Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,681
- 46,360
Mnaondaa bajeti ya serikali tazameni uchafuzi wa mazingira kama chanzo muhimu cha mapato kwa mwaka unaokuja wa fedha . Anzisheni tozo ya mazingira kwa wazalishaji bidhaa zinazofungashwa kwenye chupa na mifuko ya plastic. Mtapa pesa nyingi sana kwa mfano mkitoza shilingi 100 ya mazingira kwa kila chupa ya plastic kutoka kampuni kama MeTL, Azam, Sayona n.k
Kwa tozo hii mtapata mapato ambayo yanaweza kusaidia kuboresha mazingira ya miji ya nchi hii iliyo michafu sana kwa kuzagaa chupa za plastiki za maji ya kunywa na vifungashio vingine vya plastiki kama vya mikate, sabuni, pampas n.k
Kama iliwezekana kuanzisha tozo ya mshikamano kwa raia pia inawezakana kuanzishwa tozo ya mazingira ikiwalenga wazalishaji bidhaa.