Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Sh. Bilioni 13.9 kukarabati Bombardier nchini Canada

Ni ile ndege mpya iliyonunuliwa hivi karibuni na kupokelewa kifalmeView attachment 993742

14JAN 2019

Bombardier kukarabatiwa 
Canada kwa bilioni 13.9/-

SERIKALI imesema ndege mbili aina ya Bombardier Dash Q400 zilizonunuliwa mwaka 2016, zitapelekwa kufanyiwa ukarabati Canada mwezi ujao.
Imesema ukarabati huo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni sita (Sh. bilioni 13.860).


WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, ISACK KAMWELWE, PICHA MTANDAO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu ndani ya ndege katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Ndege hizo zilinunuliwa na serikali zikiwa na uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaozitumia kwa safari za ndani ya nchi.


“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe.


Waziri huyo alisema kuwa, baada ya kuletewa taarifa hiyo, alilazimika kumfuata Rais John Magufuli na kumshauri serikali ianze kufanya ukarabati kwa hanga lililopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ili kupunguza gharama kubwa ambazo nchi inaingia katika kuzikarabati ndege.


Alisema katika kulitekeleza hilo, serikali imeshaanza kuchukua hatua kwa kuanza kukarabati hanga hilo kwa kuweka taa na kwamba serikali imeshaingia mikataba mitatu, mmojawapo utakuwa wa kununua vifaa vya matengenezo.
Alisema Rais Magufuli ameshakubali kutoa pesa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vitakavyotumika katika hanga hilo.


“Kwa hiyo, ndugu zangu tutaanza kukarabati ndege sisi wenyewe, nimeamua kusimamia 'industry' inadumu na hakuna kurudi nyuma,” alisema Waziri Kamwelwe.


Kuhusu mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege yaliyoanzishwa na NIT, Waziri Kamwelwe, alisema yatasaidia kupata Watanzania wakaohudumia ndege zilizonunuliwa na serikali.




Aliutaka uongozi wa NIT kuhakikisha mafunzo ya kozi hiyo yanakidhi viwango vya kimataifa.
Mkuu wa NIT, Prof. Zacharia Mganilwa, alisema idadi ya wahandisi wa ndege nchini inaendelea kushuka, akibainisha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na wahandisi 172, mwaka 2016 walikuwa 74, huku asilimia 69 kati yao, wakiwa ni raia wa kigeni.


Prof. Mganiliwa pia alisema zaidi ya asilimia 70 ya matengenezo ya ndege yanafanyika nje ya nchi.
“Tulikuwa na upungufu wa marubani kwa asilimia 60, mwaka 2017, idadi yao ilikuwa 743 kati ya hao 317 walikuwa ni wazawa na 425 ni raia wa kigeni,” alisema Prof. Mganilwa.


Alisema idadi ya wahudumu wa ndege waliosajiliwa nchini imekuwa ikiongezeka tangu serikali ilipoanza kununua ndege.
Alisema mwaka 2013/14, idadi yao ilikuwa 43, mwaka 2014/15 walikuwa 42, mwaka 2015/16 walikuwa 50, mwaka 2016/17 walikuwa 96, mwaka 2017/18 walikuwa 143 na mwaka 2019 waliopo katika mafunzo ni 61.


Alisema kuwa mwaka 2015, NIT ilianzisha shule kuu ya usafiri wa anga ikiwa na idara mbili ya uhandisi wa ndege na wahudumu wa ndege.


Alisema NIT ilipewa ithibati ya kutoa mafunzo ya uhudumu ndani ya ndege Aprili 25, mwaka jana na ithibati ya utengenezaji wa ndege na urubani bado hawajapewa. Alisema kuwa kwa sasa wapo katika hatua ya nne ya kukamilisha matakwa ya kupewa ithibati hiyo.
“Bombadier mbili tulizozinunua tunatarajia kuzipeleka nchini Canada kwa ajili ya kufanyiwa 'service', na ndege moja itagharimu Dola za Marekani milioni tatu,” alisema Waziri Kamwelwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee mwinyi alishasema Tz ni kichwa ya mwendawazi! Watoto wanajifunzia kuzomea, kutukana na watu wazima wanajifuzia kupiga, kukashifu! Zinakarabatiwa kabla ya kuanza kazi!

Ndege ni feki zilinunuliwa kwa cash wajanja wakala 10% sasa wameogopa zikikarabatiwa hapa karibu Siri zitatoka kuwa ni ndege mitumba wameamua kuzipeleka huko mbali kuficha Aibu pia wajanja wanakula 10% kwenye hizo bilion 13
 
... ukarabati unaogharimu 13.8b/- kwa ndege mbili ndogo yaani wastani wa 6.9b/- kwa ndege moja yenye umri usiozidi miaka mitatu halafu ni ukarabati wa kawaida? Sina hakika kama zimesharudisha japo 15% ya gharama iliyotumika kuzinunua.
Sasa dreamliner nahisi service yake itakua billion 80

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha urongo!

hela za matumizi ya serikali hazipitishwi na Rais!

Tunataka kujua hii ni service ya kawaida ama ni ukarabati wa ubovu?

Kama ndege ni mbovu hizi ni terrible teens zimeanza ku rear their ugly face on him

Kama ni ukarabati wa kawaida kwa nini hela inaenda kuombwa nje ya ATCL, haikuwa kwenye business plan?

TUNATAKA MAJIBU!
Madhara ya kununua vitu used huwa havina ''guarantee''
 
Hivi nayo nilikuwa Bomberdiar?

Sent using Jamii Forums mobile app
swq
Ni kawaida lakini kwa bavicha kurukia mada bila uelewa wa kina.
lazima watu wa hoji kwani si zimenunuliwa kwa pesa zetu? au kwakuwa zimenunuliwa chumbani bila kutangaza tenda kama sheria zinavyotaka? unaijua sheria ya manunuzi ya umma wewe au unaropoka tu hapa? mlishindanisha makampuni mangapi?
 
Faida hazina mkuu ndio maana huoni mbwembwe za kuambiwa faida zake, siku zikianza kuzalisha faida utaona tu mbwembwe za jiwe kila kwenye hadhira tutakuwa tunatangaziwa kila siku

2020 John Walker out

hawezi kuzalisha faida

it will never ever happen!

only one airline in Africa is profitable

na hao wanaokula hasara, Kenya Airways, South Africa, Egypt, Rwanda, Morocco na kadhalika na kadhalika hatujawafikia hata robo kwa ujuzi wa biashara, mtaji, experience, equity line, viwanja vya ndege, ndege, nk...

ATCL ikizalisha faida bila serikali ku foji vitabu Magu atapewa Nobel Peace Prize on Economics!
 
Ni services ya botmbadier zote. Ni utaratibu kufanyiwa services, waziri wa mawasiliano alilielezea hili ndio maana kuna haja ya kufufua hangar la KIA.

Tatizo lenu ni kuamini kuwa kila Mtanzania ni mbumbumbu na msahaulifu. Haiwezekeni kuwa na ndege ambayo scheduled maintenance yake inagharimu USD 3 millions kila baada ya miaka miwili halafu mfanyabiashara mwenye akili timamu akainunua. Siamini kuwa ndege aina ya bombadier 400q (au yeyote yenye carrying capacity sawa) inaweza kuingiza revenue ya USD 3 millions ndani ya miaka miwili, sasa ununue ndege inagharimu zaidi ya pato lake?
Ni ccm pekee wanaoweza kutoa kiroja cha namna hii
 
Back
Top Bottom