Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

HUU USHENZI (UJAMAA) NILIWAMBIA TOKEA DECEMBER KUWA UNARUDI KWA KASI.! HAPO KIWANGO CHA AKILI KILICHOTUMIKA NI KIDOGO KULIKO CHA SISIMIZI! KAMA MAISHA YANAKUWA BORA KWA SERIKALI KUPANGA BEI HATA MTOTO MDOGO HASHINDWI KUONGOZA NCHI! SITAKI KUSIKIA YA SUMATRA NA EWURA HAPA: NAWAPINGA HATA WAO! SIUNGI MKONO MAWAZO MGANDO NA YA KIDIKTETA HAYO! JAPO HATA HIYO 1800 BADO NI KUBWA MNO. UJAMAA (USHENZI HUU) NI MFUMO WA KUJIKIMU!
 
Mkuu hiyo barua yako haijakamilika kabisa... Tunataka stamp na signature.
 
CCM wameshaifuta kwenye Katiba? Tanzania inafuata "ujamaa na kujitegemea", hiyo open market wamechomekea tu ili kuanzisha "ujasirimali" wakiwa bado IKULU.
Wadanganyika ni nani aliyewaroga?
Kushusha bei za bidhaa kwenye uchumi wa open market ni jipu.
Umesoma uchumi hata kidogo??
Unaijua kazi ya serikali kwenye open market au una payuka tu??
 
Siku chache baada ya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza zuio la uingizwaji wa bidhaa ya sukari kutoka nje ya nchi, leo March 8 2016 Serikali kupitia bodi ya sukari Tanzania, imetangaza viwango vipya vya bei ya sukari nchini vitakavyoanza kutumika hivi karibuni, akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry Semwanza amesema>>

Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja‘

‘wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi‘

‘Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo‘
View attachment 328164
Huku mbezi ya Kimara wanajifanya hawajaliona hili tangazo,, wanatupopoa hadi 2,200/= utadhani nao wana Jamhuri yao peke yao.
 
kinachosikitisha hapo ni kwamba,bei hii ni kwa tanzania nzima au ni kwa wale wanaoishi mikoa yenye viwanda vya sukari? hivi huu ukurupukaji utaisha lini?
 
Umepewa sehemu ya kupumzika unataka na Mwenye nyumba akupe MKE wake upumzike nae!!! Hivyo vifaa vya ujenzi utavitumia Kama vitafunio kwenye hiyo chai!!!??? Wabongo bwana kila kitu ujuaji....

Acha matusi kijana ............ hivi unataka watu waishi kwenye nyumba za manyasi na udongo mpaka lini!!?

Wewe sukari unaona ni kitu kikubwa mno siyo .......... kuna watu bado ni luxury kwao hata kwa hiyo 1800!!

Hili ni jukwaa la kupeana mawazo. Hakuna mahali niliposema walichokifnya ni kibaya au ni kosa .... ndiyo maana nimependekeza pia waangalie pia kwenye vifaa vya ujenzi. Pia pembejeo za kilimo zipunguziwe kodi na watoe ruzuku!!
 
Wasiishi hapo tu
Unga
Mchele
Viazi
Chai
kahawa
Vyote vyakula vinatakiwa vishuhuke baada ya bei ya mafuta kushuka gharama za usafirishaji si zimepungua???
 
Sio
Tumpe Muda Mh. JPM Mambo Yatakaa Sawa Tu Coz Kwa KipindinKifupi Tu Alichokaa Madarakani Hata Mafuta Yameshuka.

Kimsingi Huwezi Kupandisha Au Kushusha Tu Bei Ya Bidhaa Bila Kufanya Utafiti Wa Kina. Unaweza Ukashusha/Kupandisha Ukajikuta Umezidisha Kiwango Upande Mmoja Ukaumia Sana, So Ni Bora Mambo Haya Yakaenda Kwa Polepole Lakn Kwa Uhakika Ili Kuondoa Matatizo Na Malalamiko Kwa Wadau.

MAGUFULI JEMBE, WANAFIKI WANAMCHUKIA LAKIN WANAMKUBALI.
Bei imeshushwa na soko sio Rais Wangu JPM..ndio anazosifa nyingi ila tusimlimbikizie nyingine zaidi ya ukweli..hata hivyo bado bei ya mafuta iko juu mnoo kwa kulinganisha bei ya sokoni huko ughaibuni..
 
Wanavyotangaza bei ya mafuta uwa inakuaje?
Kuna watu wanashangaza sana!

Kuna wengine wanapinga utadhani price capping ndio inaanza nchini wakati EWURA kila mara wanatangaza bei elekezi za mafuta.
 
WAFUATILIWE WENGI WANAUZA 2000/- HADI 2200/-.
Mtu kanunua mfuko wa kilo 50 kwa bei ya Jumla 94000 je ye rejareja atauza shilingi ngapi ili apate faida?

Wanahangaika na Retail salers badala ya kuhangaika na whole salers
 
Haya matamko yatatuponza jamani nahisi wamekurupuka katika hili ninunue mfuko elfu 96000 halafu niuze kilo 1800 hata bei ya sasa ya 2200 ni kama msaada tu kwa raia wenzetu mfuko wa sukari ukianza kupima hizi robo mara nusu sana sana utaambulia kilo 46 mpaka mfuko unaisha na raia walivyowakali sasa anataka mzani ugote chini utadhani muuzaji anakiwanda chake home
 
Bei elekezi ya 1,800 kwa Tanzania nzima! sijui watoa bei wamepiga hesabu zao kivipi. tulishazoea wenzetu wa EWURA wakikokotoa bei hutofautiana mkoa hadi mji. Sasa hii bei ni moja tanzania nzima hapo sukari itakuwa inazalishwa kwa kila mji/mkoa au hakutakuwa na Transportation costs hapo! Sukari inazalishwa Morogoro.Kagera na Moshi sasa mimi wanisaidie,bei ya sukari mjini Morogoro itakuwa sawa na kijijini kwetu ichobela Magu? Kwa ukokotoaji upi sasa hapo? Leo hapa kwetu Mwanza mjini tunanunua 2,200. Je hao maafisa biashara wamejipanga vipi kudhibiti kufichwa kwa bidhaa hii?
 
Back
Top Bottom