Serious note ya Godbless Lema juu ya mapungufu ya taaluma, utaalamu, uzembe, elimu ndogo, UONGO ndani ya mifumo ya VYOMBO vya Usalama wa Taifa

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
50,136
Reaction score
96,161
Anaandika Godbless J Lema

TAARIFA ZA UONGO NA MATESO NA MAUAJI YA RAIA.

Mwaka 2011, jijini Arusha, kulitokea sakata zito la mauaji yaliyosababishwa na Polisi kufuatia maandamano ya wananchi waliopinga uchaguzi Meya feki wa Arusha Mjini. Tukio hilo liliacha majeraha makubwa katika mioyo ya wananchi na maswali mazito kuhusu matumizi ya nguvu za dola dhidi ya raia wasio na hatia.

Katika mazingira hayo, Waziri Mkuu wa wakati huo, Mizengo Pinda, aliwasilisha taarifa Bungeni ambayo haikuwakilisha ukweli kamili wa kilichotokea Arusha. Nilihisi dhamira yangu ya uongozi na uwakilishi wa wananchi inanitaka nisikae kimya. Nilisimama hadharani na kusema wazi kuwa taarifa hiyo ilikuwa ya uongo.

Nilimwambia Waziri Mkuu kuwa alidanganya Bunge, na kwamba uongo aliousema angeweza hata kumfundisha shetani mbinu za uongo. Nilisisitiza kuwa nilikuwa na ushahidi wa kuthibitisha nilichokisema. Spika wa Bunge, alinipa siku saba kuwasilisha ushahidi huo, la sivyo ningechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge.

Nilimjibu Spika kuwa sikuhitaji siku saba. Nilihitaji muda mfupi tu kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kwenda hotelini na kuleta ushahidi mara moja. Ilikuwa hali ngumu na yenye mvutano mkubwa wa kisiasa, lakini nilikuwa tayari kubeba gharama ya kusimama upande wa ukweli.

Baada ya Bunge kuahirishwa mchana, Waziri Mkuu alituma wasaidizi wake wanitafute, akitaka nionane naye ofisini kwake. Niliitikia wito huo. Tulipobaki wawili, aliniambia kwa sauti ya utulivu lakini yenye uzito, “ Lema, umeniita muongo hadharani kwa sauti kali sana. Unadhani uongo wangu ulikuwa upi? Tafadhali nieleze.”

Nilimweleza kwa kina kila nilichokijua kuhusu sakata la Arusha, alisikiliza kwa makini, akashika kichwa kwa mshangao, kisha akasema kwa unyenyekevu mkubwa

“Sasa nimekuelewa. Hatuhitaji kuendelea kulumbana ndani ya Bunge. Wewe potezea, nami nitamjulisha Spika asikufuatilie suala la ushahidi. Nitakuja Arusha kushughulikia jambo hili kwa kina zaidi. Kisha akatoa kauli ambayo hadi leo naona ina uzito mkubwa kwa mustakabali wa nchi yetu:

Lema, alisema , tatizo letu kubwa sasa liko kwenye recruitment ya vijana wanaoingia kwenye vyombo vya usalama. Kazi ya intelijensia ni kusema ukweli ulivyo, ili viongozi wapate mwelekeo sahihi wa kutawala. Kwa sasa tuna changamoto kubwa ya aina ya watu tunaowaajiri. Kuna kazi kubwa sana ya kufanya.”

Maneno haya yanaeleza kiini cha tatizo kubwa linalolikabili taifa letu kwa sasa. Watu wengi wameuawa, wameteswa au kupotezwa si kwa sababu walikuwa na hatia, bali kwa sababu ya taarifa za uongo, majungu na uzembe wa kitaaluma ndani ya mifumo ya usalama. Wapo wanaoandika au kuwasilisha taarifa nzito na uongo za kiintelijensia bila uchunguzi wa kina, wakati mwingine katika mazingira yasiyoheshimu hata thamani ya uhai wa binadamu.

