Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 3,132
- 16,357
Katika muendelezo wa kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Shahidi wa nane wa Jamhuri dhidi ya Sabaya ameieleza mahakama kuwa hakumshuhudia mumewe akipigwa kama alivyoeleza. Pia, ameeleza bayana kuwa simu zake hazikuchukuliwa kwa sababu mumewe alipofika alitoa simu alipokuwa amezificha Sehemu zake za siri.
Hii ni baada ya siku chache zilizopita Bakari Msangi kuieleza mahakama kuwa alipigwa karibia kufa kisha kufungwa pingu miguuni.
Kesi hiyo inaendelea kunguruma katika mahakama ya hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha chini ya Hakimu Mfawidhi Odira Omworo.
Hali hii imeleta mkanganyiko baada ya Shahidi huyo kwenda kinyume na ushahidi alioutoa mumewe.
Kesi imefikia pazuri.
-----
Shahidi wa nane wa Jamhuri katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake amesema hajawahi kumuona Sabaya akiwa anampiga Mume wake Bakari Msangi.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo akiulizwa maswali na wakili wa utetezi Dankan Oola, Shahidi huyo amesema kwa wakati wowote hakushuhudia Sabaya akimpiga Mumewe Bakari Msangi.
Amesema wakati Bakari anampigia simu waliongea na kumuambia ametekwa na baadaye aliposhuka kwenye gari ya Sabaya alikuwa wala hajafungwa pingu mguuni.
Shahidi huyu ameendelea kusema Mume wake hakuibiwa simu na aliporudi nyumbani alikuwa na simu zake zote na alimpa baada ya kuzitoa kwenye sehemu za siri.