Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

Price capping kwenye bidhaa zipi!!?

Kwenye open market economy sidhani kama inawezekana ukaweka same price across the whole country. Control measures unaweza kuweka kuzuia bei zisiwe beyond. Price capping kwenye services or utilities could be fine not on commodities. I am a Scientist but this one does not make sense to me!! I still stand to be corrected. I really have to check this before embarking on a serious discussion with any of you guys!! However, to me this would perhaps be a temporary measure ...... but what would be a permanent solution!!
UDBS oyeeee bishaneni tujue na sisi
 
Siyo babu yako sema ni watanzania wengi miaka ya 80 tulikunywa sana chai ya sukari guru

Hahahaaa. Nikweli kabisa ila baba yangu alikuwa na utatibu wa kutumia asali mara nyingi endapo sukari ikikosekana. Tumetoka mbali sana tunarudi hukohuko.

Haya ni madhara ya kukosa uzalendo na kuwawezesha wazawa kumiliki viwanda vingi hasa hivi vya kati na tukiwatukuza wawekezaji wa kihindi na wengine.

Wanachofanya wanavuna sana alafu pesa zetu wanakwenda kuficha kwenye mabenki yao.

Ndio maana wapo miaka mingi wanazalisha lakini maendeleo hakuna.
 
Price capping kwenye bidhaa zipi!!?

Kwenye open market economy sidhani kama inawezekana ukaweka same price across the whole country. Control measures unaweza kuweka kuzuia bei zisiwe beyond. Price capping kwenye services or utilities could be fine not on commodities. I am a Scientist but this one does not make sense to me!! I still stand to be corrected. I really have to check this before embarking on a serious discussion with any of you guys!! However, to me this would perhaps be a temporary measure ...... but what would be a permanent solution!!
Hata sasa serikali imeweka bei isiwe beyond shilingi 1800. Serikali haijakataza kama una ubavu unaweza kuuza sukari kwa shilingi 100 kwa kilo au kugawa bure.

Ninaamini hii ni temporary measure.

Permanent solution is investment on sugar production industries!

Huwezi kuwa na uzalishaji mwingi wa sukari nchini kama gharama ya uagizaji wa sukari nje ya nchi ni ndogo kuliko uzalishaji nchini.
 
Nikupe mfano rahisi bei ya soda ya chupa kiuhalisia ni sh 390 lakini wote ikiwa na mimi naenunua karibu na Duka lililopo kiwanda nauziwa mia tano! Kikokotoo

Gharama za usafiri kwa sasa ni sh 1.2 kg\km jiulize ingekuwaje bei ya soda ikiwa soda 3 za chupa zenye maji ni sawa na kilo moja ikiwa zitasafiri KM 1000? ( soda 3x390+1200 nauli) = 2370 =@1090 kwa soda, kumbe ulipaji wa uniform huchangia gharama kwa walio umbali mrefu...
Hivi tumeshaangalia ubora wa hii sukari? naona kama ina ladha ya sukari guru na nyingine ina kaharufu ka kiroba au ni mie tu naona hii hali. Na hili la bei linatia shaka, iweje mkazi wa kamachumu auziwe 1800 kwa kilo sawa na mtu wa kyela wakati yeye anaishi mita mia kutoka kiwandani? na anaweza enda nunua sukari kiwandani kwa miguu?
 
Mzalendo15 umenena vema. Ni wazi kkwamba sukari inaweza kushushwa bei mpaka hata 1500. Watakachofanya wazalishaji ni kupunguza ubora wa hiyo sikari ili wasipate hasara! Nadhni hata tukitaka sukari ya shs 1000 kwa kilo wazalishaji watatutengenezea. Ishu ni ubora!
 
leo asubuhi nimezunguka maduka manne yote bei ni 2400 sijui hiyo 1800 ni ya wapi!
 
Hizi issue mi nashangaa, hawa wafanya biashara wanapandisha vitu bei sana … sio kama bei 2400 ililekezwa na serikal au popote pale hapana ila wqfanya biashara wamekuwa wakijipandishia bei watakavyo bei ikiyotambulika ni ya 2000 ila utakuta duka hili 2400 mwingine 2200 wanafanya watakavyo
 
Mzalendo15 umenena vema. Ni wazi kkwamba sukari inaweza kushushwa bei mpaka hata 1500. Watakachofanya wazalishaji ni kupunguza ubora wa hiyo sikari ili wasipate hasara! Nadhni hata tukitaka sukari ya shs 1000 kwa kilo wazalishaji watatutengenezea. Ishu ni ubora!
kweli! wanaweza changanya hata na magunzi ili bei ipungue. hivi TDFA huwa wanakagua hii sukari?
 