Mwaka 2020, nilipokuwa natoroka nchini, nilikamatwa nchini Kenya. Niliwasikia baadhi ya maafisa wa vikosi maalum Kenya, wakisema kuwa mimi na wenzangu tulikuwa tunapanga kupindua nchi. Mke wangu Neema
alisikia maneno haya ya uongo ktk masikio yake, kwa huzuni na hofu, aliniuliza !

“Godbless, ni kweli ulikuwa unataka kupindua nchi?”

Nilimtazama na kumjibu kwa utani “Labda kama nchi hiyo ni wewe, mimi naweza naweza kukupindua pindua wewe tu mpenzi. Huu ni uongo mtupu.” Usiogope uongo huu , tutashinda tena.

Andiko hili si kwa ajili ya kulalamika, bali ni wito wa kutafakari. Taifa lolote linalojengwa juu ya taarifa za uongo hujenga msingi wa damu na machozi. Ukweli, hata unapoumiza, ndiyo pekee unaoweza kuokoa maisha na kulinda heshima ya nchi.

Taarifa za majungu , uongo , umbeya na ulevi zimeumiza watu wengi sana kibiashara, kijamii , makazini na wengine wamefungwa na hata kuuwawa bila hatia yoyote.
 
Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1996 ilikuwa inawaruhusu kukusanya taarifa na kuzichakata na kutoa ushauri au mapendekezo serikalini.

Lakini Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 2023 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu kufanya Jinai ya Uaminifu ikiwemo Kuteka, kuua, kuzikwa katika makaburi ya halaiki, kutoa taarifa za uongo, majungu, kufanya uzembe kwa kutotoa taarifa za ukweli, kupora, kuiba, kutengeneza uongo uonekane ukweli, uzushi, uzandiki, unafiki, n.k.

Hivyo basi, wananchi wanapaswa walifahamu hili kabla kulalamika Kwamba wanatekwa, wanauwawa au wanapotezwa maana Sheria inaruhusu hayo kufanyika endapo Ina muelekeo wa jinai ya uaminifu katika kufanya kazi za intelijensia na counter intelligence ndani ya mipaka ya Tanzania.

Asante
 
...'Jinai ya uaminifu'... Dah!
 
...'Jinai ya uaminifu'... Dah!

Ndiyo. Sheria ya Sasa ya Mwaka 2023 inawaruhusu Wana intellijensia wote awe TISS, POLICE, UHAMIAJI, MAGEREZA n.k. wale wenye wito wa special duties kufanya jinai ya uaminifu.

Hapo awali Sheria ya Usalama wa Taifa ya Mwaka 1996 ilikuwa inawaruhusu kukusanya taarifa, kuchakata taarifa na kutoa ushauri au mapendekezo serikalini. Ilikuwa inawakataza intelijensia wote kujihusisha na masuala ya ukamataji mwenye jukumu hilo kisheria alikuwa nalo police, lakini kwa sasa Sheria zinawaruhusu hata Taasisi zingine kufanya ukamataji kama vile TAKUKURU, UHAMIAJI, MAGEREZA, TISS, JW, MAMLAKA YA KUZUIA MADAWA YA KULEVYA, N.K.

Asante
 
Anaandika Godbless J Lema

TAARIFA ZA UONGO NA MATESO NA MAUAJI YA RAIA.

Taarifa za majungu , uongo , umbeya na ulevi zimeumiza watu wengi sana kibiashara, kijamii , makazini na wengine wamefungwa na hata kuuwawa bila hatia yoyote.
Naunga mkono hoja, kiukweli watu wake wanamdanganya sana mtu wetu, ila kudanganywa ni jambo moja, na kukubali kudanganyika ni jambo jingine.

Kuna vitu ambayo havionekani, ukidanganywa, una haki ya kudanganyika, kama baadhi ya dini na wahubiri, wanavyo wadanganya waumini wao kuwa Bwana Mungu Baba yuko kule juu Mbinguni, mawinguni, amekaa kwenye Kiti cha Enzi!, hapa ukiamini ni sawa kwa sababu you don't have any way to prove!, ukweli God is omniscient, omnipotent and omnipresent, yupo pote, Mungu wa kweli yuko ndani yako, uhai wako ndio uMungu ulio ndani yako!

