Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Tatizo lako hutaki kuelewa! Kwahiyo unataka kusema efficiency ya bandari ya Dar ikifikia 100% ndo cargo storage haitakuwa tatizo?
Narudia, Bandari ya Dar hata ikiongeza efficiency kwa 100000000000% not mentioning hiyo 100%, watakachofanikiwa ni improvement ya logistics. Kwamba, meli ikifunga nanga, mzigo utapakuliwa na kuwa cleared on time na kwa outward cargo, nayo itakuwa hivyo hivyo! Kwamba, kazi waliyokuwa wanafanya kwa siku 5, kukiwa na efficiency itafanyika kwa dakika 5!!
Hoja hapa ni kwamba bandari ya Dar es salaam haina uwezo wa ku-handle mzigo mkubwa. Kwamba, sawa una supersonic efficiency; inward na outward cargo imeongezeka; sasa na hiyo supersonic efficiency yako itakusaidia nini wakati hauna facilities za kutosha za kuhifadhi mzigo? Ingawaje kuna ICD za watu binafsi, lakini mzigo unapofika mteja ana haki ya kuhifadhiwa mzigo wake kwa siku 7 bila kulipa chochote... kwahiyo, hata kukiwa na ICDs za watu binagsi kila mtaa, bado bandari wana wajibu wa kuhifadhi mzigo wa mteja at least kwa siku 7... kama ndani ya hizo cku 7 itabidi kupelekwa privately owned ICDs, basi wapeleke wenyewe bandari kwa gharama zao!!
Hii yote ni kwa sababu kule bandarini hakuna maghala ya kutosha ya kuhifadhia mizigo! Kwahiyo, efficiency ita-speed up logistics lakini tatizo la msingi litabaki pale pale!
Bandari ya Tanga, nimewahi kupita pale siku moja... sina hakika kama nilichokuwa nimekiona ndicho kilichopo au ile siku maji yalikupwa! Kwa macho yangu nilishuhudia tishari zinatoa mzigo melini na kuleta gatini! Kama hivyo ndo hali yenyewe, basi maanake ni kwamba kuna shallow water.... kama kuna mtu wa Tanga humu anisaidie. But all in all, hivi pale Tanga kuna bandari ya kuboresha pale kama sio kujenga upya!!
Kwamba Kenya kutaka kujenga bandari nyingine haimanishi ndo wapo sawa... hebu jiulize kidogo! Kenya ina raslimali watu na raslimali fedha! Imetumia raslimali zote mbili kufanya feasibility study na wakaona umuhimu wa kujenga bandari kubwa zaidi kutokana na projections zao!! Yaani bado unaamini wewe usiyefahamu hata wanapokea containers ngapi kwa mwezi unaweza kuwa sawa kuliko wao? Sasa wakati nyie mnadhani ndo wataalamu zaidi wa kuzifahamu white elephant projects, Wakenya na Wamarekani kwa kuwa hawana akili hawa hapa:Kwahiyo hapa Wachina hawana akili, Kenya hawana akili, US Companies nao maboya tu lakini nyinyi tena ambao hata shipping business yenyewe hamuifahamu lakini ndo mna uwezo mkubwa wa kufahamu viable and white elephant project kwenye ports investments!!!! Sasa ikiwa $ 10 Billion mnaona ni li-project likubwa kwelikweli; what abaout hao ambao target yao ni $26 Billion?
Wengine wakati wanelezea strategy za China kujitanua, wanaandika:
China’s strategy is to have key points on the Silk Road space such as Bagamoyo become the key sites for the transcontinental exchange of manufactured goods and commodities between the Asian and African economies along the Maritime Silk Road. Chinese policy-makers are convinced that the benefits of China’s infrastructure-driven development model can also be transferred to Africa. Pamoja na yote hayo, bado mnaona Wachina ni wapumbavu wa kutaka kuwekeza Bagamoyo?!
Tatizo la Watanzania, hata vitu ambavyo hatuna utaalamu navyo tunataka kuvitolea maoni na ku-criticize na tunafanya hivyo bila ku-research wala kuuliza wenye utalaamu na suala husika!!! Yaani unakuta mtu anaibuka from nowhere na kuongea bila woga kwamba pale kina kifupi... muulize kifupi futi ngapi hana jibu... kumbe alikariri Jiografia ya shule ya msingi kwamba Mtwara ndo bandari yenye kina kirefu basi ndo tayari anajiona mtalaamu wa kufahamu wapi panafaa kujengwa bandari na wapi hapafai!!!! Muulize ili kujenga bandari kina kinatakiwa kuwa futi ngapi, hana jibu lakini bado anataka kuwa-criticize watalaamu ambao wameshafanya study!
Mimi nimekwambia siwezi kuongelea mambo ya Kenya kwa maana sina uelewa sana ila kwa hapa kwetu Bandari ya Bagamoyo ni white elephant project yaani kupoteza tu fedha, fedha ambazo tungeweza kuzitumia kuboresha kwanza hizi zilizopo kabla ya kujenga Bandari mpya yaani kwanza Reli ijengwe upya ya kuunganisha Dar na Kigoma/Mwanza; Tanga- Moshi -Arusha mpaka Musoma na Mtwara corridor ambapo reli ya kutoka MT mpaka Ziwa Nyasa hivyo vifanyike kwanza, Maziwa yetu yote yapate Bandari kwanza, tayari zipo ni kukarabati tu kama vile Kigoma, Mwanza, Musoma, Bukoba na Nyasa na kama tukitumia hiyo bilioni 10 tutafanya mengi sana kwenye hilo baada ya hapo sasa baada ya kila kitu kuwa exhausted ndiyo kama kuna haja ya kujenga Bandari nyingine from scratch basi tufanye hivyo lkn siyo kinyume chake, huko ni kupoteza fedha!
Last edited: