Serikali yaonya wanaochafua VIONGOZI kwenye mtandao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yaonya wanaochafua VIONGOZI kwenye mtandao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msanii, May 16, 2009.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  na Sauli Giliard

  SERIKALI imewaonya wanaotumia vibaya teknolojia ya mawasiliano ya habari (TEKNOHAMA) kwa kuwakashifu wengine na kuwadhalilisha viongozi.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla mara baada ya kuzindua Wiki ya Teknolojia, Mawasiliano na Habari Duniani, ambayo hapa nchini, imeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kwa kushirikiana na wadau wengine.

  Katika maadhimisho hayo yanayoongozwa na kaulimbiu ya ‘Mkinge Mtoto na Teknolojia ya Habari’, waziri huyo alisema sheria mbalimbali za kuwalinda watu wasipate madhara yanayotokana na matumizi mabaya ya TEKNOHAMA zinaandaliwa.

  “Watu wanatumia vibaya teknolojia hiyo. Watu wanawadhalilisha wenzao na hata viongozi, haya si matumizi mazuri. Mtu anafanya hivyo akiwa hapa nchini au hata Marekani, lakini kwa vile hawaonekani, tunasema sasa tutawapata,” alisema.

  Aliongeza kuwa, matumizi mabaya ya teknolojia hiyo, ikiwamo simu za mikononi, zimewaletea watu madhara makubwa kwa baadhi ya watu na hata kusababisha vifo.

  “Matumizi mabaya ya simu yanaathiri watu. Hivi karibuni msichana mmoja maeneo ya Muhimbili, alijiua baada ya kutumiwa ujumbe uliomchanganya. Haya si matumizi mazuri ya simu,” alisisitiza.

  Aliongeza kuwa, pamoja na sheria ya kudhibiti matumizi ya mawasiliano kuandaliwa, serikali imeshaanza mchakato mwingine za kuzuia simu zinazotumia mfumo binafsi (private), na hadi kufikia Julai mwaka huu, itakuwa imekwishaandaa utaratibu wa kusajili watumiaji wa huduma ya simu za mkononi.

  Waziri Msolla aliwataka wadau wa huduma za mawasiliano nchini, kupunguza gharama za huduma ya mawasiliano ili Watanzania nao waweze kunufaika na matumizi ya TEKNOHAMA.

  Akielelezea hatua ambazo serikali inazichukua kwa lengo la kuiwezesha nchi kuunganishwa, ikiwamo na mikoa na wilaya pamoja na nchi jirani, alisema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa kujenga mkonga wa mawasiliano wenye urefu wa kilomita 10,000, utakaochukua miaka miwili kukamilika, lakini utasaidia teknolojia ya mawasiliano kusambaa na kutumiwa na wengi.

  Katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Jaji mstaafu Buxton Chipeta alisema ikilinganishwa na kipindi cha muongo mmoja uliopita, kumekuwapo mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano na kufanya wadau kukaa na kutafakari juu ya mabadiliko ya tabia kwa jamii.

  Takwimu za TCRA zinaonyesha kuwa, kwa sasa kuna watumiaji wa huduma za simu za mkononi milioni 13 na kumekuwapo na ongezeko kubwa la vituo vya redio na televisheni.

  Maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Maua Daftari na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi kutoka Jiji la Dar es Salaam, yanatarajiwa kuendelea leo kwa kutembelea shule, kuona matumizi hayo katika nyanja ya elimu.


  Source: Tanzania Daima

  Nilichopata hapo: Wanajiandaa na ule kucheza wimbo wa Fella Anikulapo Kuti uitwao ZOMBI! yaani ngoma ndo imeanza kwenye lele na pamoja na kwamba wapo kweli wanaowachafua watwana wetu hawa kiukwelii lakini kama mjuavyo mtego wa panya hunasa hata mbu hivyo tujiandae kukwea karandinga sooon.
  Kama mnabisha subirini baada ya miezi minne mtakubali tu!