Lakini ukidanganywa kwa vitu vinavyo onekana kwa macho, na bado ukauamini uongo huo, then tatizo sio anayekudanganya, tatizo ni wewe unayedanganyika.

Pili, ukidanganywa kitu usichokijua, na anayekudanganya anakudanganya kwasababu anajua wewe hujui, ikitokea mtu akakugutusha kuwa unadanganywa, akiendelea kudanganywa na kudanganyika, then ni wewe, it's you mwenyewe ndio umekubali kudanganywa na kudanganyika!

Uongo kuhusu uhaini, watu wake wamemdanganya, kuwa kuna watu wamepanga uhaini wa kumpindua, watu hao lazima washughulikiwe kikamilifu!

Wakatokea wasamaria wema wakamshtua kuwa unadanganywa, Thread 'Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!' Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!

Bado alidanganyika na kuidhinisha kilichofuatia uongo huo! .

Tundu Lissu aliposema "tutakinukisha hadi uchaguzi mkuu hautafanyika", watu wake wakamdanya kauli hiyo ni ya kihaini treasonous, kiukweli kauli hiyo sio uhaini, it's just sedition, wasamaria wema wakamshauri, Thread 'Wazalendo Wapenda Haki, Msiwe na Wasiwasi, Uhaini ni Matendo na Mipango Mkakati wa Kuutenda, Sio Maneno!, Maneno ni Sedition tuu na Sio Treason!' PreGE2025 - Wazalendo Wapenda Haki, Msiwe na Wasiwasi, Uhaini ni Matendo na Mipango Mkakati wa Kuutenda, Sio Maneno!, Maneno ni Sedition tuu na Sio Treason! mtu wetu akadanyika na kuidhinisha kilichofuatia, ndio hiki sasa kinachoendelea mahakamani!.

Kubwa kuliko, ni yale maadhamano ya October 29, watu wake wamemdanganya Gen Zii wanakufata Ikulu kuja kukupindua!, akaamini, muidhinishaji wa zitumike za moto kuwadhibiti, akaidhinisha, badala ya kuzitumia to secure the state house, endapo waandamanaji wataifikia Ikulu ndipo zitumike za moto, watu wa kazi wakaingia mitaani na kuanza kuzimimina na kuua watu hovyo!

Na baada ya mauaji hayo, mkuu wao akatetea kilichotokea na nguvu ilitumika, hii maana yake, ile miili ya vile vichanga vi malaika wa Mungu, yeye hakuiona, na kama ameiona, wamemwambia ni AI, na ameamini they did the right thing!.

A Way Forward
Ni lazima aombe radhi kwa Watanzania waliouliwa kwa makosa wakati sii waandamanaji!, vinginevyo karma ipo, it's real na haina mswalie Mtume!
Thread 'Karma is Real na ipo Kweli. Everything Happens for a Reason. Wasaidizi wa Rais Samia mna wajibu wa kumsaidia Rais na Serikali yake Kuepuka Bad Karma!' Karma is Real na ipo Kweli. Everything Happens for a Reason. Wasaidizi wa Rais Samia mna wajibu wa kumsaidia Rais na Serikali yake Kuepuka Bad Karma!

Thread 'The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!' The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!

P
 
Andko ni zuri; limepangiliwa vyema na kueleweka; lakini siyo kamilifu. limegusa tu sehemu moja, tena ndogo sana ya matatizo yanayolikabili taifa letu. Tatizo la ulaghai na uongo; ambalo Lema kalielekeza kwa hicho chombo alicho kitaja. Hili siyo tatizo la hao wanausalama pekee.
Bila shaka itakuwa sahihi kusema kuwa tatizo limeenea hadi huko likianzia kwa viongozi wakuu wa nchi wenyewe

hicho chombo cha usalama kimeundwa hivyo; kusema uongo; kwa sababu wakuu wao na wateuzi wao, hiyo ndiyo sifa wanayoitaka kwenye chombo hicho, kukidhi matakwa yao ya kuvuruga akili za wananchi.

