Serikali yatoa vigezo vya kupandisha vyeo na mishahara watumishi wa umma

Kwa ivi vigezo ni vipya yeye na sisi wote tufunge midomo tumuache dereva wa lori atie gia tu hana uwezo wala mamlaka ya kuamua jambo ambalo kalizungumza tena namkumbusha hicho kiherehere chake atajikuta watoto wanashindwa kwenda chooni
 
Atapanda kwa kuwajibika mkuu haya nfan ya mwaka mmoja tu.au hujamsikia Katibu mkuu wa wizara
Najua hilo ...nasemea baada ya kuwajibika nilichokuwa nauliza kama amewajibika ipasavyo ni miaka mingapi Initially kwa anaeanza? 3/4?
 
Duu makubwa hayo, Mimi ninachofahamu zipo form wanazojaza watumishi zinaitwa opras ndizo zinazotumika ktk kupanda vyeo na mengineyo
Hizo fomu hazitumiki tena ila kila siku tunatafuta vigezo vipya na sana tumefika hapa:
"Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ndumbaro, suala la upandishwaji vyeo kwa watumishi wa umma litazingatia zaidi utendaji kazi wa mtumishi husika na si suala la sifa ya Muundo wa Utumishi (Scheme of Service) pekee kwa maana ya muda wa kutumikia miaka mitatu mitatu kama wengi wanavyodhani." Ina maana afisa utumishi akikupakazia kwamba wewe ni "mlevi" wa ...... umekwisha. Hakufafanua aina ya ulevi na kama tujuavyo ulevi upo wa aina nyingi, hata kupiga kazi kwa nidhamu ni ulevi. Ngoja maafisa utumishi waanze kuamkiwa na kupigiwa magoti kila asubuhi, ukiacha kumsalimu au kumpigia magoti umekwisha, utasooota kwenye cheo mpaka ukome!
 
Tuliambiwa mishahara ya November itakuwa mipya, sasa wanakuja na hizi habari ili watuambie kwamba bado wanafanya assessment ya walevi na wavivu, hili nalo litachukua mwaka mzima.
Hakuna jipya alilolisema! Hakuna aliyedai mlevi apandishwe daraja! Akae kimya kama hana cha kusema! Kwa taarifa hiyo atadai alikuwa kazini akitekeleza majumu yake! Kuna tija gani kwa taarifa hiyo? Je kuna afisa utumishi yeyote ameelimishwa kitu alichokuwa hakijui? Anasakama waalimu eti wanafelisha, yeye kwa taarifa hiyo amefaulisha nini? Ameongeza tija ipi? Kama hawaongezi mishahara waache! Tena waalimu ndio awaache kabisa! asiwachokoze akaishia kutuletea matatizo kwa watoto wetu! Yeye kama anashiba na watoto wake Mungu ambariki! Mungu atawatetea waalimu kwa namna nyingine! Chonde chonde waalimu watu wengine si riziki! Ni wa kuwasamehe bure! Wakishiba wanajikuta wanamkufuru Mungu na kuwakashifu wengine! Yeye anajua mazingira wanayofanyia kazi waalimu? Kuna mpaka shule nzima yenye Mwalimu mmoja au wawili kwa wanafunzi zaidi ya mia sita! Sina hakika kama anajua kuna shule hazina kabisa waalimu, mpaka zinalazimika kufungwa! Sijui amekula maharage ya wapi huyu!
 
tabu inaanza mizengwe pesa ya serikali tugawieni wengine mwaka mzima hatupati hata posho moja, tegemeo letu liko kwenye nyongeza. Utovu wa nidhamu, ulevi tunaadhibiwa kwa kunyimwa safari na kazi zenye posho, tafadhali dk usikaze sana
 
Daah kwa mara ya kwnza nikiwa mtumish wa umma nafikiri kuacha kazi mana hali ni mbaya huko tuendako.
 
Ndiyo hivo tena, mazingira yasha andaliwa kuwaacha wengine nje ya promotion!, amini nawaambieni kwa vigezo hivyo (ambavyo ni vya zamani pia) watakao panda hawatazidi elfu 50. Watakao lalamika baada kuachwa nje watawekwa kwa kundi la wazembe,wavivu,............
 
Nilishakusamehe hata kabla hujasema....
Kwasababu my Greatest strenghts yangu ni kusamehe....hata kama ukizidi kuutesa moyo wangu mi nasamehe 7*70 kwasababu najua ipo siku na wewe utanisamehe....
Asante na barikiwa mnoo
 
Ni vizuri vigezo vikazingatiwa. Maana unakuta mwalimu wa sayansi ana vipindi zaidi ya 30 na anafaulisha vizuri, lakini wale wa sanaa vipindi chini ya 6 na anafelisha. Huo mpango mzuri utawawajibisha walimu wabangaizaji. Wapo wengi!
 
Back
Top Bottom