Serikali yashusha bei ya sukari mpaka Tsh 1,800/=

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,830
43,278
Siku chache baada ya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza zuio la uingizwaji wa bidhaa ya sukari kutoka nje ya nchi, leo March 8 2016 Serikali kupitia bodi ya sukari Tanzania, imetangaza viwango vipya vya bei ya sukari nchini vitakavyoanza kutumika hivi karibuni, akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya sukari Tanzania Henry Semwanza amesema>>

Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja‘

‘wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi‘

‘Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo‘
uploadfromtaptalk1457431676607.jpg
 
Hilo agizo lifanyiwe kazi na taasisi husika,utashangaa supermarkets zote dar bado zitaendelea kuuza sukari bei ya sh2000 na zaidi
 
Tumpe Muda Mh. JPM Mambo Yatakaa Sawa Tu Coz Kwa KipindinKifupi Tu Alichokaa Madarakani Hata Mafuta Yameshuka.

Kimsingi Huwezi Kupandisha Au Kushusha Tu Bei Ya Bidhaa Bila Kufanya Utafiti Wa Kina. Unaweza Ukashusha/Kupandisha Ukajikuta Umezidisha Kiwango Upande Mmoja Ukaumia Sana, So Ni Bora Mambo Haya Yakaenda Kwa Polepole Lakn Kwa Uhakika Ili Kuondoa Matatizo Na Malalamiko Kwa Wadau.

MAGUFULI JEMBE, WANAFIKI WANAMCHUKIA LAKIN WANAMKUBALI.
 
Wakumbuke lakini na kutoa bei elekezi ya jumla pia,kwa kuwa hapa dsm sukari ya 50kg inauzwa 95,000-94,000 kwa bei ya jumla,sasa ukiuza kwa 1800@kg utapata Tsh 90,000.sasa hiyo itakuwa ni biashara kweli au msaada.
 
Mtu wa Kilombero, Mtibwa, Moshi - TPC na Kagera - Sugar naye atanunua kwa bei hiyohiyo wakati production imo ndani ya miji husika, nadhani bei inatakiwa kuwa reviewed kwa maeneo hayo
 
Back
Top Bottom