TBS yawataka wananchi kusoma taarifa zilizopo kwenye vifungashio vya bidhaa ili kuepuka madhara ya kiafya kabla ya matumizi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
20230530_072027.jpg
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wananchi kusoma taarifa zilizopo kwenye vifungashio vya bidhaa hususani za vyakula ili kuepuka madhara mbalimbali ya kiafya yanayoweza kujitokeza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29,2023 Jijijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Ukaguzi na Utekelezaji wa Sheria TBS, Bw. Moses Mbambe amesema kuna umuhimu mkubwa wananchi wakawa wanasoma taarifa kwenye vifungashio vya chakula kwani inasaidia kuelewa matumizi sahihi ya chakula kilichomo ndani ya kifungashio bila kuleta madhara.

“Wananchi wengi wamekuwa hawatengi muda wa kusoma zile taarifa zilizopo kwenye vifungashio, tumekuwa tukipokea malalamiko ya wateja, amenunua chakula fulani baada ya kukitumia akajikuta amepata madhara ya kiafya lakini aliposoma taarifa zile za kifungashio anakuta chakula kilikuwa kimekwisha muda wake wa matumizi”. Amesema

Pamoja na hayo amesema suala la uwekaji wa taarifa za lebo kwenye vifungashio ni suala muhimu na vilevile ni suala la kisheria ambalo linawataka wazalishaji wa vyakula vilivyofungashiwa kuweka taarifa zao kwenye vifungashio vyao kwa mujibu wa kiwango cha chakula husika.

Amesema kinywaji cha Energy Drink kimekuwa kikileta matatizo ya kiafya hasa ya moyo kwa wanywaji wa kinywaji hicho kwasababu ya uwepo wa kiwango kikubwa cha Caffeine ndo maana kwenye taarifa zilizopo kwenye lebo ya kifungashio cha kinywaji hicho imeelezwa kiwango cha utumiaji kwa siku na ni vyema watumiaji wakazingatia maelekezo

“Kwenye kopo moja la kinywaji hiki wakati mwingine inakuwa na caffeine isiopungua miligramu 500, ukiinywa nyingi inaweza kukuletea madhara ya kiafya kwasababu unakunywa kinywaji kingi kuliko kile ambacho kimewekwa kikomo kwa siku”. Ameeleza
 
Kwani wao kazi yao ni nini. Ana uhakika kila mtumiaji wa bidhaa anajua kusoma
 
Waache ujinga hao!!

Wanatutoa kafara KWA bidhaa sumu!!

Ina maana wameshindwa wanataka tuwasaidie kukagua viwango vya bidhaa sio!!?
 
TBS ihakikishe inatoa Pia Elimu Mashuleni ambapo wanafunzi Hadi wa kidato Cha Nne wanaweza kununua kifurushi Cha unga Cha Juice Cola na Kuilamba kavu bila Kuongeza Maji Huku kifurushi hiko kikiwa na Maandishi Makubwa Tuu yasemayo "USITUMIE BILA KUCHANGANYA NA MAJI"
 
Usalama wowote unaanzia na wewe

Ova
Wa barabarani kweli. Wewe kua mkweli lini umekaa unaanza kusoma viambata vya kwenye bidhaa? Mbona sigara zinatangazwa redioni na warning inatolewa hapo hapo. Kwanini na bidhaa nyingine zenye shida isiwe hivyo mpaka mtu uanze kusoma
 
Back
Top Bottom