  Lakini kama jamii tujiulize

  1. Kwa nini viongizi wachafuliwe? je ni wasafi kihivyo?
  2. Tafsiri ya kuchafuliwa kiongozi ni ipi? hapa wafafanue kiwango au ishu zipi zinazogusa stake ya usafi wa kigogo? Maana isije ikawa neno fisadi kwao ni tusi zito sana. hehe
  3. Ni mpaka viongozi wakichafuliwa ndipo hatua huchukuliwa? mbona sisi tunachafuliwa kweupeee na hata taarifa zikitolewa kwa vyombo husika hakuna jipya.... Angalizo Magazeti ya Shigongo na wenzake yanavyotuchafua na kuichafua jamii kila kukicha.
  4. Lini tutapata viongozi wenye busara ambao kauli zao zitaeleweka bila maswali mengi?
  Ah nshajichokea mie.
  TUKATE ISHU
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na hawa nao wakue sasa..!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wanachimba biti tu hao...hawana lolote.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hivi mtu aliyechafuka anaweza kuchafuliwa tena.. au ni aina ya uchafu ndiyo tatizo? kwa mfano aliyechafuka kwa matope haruhusiwi kuchafuliwa kwa shombe.. kwa sababu linanuka zaidi..
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wenzako hawauoni huo uchafu unaouona wewe. Watasema wewe una hallucinate tu...
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  May 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Akichaguliwa na yeye si anajisafisha ? Au anaweza kufikisha suala hilo katika vyombo vya sheria hata tovuti iliyomkashifu inaweza kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kutoa maelezo zaidi
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mtu mchafu hawezi kuchafuliwa...
   
 8. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Anaweza..... lakini kwa kuchafuliwa zaidi maana hata uchafu nao una gredi ndio maana kuna nguo waweza kufua na mbuni ila zilizochafuka na grisi mpaka zilowekwe kwa sabuni ya unga
   
 9. L

  LeoKweli JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani haukumwelewa mheshimiwa waziri, alikuwa anamaanisha kwamba msiongelee UFISADI , kwasababu mnawachafulia mazingira ya kula.
   
 10. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #10
  May 16, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  mtu akikupaka matope kichwani halafu akaja kukuambia ule matope hayo kesho yake anakumwagia maji machafu
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Anayetakiwa kuonywa na Serikali ni yule aliyetamka maneno haya kwenye jukwaa la siasa dhidi ya wananchi wa Tanzania:


   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  May 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ama kweli mawaziri wetu hawana kazi!.. yaani hata sielewi niseme nini... Duh!
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  -- Vs --

  Which is which?!!!!!

  grrrrrrrrrrrrrr!! Habari hii inanikera kila ninaporudia kuisoma....
   
 14. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hili Taifa letu lingekuwa lina viongozi wazalendo wa kweli na wapenda maendeleo ya nchi kwa maliasiri tulizonazo, hivi sasa tungelikuwa hatuko duni kama hivi wengi tulivyo. Viongozi wetu tuliowachagua kwa matumaini ya kutuongoza wameshindwa kufanya hivyo, hivyo wametudharirisha sisi wananchi wa Taifa hili kwa muda wote huu wao kama viongozi. Jambo ambalo linapelekea hata viongozi wenzao kwa kujisahau kuwa wao ndiyo wametufikisha hapa kutukana ndugu zetu vijijini kwa kukosa njia za mawasiliano na uelewa wa mambo yaliyo ya msingi kwa kila mmoja wetu.

  Hiyo kampeni ni bora waibatize iwe: "wakinge watoto wa matajiri kwa Teknolojia ya Habari" au kiusahihi zaidi: "Mkinge Mtoto Mwenye Uwezo wa Kuwa na Simu, TV, Computer kutoka katika madhara ya Teknolojia ya Habari"

  Neno "madhara" halimo kwenye motisha ya kampeni... Watoto na wanananchi waliowengi wala hawana nishati za kucharge simu zao, sembuse kupata hizo habari? Mh. Mkuchika mwenyewe kataja kuwa TV na magazeti hayawafikii.

  Eti mbinu za kuwalinda watu na madhara ya Teknohama zinaandaliwa. Just be frank, and tell us that you are about to copy and paste the Chinese communist ways of dealing with government critics.

  Gung ho!!

  Ballyhoos!!

  [R.I.P. kwa huyo Dada]
  Lakini jamani, huu ni mfano gani kuuweka hapa kama kielelezo ya madhara ya Teknohama? Nikizingatia sensitivity iliyopo, kweli mfano kama huu mtu huwezi kujiuliza kuwa kuna watu hapo miaka chini ya 15 tu iliyopita walikuwa wanatumiwa barua kwa njia ya posta na walikuwa wana commit suicide kutokana na ujumbe uliomo kwenye barua hizo? Isitoshe, karibia matukio yote ya watu kujinyonga/kujiua yanasababishwa na mawasiliano kati ya watu au kundi la watu; Sasa je, tupinge njia zote za mawasiliano kwa sababu watu huweza kujiua kwa jumbe zitumiazo njia hizo?!!


  Whoo woo whooo.... scary!! Routing za simu nje ya nchi ndiyo kwishney kabisa, au siyo?! How draconian!!

  I whole heartedly support the Minister's statement. The imminent fibre optic trunk should play a big role in making the aforementioned a reality.

  Ingependeza kwa saaaaaana kama angeongezea na kwamba; serikali inasomesha wataalam kadhaa katika kuhakikisha hili linafanikiwa, pia serikali ina andaa mpango huu au ule katika kuhakikisha wananchi wanafahamu vyema matumizi ya teknolojia inayotarajiwa kuwafikia ndani ya miaka miwili.


  Mambo ya maisha ya "misheni town" yanawafanya viongozi wetu wasahau kabisa kuwa kuna mamilioni ya wananchi walioko vijijini ambao hawajui hata namna ya kuwasha taa ya stima, sembuse kutuma SMS!!


   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Viongozi wamejichafua wenyewe na wala wasitafute mchawi kuhusiana na kuchafuka kwao na sasa hivi hawana uwezo tena wa kujisafisha wanachoweza kufanya ni kuachia ngazi tu maana Watanzania wengi hatuna imani nao kabisa.
   
 16. GreatConqueror

  GreatConqueror Member

  #16
  May 16, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Je nani atkaewashughulikia wanamtandao waliowachafua wenzao kwa kutumia vyombo vya habari 2005. Mkuki kwa nguruwe...
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Waziri Professor mzima anayeelewa accountability na freedom of speech anashindwa hata kuweka wazi kuchafuliwa kwa viongozi ni kupi na genuine criticism ni nini, na kufanya maneno yake yaonekane kama ni vitisho vya a totalitarian regime against freedom of speech.
   
 18. j

  jibabaz Member

  #18
  May 17, 2009
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli. Pia kuongeza, ukiona mtu mchafu ukamwambia aisee ndugu yangu we umechafuka, hio ni kosa? Ama la hawa viongozi wetu wamezoea kuvimbishwa kichwa. Mijitu mikubwa lakini laaa..yaani wanataka umwambie kuwa eeh unafanya kazi nzuri, watu wanawasingizia. lakini unakubalije kusikia uongo juu yako namna hio?? Wee mchafu basi ni Mchafuuuu..kaa Msafi basi ni msafii..
   
 19. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  "hawaonekani" Yaani Invisible?
   
 20. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #20
  May 17, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wiki iliyopita Kulikuwa na wiki ya TEKNOHAMA ambapo mada kuu ilikuwa ni kumkinga motto dhidi ya mitandao , sikufanikiwa kufika katika maadhimisho yenyewe lakini kuna nimeviandaa naamini vitasaidia sana katika kuwakinga , kuwalinda na kuwaelimisha watoto hata wale wengine ambao wanataka kuanza au kujiendeleza katika TEKNOHAMA .