Lema hajasema kama alipata mrejesho wowote kutoka kwa Pinda baada ya mazungumzo yao huko ofisini kwa Pinda na kuahidi angetembelea Arusha. Nachelea kusema, kuwa Lema hakuona sababu ya kueleza kilicho fuata baada ya ahadi hiyo; kwa sababu hapakuwa na lolote la maana lililofanyika, hata baada ya pinda kuambiwa ukweli.

Nchi yetu imefika kwenye hatua mbaya sana. Matatizo yetu sasa siyo ya uongo na ulaghai tu tena; bali sasa tumefika kwenye wenye mitutu kunyamzisha wasiokuwa na mitutu.

Hakuna binaadam anayeweza kuzoea kutishiwa uhai na yeye akabaki tu akiweweseka bila ya kutafuta njia za kulinda uhai wake.

Samia na Genge lake linatupeleka kwenye hatua ambayo hawa wanaowindwa na wao walazimike kutafuta njia za kujikinga uhai wao usichukuliwe kama mifugo tu..

Samia na wenzake wanaamini wanayo majeshi ya kuwalinda wao, huku wakiendelea kuua waTanzania wasiokubaliana nao; lakini asisahau kuwa, jeshi siyo swala la kushika bunduki tu na kufuata amri pekee.

Kuna jeshi kubwa zaidi la mamilioni ya waTanzania ambalo hataweza kupanbana nalo na kubaki madarakani kwa nguvu.. uongo na ulaghai una mwisho wake.
 
Anaandika Godbless J Lema

TAARIFA ZA UONGO NA MATESO NA MAUAJI YA RAIA.

Mwaka 2011, jijini Arusha, kulitokea sakata zito la mauaji yaliyosababishwa na Polisi kufuatia maandamano ya wananchi waliopinga uchaguzi Meya feki wa Arusha Mjini. Tukio hilo liliacha majeraha makubwa katika mioyo ya wananchi na maswali mazito kuhusu matumizi ya nguvu za dola dhidi ya raia wasio na hatia.

Katika mazingira hayo, Waziri Mkuu wa wakati huo, Mizengo Pinda, aliwasilisha taarifa Bungeni ambayo haikuwakilisha ukweli kamili wa kilichotokea Arusha. Nilihisi dhamira yangu ya uongozi na uwakilishi wa wananchi inanitaka nisikae kimya. Nilisimama hadharani na kusema wazi kuwa taarifa hiyo ilikuwa ya uongo.

Nilimwambia Waziri Mkuu kuwa alidanganya Bunge, na kwamba uongo aliousema angeweza hata kumfundisha shetani mbinu za uongo. Nilisisitiza kuwa nilikuwa na ushahidi wa kuthibitisha nilichokisema. Spika wa Bunge, alinipa siku saba kuwasilisha ushahidi huo, la sivyo ningechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge.

Nilimjibu Spika kuwa sikuhitaji siku saba. Nilihitaji muda mfupi tu kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kwenda hotelini na kuleta ushahidi mara moja. Ilikuwa hali ngumu na yenye mvutano mkubwa wa kisiasa, lakini nilikuwa tayari kubeba gharama ya kusimama upande wa ukweli.

Baada ya Bunge kuahirishwa mchana, Waziri Mkuu alituma wasaidizi wake wanitafute, akitaka nionane naye ofisini kwake. Niliitikia wito huo. Tulipobaki wawili, aliniambia kwa sauti ya utulivu lakini yenye uzito, “ Lema, umeniita muongo hadharani kwa sauti kali sana. Unadhani uongo wangu ulikuwa upi? Tafadhali nieleze.”

