufungana midomo inazidi kuota mizizi, na hii inasababishwa na teuzi zinazotolewa kwasababu ya kujipendekeza kwa viongozi, matokeo yake wengi wa wateuliwa wanageuzwa watumwa wa kifikra wa mabosi, wao wanachojua ni kusifia tu, na kuwatisha wanaowapinga hata kama ni kwa hoja.
 
Tabia ya kufungana midomo inazidi kuota mizizi, na hii inasababishwa na teuzi zinazotolewa kwasababu ya kujipendekeza kwa viongozi, matokeo yake wengi wa wateuliwa wanageuzwa watumwa wa kifikra wa mabosi wao.
...ni kweli kabisa.
 
Watu wanahangaika sana kuulinda ugali.

Siku Samia akiachia madaraka atajua hajui. Marafiki feki ni wengi sana.
 
Wewe naye umezidi, sijui unanufaikaje kwa kumuongelea vibaya Rais wa Tanzania, huchoki? Kila uzi wako ni kumsema vibaya, hana jema au zuri alilolifanya kwa muda mfupi?? Mpe heshima yake hata kama hajakuzaa.
 
raisi huwa anapongezwa hakosolewii nani alikwambia baba nyumbani huwa anakoseaaa .......mara nyingi anapitiwa tuuuu
 
Wewe naye umezidi, sijui unanufaikaje kwa kumuongelea vibaya Rais wa Tanzania, huchoki?? Kila uzi wako ni kumsema vibaya, hana jema au zuri alilolifanya kwa muda mfupi?? Mpe heshima yake hata kama hajakuzaa.
Jikite kwenye mada.
 
Huu upuuzi wa eti akikosolewa fulani ni kosa na hali ikiwa vilevile kwa mwingine eti ni uhuru wa maoni si sawasawa kabisa.

Jana amenukuliwa Shaka msemaji wa CCM akisema wale wote walio mshambulia Ndugai eti wametoa maoni yao binafsi na ni uhuru wao.

Ajabu kupitia huohuo uhuru wa maoni binafsi akikosolewa Rais Samia ni kosa!

Si sawasawa hata kidogo.
Tutofautishe "Uhuru" na "Haki"
 
Back
Top Bottom