  Kila mwananchi bila kujali anakaa kijijini au mjini, wasomi au si wasomi, ni lazima waandaliwe kutumia fursa za TEKNOHAMA kwa kuondoa mgawanyiko uliopo katika matumizi, ili kukuza uchumi ikiwa ni pamoja kwenda sambamba na karne ya sayansi na teknolojia

  Hakuna mabishano au makubaliano yoyote kama wewe na mtoto wako au mdogo wako mnaingia katika mtandao ,unachohitaji ni utumiaji wa akili , wakati mwingine ujanja Fulani na maarifa zaidi , hizi ni njia ambazo zinakufanya utumie mtandao kwa amani wewe na mtoto wako .

  • Ongea na mtoto wako au mwanao kuhusu mabaya ya mtandao na vitu vinavyotisha au kuogopesha katika mtandao pia mtandao unavyoweza kutumika kwa mambo au jambo nzuri pia , mfundishe mwanao kuongelea tabia zake anapokua katika mtandao nini anafanya akuhadithie , ongea nae kuhusu njia sahihi za kutumia mtandao na computer kwa ujumla

  • Soma na jifunze zaidi kuhusu mtandao na computer yako ili ujue mtoto wako anavyojisikia anapokuwa katika mambo hayo kama wewe , usimkataze mtoto wako atumie technologia mpya kwa sababu tu wewe hujui , mwache ajifunze mambo mapya kwa faida zake

  • Weka computer hiyo sehemu huru sio ya kujificha hapo utaweza kumchunguza mtoto wako vizuri vitu anavyopenda kufanya na tovuti anazotembelea wakati yuko katika mtandao .

  • Kama mtoto wako ni mdogo sana unatakiwa uende nae anapoenda kutumia computer haswa anapoingia katika mtandao .

  • Tenga muda maalumu wa kukaa na mtoto wako katika mtandao , muangalie wote tovuti munazozipenda , na hata umfundishe kutumia baadhi ya vitu katika computer hiyo .

  • Tengeneza mkataba maalumu au sheria maalumu za matumizi ya computer kwa mtoto wako , mfano wake uko hapo chini

  o Aina ya tovuti ambazo anaweza na ambazo hawezi kutembelea
  o Kitu cha kufanya kama anakutana vitu vya ajabu ( kama mtu anamwomba jina lake , namba zake za simu au taarifa zingine za siri )
  o Njia za kuepukana na kushugulika na matatizo ya mtandao kama vitisho , uonevu na mabaya mengine
  o Aina ya mambo yanayotakiwa katika mtandao kama chat ,email , shoping au kuangalia tu kurasa za tovuti , download na mengine mengi
  o Aina ya taarifa wanazowapa wenzao katika mtandao au wanazobadilishana
  o Kufuta taarifa za tovuti ambazo ametembelea kama akishatoka katika mtandao
  o Muda anaotumia katika computer au katika mtandao
  o Jinsi watakavyolinda na kuheshimu mkataba au sheria hizi wanapokuwa katika mtandao na utumiaji wa computer

  • Ukitengeneza mkataba au maelezo haya , fanya mkataba na mtoto wako au wowote anayetumia computer na mtandao

  • Ni ukweli ulio wazi kwamba ukimpa mafunzo zaidi mtoto wako mwisho wa siku anaweza kujua kutumia computer vizuri na zaidi kushinda wewe , na ataweza kujua tovuti ambazo wewe umetembelea au unazopenda kuangalia kwahiyo uwe makini unaweza kutembelea tovuti za ajabu uwe unafuta hizo historia

  • Mfundishe mtoto wako kuuliza maswali za taarifa au habari anazoona au kukutana nazo katika mtandao na kutafuta maarifa zaidi , wewe ufanye hivyo kwa faida zako .

  Pamoja vitu vyote hapo juu pia kuna program nyingi sana zinazouzwa zinazoweza kumsaidia mtoto wako kuwa busy na masomo yake au na vitu vingine katika computer yake zaidi ya hayo , programu zingine zinaweza kuzuia mtoto asiweze kufanya baadhi ya vitu kadhaa , au kuweka muda maalumu kwa ajili ya kutumia na hata zingine za kuzuia baadhi ya tovuti zisifunguke .

  USIKU MWEMA
   
Loading...