benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Wiki hii Tanzania imekuwa na aJenda moja kubwa tu kuanzia vijiweni, kwenye vyombo vya habari, kwenye vyombo vya usafiri mpaka kwenye sehemu za kupiga pombe.
Kila mmoja amekuwa akijadili mkataba ulioridhiwa na Bunge leo kati ya Serikali ya Tanzania na ile ya UAE kuhusu masuala ya uendeshaji na uendelezaji wa bandari.
Baada ya mijadala mingi, ikiwemo ya kujenga, kukosoa, kupotosha, kuelimisha, kufundisha mimi nimetoka na jambo moja kubwa sana.
Baada ya kupitishwa kwenye tanuru la moto na kuminywa kwa wale wote waliokuwa wakiikosoa na kuisema serikali wakati wa awamu ya mwendazake, hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan ameirudisha nchi katika mstari ambao watanzania wanaweza kutoa maoni bila woga wa kutekwa wala kupotea,
Rais Samia amerudisha uhuru wa kujieleza na kutoa maoni nchini, ambapo leo kupitia bunge live ambalo aliridhia kurejeshwa kwake tumeshuhudia mjadala wa wazi wenye kujenga na kusimamia maslahi ya taifa.
Ndugu zangu wanajamvi, kwa hili Rais Samia tumpe maua yake ya kutosha: