Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

Kwa mtazamo wangu hili ni tangazo tu, utekelezaji ni ziro,, jana na leo asubuhi nimepita madukani kununua sukari kwa research kuona kama agizo hili linatekelezwa,, hakuna kitu sukari bado unauzwa 22000 kwa kilo na ukiuliza unaambiwa ndo amenunua kwa kuuza bei hiyo,, hebu wahusika fuatilieni
 
Tunaanza kuinusa harufu ya Tanzania yetu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki rais Dr. JPM.
 
Kwa mtazamo wangu hili ni tangazo tu, utekelezaji ni ziro,, jana na leo asubuhi nimepita madukani kununua sukari kwa research kuona kama agizo hili linatekelezwa,, hakuna kitu sukari bado unauzwa 22000 kwa kilo na ukiuliza unaambiwa ndo amenunua kwa kuuza bei hiyo,, hebu wahusika fuatilieni
Rekebisha bei yako mkuu
 
Uchumi ni sayansi ambayo unaweza fanya utabiri sio mara zote watu wanakua sawa lakini kwa hapa ata wakisema watumie nguvu kufanya implementation bei ya sukari kilo sh/1800 it wont work nationally give it three month maximum there is so much of middleman costs and current market environment ambazo serikari aijazingatia.
 
Mtu wa Kilombero, Mtibwa, Moshi - TPC na Kagera - Sugar naye atanunua kwa bei hiyohiyo wakati production imo ndani ya miji husika, nadhani bei inatakiwa kuwa reviewed kwa maeneo hayo
Uko sawa lakini kufanya bei moja kuwa uniform ni kuwa wale walioko maeneo ya viwandani walipe zaidi ili kuwawezesha walioko mbali wamudu bei hiyo. Kwa mfano tunapolipa bima ya afya watumishi wote au Sh. 10,000/= kwa mwaka, sio wote wanaolipa wataugua lakini wanawapa wepesi wanaougua. Kwa sukari ni hivyo hivyo itawapa advantage walioko mbali kununua sukari kwa bei nafuu chini ya gharama halisi mfano kutoa sukari toka Kilombero kuipeleka Tabora kiuhalisia gharama zote zikiingizwa mtu wa Tabora atastahili kuinunua kwa pengine Sh. 3500/=. Pia inasaidia kuwadhibiti walanguzi.
 
Siku chache baada ya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza zuio la uingizwaji wa bidhaa ya sukari kutoka nje ya nchi, leo March 8 2016 Serikali kupitia bodi ya sukari Tanzania, imetangaza viwango vipya vya bei ya sukari nchini vitakavyoanza kutumika hivi karibuni, akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry Semwanza amesema>>

Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja‘

‘wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi‘

‘Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo‘
View attachment 328164

Serikali na Bodi ya sukari wasitangaze maagizo kwa kukurupuka. Sisi wafanyabiashara wa rejareja tumenunua sukari kwa bei ya tzs 92,000 kwa mfuko wa kilo 50, hii ni shs 1.840 kwa kilo! Amri ya kuuza kwa tzs 1,800 itatekelewaje? Walitakiwa kwanza kuhakikisha kuwa wenye viwanda wameshusha bei ndipo watangaze bei elekezi. Mwezi Septemba, 2015 bei ya wasambazaji ilikuwa tzs 80,500 kwa mfuko wa kilo 50 yaani shs 1610 kwa kilo. Wakirudisha bei hiyo ndipo hii ya 1,800 itatekelezeka.
Pia wauzaji wa jumla waruhusiwe kuchukua sukari viwandani moja kwa moja badala ya kupitia kwa distributors ambao ni middlemen na ndiyo waagizaji wa sukari ya nje ya nchi inaua viwanda vyetu. Waziri Mwaijage kama umo humu chukua hatua,
 
12799366_1054644107933380_4004575374299277551_n.jpg

Maoni yangu serikali iwachukulie hatua kali wafanyabiashara wote wanohujumu uchumi kwa kulangua sukari, ili iwe fundisho kama ilivyokuwa kwa watorosha makontena bndarini
 
Serikali Ijikite Katika Kushusha bidhaa zinazowalenga wananchi moja kwa moja kama Unga, Mchele, Petrol na jamii zake kama Mafuta ya taa na Diesel, Dawa za Mifugo na Binadamu Sijawahi kuona mtu amekufa kwa kutokunywa Chai au kutokula Nyama.
Mkuu sukari ina matumizi mengi. Sio kwenye chai tu!Viwanda vingi vinaihitaji sukari ili kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi yetu ya kila siku.
 
Mkuu sukari ina matumizi mengi. Sio kwenye chai tu!Viwanda vingi vinaihitaji sukari ili kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi yetu ya kila siku.
Fikiri kwa Kina Kiwanda gani kitatumia Sukari Inayouzwa Tzs. 1,800 Sukari ya Viwandani ni tofauti na Ukitumia nusu kilo Inatoa Pipa la Juice wakati Sukari iliyopunguzwa bei Kilo moja haitoshi kwenye ndoo ya Lita 10. Na hii sukari ni kosa kuuza maduka ya mitaani japo nimeona akina mama wengi wanotengeneza Juice na wanaweka hiyo Sukari ni Sumu.
 
Indeed. ..wafanyabiashara sio serikali. Serikali ni kubwa kuliko individuals
 
Back
Top Bottom