Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

Kuna haja ya kufuatilia na kusimamia vzr sana maana kwel kuna maeneo wanauza zaid 1800
 
Safi sana magufuli hapa tumepata bonge la kiongozi viva jpm
Aisee..! Wewe ni kusifu kila kitu tu, wala hujipi muda wa kutafakari.

Haya jiandae kunywa chai bila sukari, au jiandae kuunga foleni kubwa ili kununua sukari, pia tegemea sukari kuuzwa kwa bei ya kulangua zaidi huko kwenye dark market.
 
Haya matamko yatatuponza jamani nahisi wamekurupuka katika hili ninunue mfuko elfu 96000 halafu niuze kilo 1800 hata bei ya sasa ya 2200 ni kama msaada tu kwa raia wenzetu mfuko wa sukari ukianza kupima hizi robo mara nusu sana sana utaambulia kilo 46 mpaka mfuko unaisha na raia walivyowakali sasa anataka mzani ugote chini utadhani muuzaji anakiwanda chake home
Naona ni vita kat ya wafanyabiashara na wateja humu ndani,...hii awamu nyingne mlipoambiwa mtaisoma namba mlifikir mchezo eeh?
 
hivi wakulima (outgrowers) wa mtibwa walipatwa na kadhia ipi? mwenye kujua pls
 
Bei ya mafuta ya mikoani ni kubwa kiasi Fulani kulinganisha na DSM kufidia gharsma za usafirishaji.
Unataka kuniambia EWURA uwa wanatoa bei za kila mkoa?
 
Tumpe Muda Mh. JPM Mambo Yatakaa Sawa Tu Coz Kwa KipindinKifupi Tu Alichokaa Madarakani Hata Mafuta Yameshuka.

Kimsingi Huwezi Kupandisha Au Kushusha Tu Bei Ya Bidhaa Bila Kufanya Utafiti Wa Kina. Unaweza Ukashusha/Kupandisha Ukajikuta Umezidisha Kiwango Upande Mmoja Ukaumia Sana, So Ni Bora Mambo Haya Yakaenda Kwa Polepole Lakn Kwa Uhakika Ili Kuondoa Matatizo Na Malalamiko Kwa Wadau.

MAGUFULI JEMBE, WANAFIKI WANAMCHUKIA LAKIN WANAMKUBALI.
Ndugu usijivue akili kwa kupongeza pasipo kutumia angalau akili yako kidogo kufikiri, hilo agizo juu ya kushusha bei ya sukari ni kiini macho kwani hapo wanazungumzia bei ya wauzaji wa rejareja huku wakishindwa au kuacha kwa makusudi kuzungumzia bei ya wauzaji wa jumla. labda nikuambie tu kwa sasa mfuko wa sukari Kg 25 unauzwa Tshs. 47,000/= - 48,000/= kutoka bei ya tshs. 44,500/= sasa huyo anayetoa agizo hilo anawafanya watanzania ni mazuzu kwani anajua wazi yeye ni mnufaika na ongezeka la hiyo bei ya jumla analeta mazingaombwe ya kutoa agizo ya kuwapangia bei wauazji wa reja reja.
 
Unataka kuniambia EWURA uwa wanatoa bei za kila mkoa?
Duh!! mbona umeuliza swali la kipuuzi kiasi hiki, yaani uwezo wako wa kufikiri umepungua kuliko kawaida kwani ni wazi haufuatilii kabisa suala zima la matangazo ya kupanda au kushuka kwa bei ya mafuta (Fuel).
 
dahh sijui katika uchumi huria jambo hili linakaaje.
endeleeni ktupapangia huku nyanya 2 mia 5, kitunguu kimoja mia 3.
 
kitakachotokea ni retail shop owners kutokuinunua hiyo bidhaa ikiwa haina tija kwao. hapo ndipo sukari itaadimika mtaani lakini viwandani imejaa.
 
Serikali Ijikite Katika Kushusha bidhaa zinazowalenga wananchi moja kwa moja kama Unga, Mchele, Petrol na jamii zake kama Mafuta ya taa na Diesel, Dawa za Mifugo na Binadamu Sijawahi kuona mtu amekufa kwa kutokunywa Chai au kutokula Nyama.
 
Haya matamko yatatuponza jamani nahisi wamekurupuka katika hili ninunue mfuko elfu 96000 halafu niuze kilo 1800 hata bei ya sasa ya 2200 ni kama msaada tu kwa raia wenzetu mfuko wa sukari ukianza kupima hizi robo mara nusu sana sana utaambulia kilo 46 mpaka mfuko unaisha na raia walivyowakali sasa anataka mzani ugote chini utadhani muuzaji anakiwanda chake home
Mkuu umeongea point sana. Wauzaj reja reja wanauza kulingana na walivyo nunua maduka ya jumla, sasa badala wawabane wauzaj wa jumla wanabana wa rejareja hiv mshaur wao ni nan? Maduka ya jumla yakishusha automatically wa reja reja lazima washushe
 
Duh!! mbona umeuliza swali la kipuuzi kiasi hiki, yaani uwezo wako wa kufikiri umepungua kuliko kawaida kwani ni wazi haufuatilii kabisa suala zima la matangazo ya kupanda au kushuka kwa bei ya mafuta (Fuel).
Wewe punguani kweli siku zote tabia za mashoga ni kurukia kila jambo swali umeulizwa wewe au unatafuta baasha kwa nguvu.
 
Bad economics ninge elewa kana kwamba wazalishaji wangefungua distribution centres zao kila mkoa kwanza na kuzifikisha sukari huko halafu wapange bei lakini muuzaji wa jumla awezi kuja kufuata sukari kagera na morogoro ambapo cost zake ni tofauti halafu aweze pewa fixed price it is just not business sense na sioni encouragement ilipo.

Hao wazalishaji wenyewe nimesikia wakidai ina gharimu karibu 1900 kuzalisha kilo serikari ilisema itachunguza ukweli wake, sasa sijui wameitimisha vipi kwa kilo ya 1800 ya reja reja? sukari inazalishwa kwa kiasi gani na faida ya muuzaji wa kati iko wapi na wa reja reja iko wapi jumlisha na VAT kama imewekewa.

Ni hivi either way kama hakuna faida ya biashara na jamaa wasipowekeza kwenye distribution centre ni sera itakayokufa yenyewe hiyo sukari itauzika mikoa inayozalishwa kama faida ni ndogo na sehemu zingine wajiandae kunywa uji wa chumvi biashara si kazi ya kanisa (kwa lugha ya mtaani kwetu kazi ya bure, maana kuna mijitu humu yakisikia maneno ya dini inakurupuka) sasa ikitokea uhaba jamaa watakwambia watu wanahodhi sukari au wanafanya hujumu ya makusudi wakati sera yenyewe aina uhalisia ya kuwapa watu morale ya kufanya biashara.

Watch this space
 
HOW ABOUT CLOSING STOCK WALIYONAYO WAFANYABIASHARA, AMBAYO BY FIFO NA AVCO IKO VALUED AT 2000/=
Hao walikua wanauza kwa ujanja wapate faida kubwa, ila walikua wananunua bei rahisi, hata wakiuza 1800 faida ipo. Hakuna excuse yeyote walizoea kutulangua
 
Jana tarehe 8 nimenunua kilo ya sukali kwa 2200/= naona hiyo elekezi ni maneno wala si implementation
 
Back
Top Bottom