Nilimweleza kwa kina kila nilichokijua kuhusu sakata la Arusha, alisikiliza kwa makini, akashika kichwa kwa mshangao, kisha akasema kwa unyenyekevu mkubwa

“Sasa nimekuelewa. Hatuhitaji kuendelea kulumbana ndani ya Bunge. Wewe potezea, nami nitamjulisha Spika asikufuatilie suala la ushahidi. Nitakuja Arusha kushughulikia jambo hili kwa kina zaidi. Kisha akatoa kauli ambayo hadi leo naona ina uzito mkubwa kwa mustakabali wa nchi yetu:

Lema, alisema , tatizo letu kubwa sasa liko kwenye recruitment ya vijana wanaoingia kwenye vyombo vya usalama. Kazi ya intelijensia ni kusema ukweli ulivyo, ili viongozi wapate mwelekeo sahihi wa kutawala. Kwa sasa tuna changamoto kubwa ya aina ya watu tunaowaajiri. Kuna kazi kubwa sana ya kufanya.”

Maneno haya yanaeleza kiini cha tatizo kubwa linalolikabili taifa letu kwa sasa. Watu wengi wameuawa, wameteswa au kupotezwa si kwa sababu walikuwa na hatia, bali kwa sababu ya taarifa za uongo, majungu na uzembe wa kitaaluma ndani ya mifumo ya usalama. Wapo wanaoandika au kuwasilisha taarifa nzito na uongo za kiintelijensia bila uchunguzi wa kina, wakati mwingine katika mazingira yasiyoheshimu hata thamani ya uhai wa binadamu.

Mwaka 2020, nilipokuwa natoroka nchini, nilikamatwa nchini Kenya. Niliwasikia baadhi ya maafisa wa vikosi maalum Kenya, wakisema kuwa mimi na wenzangu tulikuwa tunapanga kupindua nchi. Mke wangu Neema
alisikia maneno haya ya uongo ktk masikio yake, kwa huzuni na hofu, aliniuliza !

“Godbless, ni kweli ulikuwa unataka kupindua nchi?”

Nilimtazama na kumjibu kwa utani “Labda kama nchi hiyo ni wewe, mimi naweza naweza kukupindua pindua wewe tu mpenzi. Huu ni uongo mtupu.” Usiogope uongo huu , tutashinda tena.

Andiko hili si kwa ajili ya kulalamika, bali ni wito wa kutafakari. Taifa lolote linalojengwa juu ya taarifa za uongo hujenga msingi wa damu na machozi. Ukweli, hata unapoumiza, ndiyo pekee unaoweza kuokoa maisha na kulinda heshima ya nchi.

Taarifa za majungu , uongo , umbeya na ulevi zimeumiza watu wengi sana kibiashara, kijamii , makazini na wengine wamefungwa na hata kuuwawa bila hatia yoyote.
1766440212718.jpg
 
Kwa sasa uovu imekuwa ndio nguzo ya serekali kutawala. Na haya ni matokeo ya chama kukaa madarakani muda mrefu huku umma ukiwa umekichoka. Na uovu huu utaendelea hadi ufanyike uasi mkubwa japo utamwaga damu sana, lakini ndio pekee utakomboa taifa hili.

Ertugrul Bey HAYA LAND HOV
Safari hii kuna 'elements' mpya kaziingiza Samia na kuzifanya zionekana kuwa na nguvu zaidi ya hicho chama chakavu.

'Element' ya nguvu ya kizanzibari imepamba moto sana chini ya Samia Zanzibar imejitokeza na kuwa na nguvu sana katika utawala huu. Siasa zile zile za huko visiwani zimeingizwa na kuwa mbele hadi huku Tanganyika, na Tanganyika haina jibu. Akina Kombo wanapigana kufa kupona Zanzibar iendelee kutawala.

'Element' za kibiashara; hadi kuwafanya watu kuwa bidhaa tu inayonunuliwa ili ikidhi mahitaji ya mnunuzi. Watazame akina Kabutu Kalamaganda, Nchemba Madilu, mvaa maskafu; vinyago kama akina gerson Msigwa; wote hadi wazee kama Butiku, hao ni bidhaa tu inayonunulika kwa pesa ili kukidhi mahitaji ya mnunuzi. Wateule wote wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama; aidha ni bidjhaa; au ni wahusika na 'element' ya Uzanzibar au Udini.

