BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
Ni uamuzi wa Serikali kupitia Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima ikiwa ni baada ya Video ya Tangazo la huduma za 'Massage' iliyowekwa Mitandaoni, kuripotiwa kuwa ina Vitendo vilivyo kinyume na maadili.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo, huduma za Kituo zimesitishwa kuanzia Oktoba 26, 2023 kutokana na kutokidhi vigezo vya Sheria Namba 23 ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, pia mmiliki ametozwa faini ya Tsh. Laki 5 pamoja na kupewa maelekezo mengine ambayo kama atayakiuka atafikishwa Mahakamani.
Pia,, Waziri Gwajima ameelekeza Mamlaka Husika kuwafuatilia Watoa Huduma wengine ili kuwabaini wasiotimiza matakwa ya Sheria na ikiwemo kuathiri Ustawi wa Jamii na kuchochea Mmomonyoko wa Maadili unaosababisha matukio ya Unyanyasaji, Udhalilishaji wa Kijinsia ambapo waaathirika wakuu ni Watoto.
Aidha, Wizara imetoa mawasiliano ya moja kwa moja kwa wanaotaka kuripoti masuala mbalimbali Wizarani watumie namba 0734 986503 na 026 2160250, matukio ya Ukatili wa Watoto namba 116 Saa 24 kila siku bila malipo. Na iwapo Waziri mwenye dhamana atahitajika, tuma ujumbe kwenye namba 0765 345777 na 0734 124191.
=============