Serikali leo imetangaza viwango vipya vya bei ya sukari nchini vinavyoanza kutumika kuanzia sasa. Kwa mujibu Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry Semwanza bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja

20160308_113718-1.jpg
haya ni maamuzi mazuri lakini ipo hofu moja,
Ukisoma hilo agizo limembana muuza rejareja,lakini kunaulazima pia muuza jumla nae akabanwa auze bei ambayo anaeuza rejareja nae akiuza kwa 1800 apate faida,hawa wa jumla wakiachwa bila kuwapa bei elekezi huenda kukawa na usumbufu
 
Serikali leo imetangaza viwango vipya vya bei ya sukari nchini vinavyoanza kutumika kuanzia sasa. Kwa mujibu Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry Semwanza bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja

Changa la macho kama kawaida ya Serikali ya CCM, kushusha kila sehemu iuzwe 1,800/? haiwezekani kwa sababu hamjazingatia mambo meengi katika soko letu na mazingira ya upatikanaji pamoja na gharama zake.....

Bora mkakaa kimya sababu mnatuchefua sana wananchi, acheni usanii.

20160308_113718-1.jpg
 
Je bei hiyo ni kila mkoa na mji au kwa mikoa jirani na Kilimanjaro, Morogoro na Kagera tu? Bei elekezi haijafafanua jambo hilo?
Wanavyotangaza bei ya mafuta uwa inakuaje?
 
Hizi issue mi nashangaa, hawa wafanya biashara wanapandisha vitu bei sana … sio kama bei 2400 ililekezwa na serikal au popote pale hapana ila wqfanya biashara wamekuwa wakijipandishia bei watakavyo bei ikiyotambulika ni ya 2000 ila utakuta duka hili 2400 mwingine 2200 wanafanya watakavyo
hivi bei za mafremu nani anapanga? unataka bei ya sukari mlimani city iwe sawa na manzese?
 
Kwenye open market economy huwezi kufanya hivyo. Hayo maelekezo yataleta utata ............. bei ya sukari Morogoro, Moshi au Kagera kunakozalishwa sukari haiwezekani ikawa sawa na Mtwara, Mbeya au Kigoma!! Kama ni hivyo basi itabidi serikali ifidie gharama zingine.

Washushe pia bei za vifaa vya ujenzi!!
Umepewa sehemu ya kupumzika unataka na Mwenye nyumba akupe MKE wake upumzike nae!!! Hivyo vifaa vya ujenzi utavitumia Kama vitafunio kwenye hiyo chai!!!??? Wabongo bwana kila kitu ujuaji....
 
Hivi tumeshaangalia ubora wa hii sukari? naona kama ina ladha ya sukari guru na nyingine ina kaharufu ka kiroba au ni mie tu naona hii hali. Na hili la bei linatia shaka, iweje mkazi wa kamachumu auziwe 1800 kwa kilo sawa na mtu wa kyela wakati yeye anaishi mita mia kutoka kiwandani? na anaweza enda nunua sukari kiwandani kwa miguu?

Hata mimi hii sukari ya Tanzania yenye mfuko mpya, ambao una rangi ya kijani kidogo, naona ipo tofauti radha yake siilewi kabisa, hata jirani yangu alinambia anaona haikolei kama ile ya mwanzo.
 
Hivi tumeshaangalia ubora wa hii sukari? naona kama ina ladha ya sukari guru na nyingine ina kaharufu ka kiroba au ni mie tu naona hii hali. Na hili la bei linatia shaka, iweje mkazi wa kamachumu auziwe 1800 kwa kilo sawa na mtu wa kyela wakati yeye anaishi mita mia kutoka kiwandani? na anaweza enda nunua sukari kiwandani kwa miguu?
Wabongo kwenu hakunaga jema kutwa lawama hata mlambwe makalio ....sasa ww unatakaje kwa mfano?
 
Serikali naona inaiga Venezuela, hii kitu itawacost na tunako elekea Serikali itaanza kuagiza bidhaa yenyewe time will tell na huo ndo utakuwa mwisho, Hakuna kitu kibaya sana kama kufanya kazi kutaka kuridhisha jamii kwa mazingira ambayo hayawekani
 
Kwa hiyo mmeshafanya price capping kwa bidhaa na huduma ngapi mpaka muda huu?
Na lengo lenu la kufanya price capping ni nini?
Ile price capping kwa elimu, shule mmeshaifanyia tathmini? Ilikuwa laki 3 na ushee? Tozo wanayolipa wazazi na wafadhili wao kama ada ya shule ikoje leo? Imeshuka au imeshushwa?
'Ujinga' wa Ikulu unarudi kwa kasi
Serikali yapiga ‘stop’ Shule binafsi kupandisha Ada
Serikali yapanga bei tiba hospitali binafsi
Badala ya kujikita kwenye hoja iliyoko mezani unaanza kuleta porojo za kisiasa.

Hoja iliyoko mezani ni price capping ya sukari. Kama unataka tuanze kujadili hoja ulizozileta, fungua Thread/Mada nyingine ili tuanze kujadili.
 
Back
Top Bottom