'Element' ya UDINI. BAKWATA na Mashekh wao wanawaona TEC na wengine kuwa ndio maadui, wasiomtaka Samia kwa sababu ya uislam wake. hawa hawaangalii uongozi wake bali dini yake tu basi..

ukiniuliza mimi mchango wa CCM ni upi katika yote haya, nitashindwa kujibu; kwa sababu siioni CCM tena siku nyingi kidogo, hata kwenye enzi za Magufuli. Chama kimekuwa ni kasha tu la kutumiwa na yeyote aliyepo madarakani.
 
Exactly.
 
Anaandika Godbless J Lema

TAARIFA ZA UONGO NA MATESO NA MAUAJI YA RAIA.

Mwaka 2011, jijini Arusha, kulitokea sakata zito la mauaji yaliyosababishwa na Polisi kufuatia maandamano ya wananchi waliopinga uchaguzi Meya feki wa Arusha Mjini. Tukio hilo liliacha majeraha makubwa katika mioyo ya wananchi na maswali mazito kuhusu matumizi ya nguvu za dola dhidi ya raia wasio na hatia.

Katika mazingira hayo, Waziri Mkuu wa wakati huo, Mizengo Pinda, aliwasilisha taarifa Bungeni ambayo haikuwakilisha ukweli kamili wa kilichotokea Arusha. Nilihisi dhamira yangu ya uongozi na uwakilishi wa wananchi inanitaka nisikae kimya. Nilisimama hadharani na kusema wazi kuwa taarifa hiyo ilikuwa ya uongo.

Nilimwambia Waziri Mkuu kuwa alidanganya Bunge, na kwamba uongo aliousema angeweza hata kumfundisha shetani mbinu za uongo. Nilisisitiza kuwa nilikuwa na ushahidi wa kuthibitisha nilichokisema. Spika wa Bunge, alinipa siku saba kuwasilisha ushahidi huo, la sivyo ningechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge.

Nilimjibu Spika kuwa sikuhitaji siku saba. Nilihitaji muda mfupi tu kutoka nje ya ukumbi wa Bunge, kwenda hotelini na kuleta ushahidi mara moja. Ilikuwa hali ngumu na yenye mvutano mkubwa wa kisiasa, lakini nilikuwa tayari kubeba gharama ya kusimama upande wa ukweli.

Baada ya Bunge kuahirishwa mchana, Waziri Mkuu alituma wasaidizi wake wanitafute, akitaka nionane naye ofisini kwake. Niliitikia wito huo. Tulipobaki wawili, aliniambia kwa sauti ya utulivu lakini yenye uzito, “ Lema, umeniita muongo hadharani kwa sauti kali sana. Unadhani uongo wangu ulikuwa upi? Tafadhali nieleze.”

Nilimweleza kwa kina kila nilichokijua kuhusu sakata la Arusha, alisikiliza kwa makini, akashika kichwa kwa mshangao, kisha akasema kwa unyenyekevu mkubwa

“Sasa nimekuelewa. Hatuhitaji kuendelea kulumbana ndani ya Bunge. Wewe potezea, nami nitamjulisha Spika asikufuatilie suala la ushahidi. Nitakuja Arusha kushughulikia jambo hili kwa kina zaidi. Kisha akatoa kauli ambayo hadi leo naona ina uzito mkubwa kwa mustakabali wa nchi yetu:

Lema, alisema , tatizo letu kubwa sasa liko kwenye recruitment ya vijana wanaoingia kwenye vyombo vya usalama. Kazi ya intelijensia ni kusema ukweli ulivyo, ili viongozi wapate mwelekeo sahihi wa kutawala. Kwa sasa tuna changamoto kubwa ya aina ya watu tunaowaajiri. Kuna kazi kubwa sana ya kufanya.”

