Serikali yatoa siku 90 vifungashio vya plastiki visivyo na kibali cha TBS viondolewe sokoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Wazalishaji na wasambazaji wa vifungshio wamepewa miezi mitatu kuondoa sokoni bidhaa hizo zisizokidhi vigezo vinginevyo wajiandae kukutana na mkono wa sheria.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu ametoa agizo hilo leo Januari 8 alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

Ummy amesema kumeibuka wimbi la mifuko ya plastiki kwa kisingizio cha vifungashio wakati vingi havikidhi vigezo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Waziri amesema licha ya kutambua kuwa mazingira yanaathiriwa, lakini ameona awape muda huo waliokuwa na mzigo mkubwa wawe wamemaliza ili kuepuka hasara.

"Baada ya hapo, sitakuwa na msamaha na mtu maana nimetoa nafasi hiyo kwa kuzingatia serikali yetu inajali wanyonge tusingependa wapate hasara," amesema Mwalimu.

Amewataka watengenezaji wa mifuko kupata vibali kutoka Shirika la viwango Tanzania (TBS) ambao wanamamlaka ya kutoa vibali vya viwango.

Kwa mujibu wa Waziri, serikali haitawavumilia wazalishaji, wasambazaji na watumiaji ambao watakutwa baada ya hapo wakiwa na mifuko ambayo haina nembo ya TBS.
 
Back
Top Bottom