Serikali yatoa vigezo vya kupandisha vyeo na mishahara watumishi wa umma

Wanatafuta namna ya kukimbia jukumu.
Term hii sheria na kanuni zimekanyagwa na bahati mbaya wenye nafasi ya kuwapazia sauti nao wapo chini ya uvungu
Serikalini bora kutumia utaratibu huo huo wa miaka mitatu mitatu vingnevyo kutakuwa na bias maana maeneo mebgi hasa Halmashauri wazugaji wengi hivyo utashitukia kuna watakaopandishwa mshahara sio walengwa...vinginevyo wawe wanapandisha kwa kuangalia inflation (yaani wawe wanafanya inflation adjustment kila baada ya miezi 6 au mwaka)
 
Hakuna jipya alilolisema! Hakuna aliyedai mlevi apandishwe daraja! Akae kimya kama hana cha kusema! Kwa taarifa hiyo atadai alikuwa kazini akitekeleza majumu yake! Kuna tija gani kwa taarifa hiyo? Je kuna afisa utumishi yeyote ameelimishwa kitu alichokuwa hakijui? Anasakama waalimu eti wanafelisha, yeye kwa taarifa hiyo amefaulisha nini? Ameongeza tija ipi? Kama hawaongezi mishahara waache! Tena waalimu ndio awaache kabisa! asiwachokoze akaishia kutuletea matatizo kwa watoto wetu! Yeye kama anashiba na watoto wake Mungu ambariki! Mungu atawatetea waalimu kwa namna nyingine! Chonde chonde waalimu watu wengine si riziki! Ni wa kuwasamehe bure! Wakishiba wanajikuta wanamkufuru Mungu na kuwakashifu wengine! Yeye anajua mazingira wanayofanyia kazi waalimu? Kuna mpaka shule nzima yenye Mwalimu mmoja au wawili kwa wanafunzi zaidi ya mia sita! Sina hakika kama anajua kuna shule hazina kabisa waalimu, mpaka zinalazimika kufungwa! Sijui amekula maharage ya wapi huyu!

The reality is "We are not equal".
 
Kwa nini kama mnao ushahidi wa wazi kuwa mtumishi ni mzembe,mlevi na asiye na maadili msimfukuze kazi tu kuliko kumnyanyasa kwa kumnyima nyongeza ya mshahara?Hao wanaopandisha watu mishahara wakimuonea mtu ni hatua zipi zitachukuliwa?Mtazuiaje rushwa ya ngono ambayo imetumika sana kupandisha watoto wa kike warembo kazini?
 
Dalili za wenye KADI kuula zinaanza kuonekana, hongereni sana wafanyakazi watiifu hasa kwenye hili la uchumi wetu kupanda, yaani wote mliosema umepanda mtapandishwa madaraja tunachowaomba endeleeni kusema hivyo.....namalizia na HAPA KAZI TU.
 
Opras zitajazwa lkn hola.
Na hapo atasema hadi uhakiki.
Muda unaenda mwakani hiyooooooo imefika. Vigezo kibao....Mara paaaah! 2020 imefika
 
Na ndio kazi zitadorora ofisini..takwimu za uwajibikaji zitakuwa Nzuri sana ,,ila za kupika .tumechoka kuwekewa visababuuuu
 
Nami naomba kuuliza Mkuu
hivi Mtumishi akiajiriwa kwa mara ya Kwanza anapanda cheo/miaka 3 inaanza kuhesabika kuanzia lini? yaani je ule mwaka wa Probation 1year unahesabika au unautoa? say Mtumishi kaajiriwa mwaka 2015,je mwaka gani mtumishi huyu atapanda daraja?
Cc:
Alwatan
Kuna kitu kinaitwa mkataba wa kaz unaanza kuhesabu muda wa kuanza kazi mara tu unapojaza huu mkataba kwa mfano mkataba umejaza 03/03/2017 mpaka kufika 03/03/2018 teyar Mwaka ivyo ili uwepo kazini miaka mitatu utaanza 03/03/2017-03/03/2020 ila mshahara wa daraja lipya utaanza kulipwa ktk Mwaka mpya wa serikali ambao utakuwa mwezi wa 7 mwaka 2020.
 
Divine and lule
Nikubaki kumuhisi mwenzio kaongezwa msahala kumbe wote tuko sawa hakuna aliyeongeswa.
Kila MTU kivyake vyake
Msisahau kujiajili huku mkisubiri nyongeza ya mshahara.
Mshahara + ujasiliamali = √

No.Ngapi hiyo !!!!!!
 
Kuna kitu kinaitwa mkataba wa kaz unaanza kuhesabu muda wa kuanza kazi mara tu unapojaza huu mkataba kwa mfano mkataba umejaza 03/03/2017 mpaka kufika 03/03/2018 teyar Mwaka ivyo ili uwepo kazini miaka mitatu utaanza 03/03/2017-03/03/2020 ila mshahara wa daraja lipya utaanza kulipwa ktk Mwaka mpya wa serikali ambao utakuwa mwezi wa 7 mwaka 2020.
Basi kuna Rafiki yangu yupo serikalini aliajiriwa 2015 na Taasisi fulani serikalini akaambiwa daraja atapanda 2019 kwasabbu mwaka mmoja ni wa Probation Duu Aiseee...
 
Basi kuna Rafiki yangu yupo serikalini aliajiriwa 2015 na Taasisi fulani serikalini akaambiwa daraja atapanda 2019 kwasabbu mwaka mmoja ni wa Probation Duu Aiseee...
Ilo zengwe sasa ila mm nilianza 2013 na 2016 niliwekwa ktk mpango wa kupanda daraja.
 
Back
Top Bottom