Maneno haya yanaeleza kiini cha tatizo kubwa linalolikabili taifa letu kwa sasa. Watu wengi wameuawa, wameteswa au kupotezwa si kwa sababu walikuwa na hatia, bali kwa sababu ya taarifa za uongo, majungu na uzembe wa kitaaluma ndani ya mifumo ya usalama. Wapo wanaoandika au kuwasilisha taarifa nzito na uongo za kiintelijensia bila uchunguzi wa kina, wakati mwingine katika mazingira yasiyoheshimu hata thamani ya uhai wa binadamu.

Mwaka 2020, nilipokuwa natoroka nchini, nilikamatwa nchini Kenya. Niliwasikia baadhi ya maafisa wa vikosi maalum Kenya, wakisema kuwa mimi na wenzangu tulikuwa tunapanga kupindua nchi. Mke wangu Neema
alisikia maneno haya ya uongo ktk masikio yake, kwa huzuni na hofu, aliniuliza !

“Godbless, ni kweli ulikuwa unataka kupindua nchi?”

Nilimtazama na kumjibu kwa utani “Labda kama nchi hiyo ni wewe, mimi naweza naweza kukupindua pindua wewe tu mpenzi. Huu ni uongo mtupu.” Usiogope uongo huu , tutashinda tena.

Andiko hili si kwa ajili ya kulalamika, bali ni wito wa kutafakari. Taifa lolote linalojengwa juu ya taarifa za uongo hujenga msingi wa damu na machozi. Ukweli, hata unapoumiza, ndiyo pekee unaoweza kuokoa maisha na kulinda heshima ya nchi.

Taarifa za majungu , uongo , umbeya na ulevi zimeumiza watu wengi sana kibiashara, kijamii , makazini na wengine wamefungwa na hata kuuwawa bila hatia yoyote.
Kwa maongezi ya Pinda Na Lema Ni wazi Pinda alikuwa Na akili nyingi kuliko Lema🤣🤣🤣,alinunua utashi wa Lema Kwa hisia Na kuonesha uchache wa info
 
Game of comparison never end.
Aya wewe na andazi kipi kina akili?

Tupe majibu
 
Moja ya maelezo bora kabisa ya kufungia mwaka.

Swali ni kwanini wahusika serikalini wanajua matatizo lakini hawataki kuyarekebisha shida ni matumbo yao au dhamira.
 
Naunga mkono hoja, kiukweli watu wake wanamdanganya sana mtu wetu, ila kudanganywa ni jambo moja, na kukubali kudanganyika ni jambo jingine.

Kuna vitu ambayo havionekani, ukidanganywa, una haki ya kudanganyika, kama baadhi ya dini na wahubiri, wanavyo wadanganya waumini wao kuwa Bwana Mungu Baba yuko kule juu Mbinguni, mawinguni, amekaa kwenye Kiti cha Enzi!, hapa ukiamini ni sawa kwa sababu you don't have any way to prove!, ukweli God is omniscient, omnipotent and omnipresent, yupo pote, Mungu wa kweli yuko ndani yako, uhai wako ndio uMungu ulio ndani yako!

Lakini ukidanganywa kwa vitu vinavyo onekana kwa macho, na bado ukauamini uongo huo, then tatizo sio anayekudanganya, tatizo ni wewe unayedanganyika.

Pili, ukidanganywa kitu usichokijua, na anayekudanganya anakudanganya kwasababu anajua wewe hujui, ikitokea mtu akakugutusha kuwa unadanganywa, akiendelea kudanganywa na kudanganyika, then ni wewe, it's you mwenyewe ndio umekubali kudanganywa na kudanganyika!

Uongo kuhusu uhaini, watu wake wamemdanganya, kuwa kuna watu wamepanga uhaini wa kumpindua, watu hao lazima washughulikiwe kikamilifu!

Wakatokea wasamaria wema wakamshtua kuwa unadanganywa, Thread 'Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!' Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies!

Bado alidanganyika na kuidhinisha kilichofuatia uongo huo! .

