Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Inaelekea habari hii ina mawaa/uongo kwani Bombardier zimekuja juzi tu na kabla ya hapo ATCL hawakuwa na ndege aina ya Bombardier
Kaka ATCL kabla ya kununuliwa hizi ndege sita mpya za Magufuli walikuwa na Bombardier mbili zenye namba za usajili 5H-MWG, na 5H- MWF, tofauti ya hizo ndege za zamani na hizi bombardier mpya za Magufuli ni model, hizi mpya ni Q400 na zina speed kubwa na capicity ya abiria ni kubwa kidogo kuliko zile Bombadier zetu za zamani ambazo model yake ni DHC8 (kwa sasa ni mbovu na zinahitaji kufanyiwa matengenezo)
 
... ukarabati unaogharimu 13.8b/- kwa ndege mbili ndogo yaani wastani wa 6.9b/- kwa ndege moja yenye umri usiozidi miaka mitatu halafu ni ukarabati wa kawaida? Sina hakika kama zimesharudisha japo 15% ya gharama iliyotumika kuzinunua.
Inaitwa Remanufacturing. Yani ndege inabomolewa yote, wanaanza kurudishia kifaa kimoja kimoja. Vilivyozeeka vinawekwa pembeni na kufungwa vipya.
 
Muwe mnasoma habari in deep. Sio zile mpya. Hii ni bomberdier Q300 ambayo iliharibika kitambo.. hii ilikuwepo zamani kabla ya hizi mpya kuja. Ndio ndege pekee atcl walibaki nayo.

Hizi mpya ni Q400 .inayoenda kufanyiwa matengenezo ni Q300
Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaitwa Remanufacturing. Yani ndege inabomolewa yote, wanaanza kurudishia kifaa kimoja kimoja. Vilivyozeeka vinawekwa pembeni na kufungwa vipya.
... huchukua muda gani kuzeeka? Navyojua hizo ndege ni mpya kwa maana hazina umri wa zaidi ya miaka mitatu! Sitaki kuamini kwamba kila baada ya miaka isiyozidi mitatu ndege inatakiwa ibolewe YOTE na kurudishia kifaa kimoja kimoja! Huu ni wazimu!
 
Ile ya mwanza ilishatengamaa. Na inafanya kazi. Hii ni nyingine kabisa.. ya siku nyingi sana
May be Itakuwa ile bombadier iliyokuwa imekaa mwanza airport kwa miezi kibao ikiwa mbovu!

Nchi masikini kumiliki ndege ni sawa na mtu masikini wa kutupa kumiliki gari, Ataliweka juu ya mawe tu maana gharama zake hatoziweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ni habari nyeusi ila siwezi kushangaa ATCL kuendeshwa kwa Ruzuku kama TTCL na Tanesco Ndiyo maana CAG alitungiwa sheria ya kumzuia asikague ATCL na mashirika mengenine ya umma yanayoendeshwa kwa Ruzuku #2020 Lissu#
 
Ni services ya botmbadier zote. Ni utaratibu kufanyiwa services, waziri wa mawasiliano alilielezea hili ndio maana kuna haja ya kufufua hangar la KIA.
... hilo hangar la KIA litasaidia nini? Vipuri vitatengenezwa hapo? Kwa kiasi kilichotajwa, 13.8 billion, gharama kubwa iko kwenye vipuri kuliko fuel ya kwenda na kurudi Canada. Tena kwa aina ya chombo, yaani ndege, bora wakafanyie huko huko kuliko ubabaishaji wa hapa!
 
Sidhani kama uliyemjibu amesema ni boeing. Lipind cha mkapa atcl (wakati huo ikiitwa atc) . Iliwahi kununua bombadier Q300. Na hii ndio ndege pekee atcl walikuwa nayo.. iliharibika na kupelekwa kwenye hanger.
Hizi mpya ni Q400.
Wewe ndo huache uongo, ndege ile ya Boeing haiwezi kukarabatiwa na kampuni ya bombardier mkuu, ndege husika ni among zile bomberdier za mwanzo. hayo matango poli kawalishe uvccm pale Lumumba

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini mnaaminisha umma mambo ya uongo?? Km huna jambo la kupost la maana si ukae kimya? Chombo chochote kufanyiwa ukarabati ni jambo la kawaida na wala siyo dhambi....kama mnadhani sisi tutarudi nyuma kwa maneno yenu ya kijinga mmekwama,MAGUFULI MBELE KWA MBELE hadi 2025 asiyetaka ruksa kuhama nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja ya msingi hapa ni ndege mbili MPYA zenye umri usiofikia miaka mitatu kufanyiwa service ya 13.8 billion! Huo ndio msingi wa hii habari na sio chombo kufanyiwa ukarabati!
 
IMG_0618.JPG


Kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kuwa, Ndege 2 za Bombardier zitapelekwa nchini Canada kwa service itakayogharimu bilioni 13.9, Mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi, akiongea na TBC leo asubuhi, ameeleza kuwa, kwa kawaida ndege hufanyiwa service kwa masaa na kwamba service kubwa hufanyika kila baada ya ndege kukimbia kwa muda wa masaa 4,000.

Matindi alisema kuwa wakati wa kuifufua ATCL ilikuwa na Marubani 11 lakini kwa sasa ina Marubani 50, kati yao 48 wazawa na 02 wageni.
Mipango iliyopo ni kufikisha marubani 60.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, maboresho makubwa yamefanyika ya kuajiri wahandisi wapya na wa zamani na kufikisha idadi ya wahandisi 80.

Matindi alisema kuwa, wanatarajia kuanzisha program ya kuchukua wanafunzi kutoka vyuoni mmoja kwa moja na kuwafundisha na kwamba watakaoonyesha moyo wa uzalendo na maadili wataajiriwa.

Updates:
IMG_0619.JPG
 
Back
Top Bottom