Tundu Lissu aliposema "tutakinukisha hadi uchaguzi mkuu hautafanyika", watu wake wakamdanya kauli hiyo ni ya kihaini treasonous, kiukweli kauli hiyo sio uhaini, it's just sedition, wasamaria wema wakamshauri, Thread 'Wazalendo Wapenda Haki, Msiwe na Wasiwasi, Uhaini ni Matendo na Mipango Mkakati wa Kuutenda, Sio Maneno!, Maneno ni Sedition tuu na Sio Treason!' PreGE2025 - Wazalendo Wapenda Haki, Msiwe na Wasiwasi, Uhaini ni Matendo na Mipango Mkakati wa Kuutenda, Sio Maneno!, Maneno ni Sedition tuu na Sio Treason! mtu wetu akadanyika na kuidhinisha kilichofuatia, ndio hiki sasa kinachoendelea mahakamani!.

Kubwa kuliko, ni yale maadhamano ya October 29, watu wake wamemdanganya Gen Zii wanakufata Ikulu kuja kukupindua!, akaamini, muidhinishaji wa zitumike za moto kuwadhibiti, akaidhinisha, badala ya kuzitumia to secure the state house, endapo waandamanaji wataifikia Ikulu ndipo zitumike za moto, watu wa kazi wakaingia mitaani na kuanza kuzimimina na kuua watu hovyo!

Na baada ya mauaji hayo, mkuu wao akatetea kilichotokea na nguvu ilitumika, hii maana yake, ile miili ya vile vichanga vi malaika wa Mungu, yeye hakuiona, na kama ameiona, wamemwambia ni AI, na ameamini they did the right thing!.

A Way Forward
Ni lazima aombe radhi kwa Watanzania waliouliwa kwa makosa wakati sii waandamanaji!, vinginevyo karma ipo, it's real na haina mswalie Mtume!
Thread 'Karma is Real na ipo Kweli. Everything Happens for a Reason. Wasaidizi wa Rais Samia mna wajibu wa kumsaidia Rais na Serikali yake Kuepuka Bad Karma!' Karma is Real na ipo Kweli. Everything Happens for a Reason. Wasaidizi wa Rais Samia mna wajibu wa kumsaidia Rais na Serikali yake Kuepuka Bad Karma!

Thread 'The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!' The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!

P
Pascal Mayalla umeandika vema sana! Noel Njema
 
“Sasa nimekuelewa. Hatuhitaji kuendelea kulumbana ndani ya Bunge. Wewe potezea, nami nitamjulisha Spika asikufuatilie suala la ushahidi. Nitakuja Arusha kushughulikia jambo hili kwa kina zaidi. Kisha akatoa kauli ambayo hadi leo naona ina uzito mkubwa kwa mustakabali wa nchi yetu:
Ukisoma maelezo haya utagundua Pinda si kwamba alikuwa hajui ukweli,alikuwa anaujua, ilaa Kwa Mujibu wa mfumo wa Chama Na nafasi yake hakuweza kusimamia ukweli, Na alipoona Lema anajua ,maelezo aliyompatia yanaweza yakawa summarised Kwa usemi Huu " bwa Lema funika kombe mwanahalamu apite"

Kwa Ufupi dingi alizungumza Na Lema kama jasusi ,Ila Lema alizungumza Na dingi kama kiongozi, (Lema alishindwa kumsoma dingi)
 
Game of comparison never end.
Aya wewe na andazi kipi kina akili?

Tupe majibu
Huwezi kunielewa coz umetanguliza mahaba umeacha kutumia akili, ukipenda sana akili huwa zinaenda likizo kinachobaki ni hisia, Sasa hivi umevurugwa Na mahaba Kwa Lema ,Na you are no longer analytical,

Pinda Na Lema hawapo kwenye hisia zangu hivo Nina uwezo mzuri wa kuwachambua
 
Kazi ya intelijensia ni kusema ukweli ulivyo, ili viongozi wapate mwelekeo sahihi wa kutawala. Kwa sasa tuna changamoto kubwa ya aina ya watu tunaowaajiri. Kuna kazi kubwa sana ya kufanya.”
Mambo mazito haya
 
Back
Top Bottom