Serikali yangu haijanitendea haki

Serikali yangu haijanitendea haki

Kilichosababisha mkose mkopo ni necta, wamepasisha mpaka vilaza sasa saivi wote wanahitaji kuingia chuoni, haya sasa. Tanzania mfumo wa elimu ni mbovu
 
Sasa wewe hasira za kukosa mkopo tu....Hebu fikiria hasira za Watanzania milioni 45 kuhusiana na ufisadi, ujangili, ugaidi, utajiri wa nchi kuwanufaisha wachache, watoto wako kukosa mikopo/ajira huku wakiambiwa wajiajiri wakati hawana mitaji ya kuanzia biashara na wao wenye mitaji ya kuanzia biashara watoto wao wanawaingiza kinyemela katika taasisi mbali mbali nchini, hasira za kuona mikataba ya mbali mbali nchini haijali maslahi ya nchi hata kidogo. Warudishie kadi ya Mamndenyi.


Aiseee huu uandishi huu mbona hivi?
 
Last edited by a moderator:
Am serious my man. Bodi ya mikopo ina utani na watu. Wafute mashule yao ya serkali. Kwani watoto si watasoma tu.

Nenda physically pale HESLB waeleze kinagaubaga ikiwezekana ukate rufaa ningekua karibu ningekusaidia maana ni haki yake huyo dogo
 
Salamu sana.
Hapa nakaribia kupasuka kwa uhuni niliofanyiwa na bodi ya mikopo.
Imekuwaje mtoto wa mimi mkulima asipewr mkopo hata senti moja.

Kasoma shule za kidumu na mfagio tokea msingi hadi a levo.

Mtoto wa kike kajitahidi kapata div moja. Jkt kwa mujibu kaende. Leo wanasema eti budget exhausted.

Bado sijaelewa somo.

Tena mi nalalamika kivyangu. Na wewe ulalamike yako.

Chanzo cha kuifilisi bajeti ya masomo ya juu kipo hapa.

Poleee njoo UD hapa kitivo cha sheria nikuleee....

Maaana sisi wengine serikali inatuogopa..Lol
 
Maneno makali lakini si uongo Mkuu. Sasa kama unashangazwa na maneno makali mauaji ya Mwangosi na hadi leo muuaji wake kupeta uraiani hushangai Mkuu? Waliotaka kumuua Dr Ulimboka hadi leo hii bado wapo mtaani hushangai mkuu?, Nchi tajiri kama ya kwetu viongozi wanakuwa mabilionea hata kuficha pesa nyingine nchi za nje huku Watanzania walio wengi wakishindwa kujua hata mlo mmoja kwa siku hawajui utatoka wapi, hushangai Mkuu?

Maneno makali
 
Maneno makali lakini si uongo Mkuu. Sasa kama unashangazwa na maneno makali mauaji ya Mwangosi na hadi leo muuaji wake kupeta uraiani hushangai Mkuu? Waliotaka kumuua Dr Ulimboka hadi leo hii bado wapo mtaani hushangai mkuu, Nchi tajiri kama ya kwetu viongozi wanakuwa mabilionea hata kuficha pesa nyingine nchi za nje huku Watanzania walio wengi wakishindwa kujua hata mlo mmoja kwa siku hawajui utatoka wapi, hushangai Mkuu?

Basi inatosha.
 
mkiambiwa uozo wa CCM mliua hamuelewi! kua uyaone
 
Kitabu cha TCU kinaonesha vigezo vingi sana! Kwanza kuna wenye 1& 2 kwa masomo ya art na hadi 3 masomo ya sayansi wana sifa ya kupata mikopo!
Pia kuna course priority kama Ualimu na Udaktari!

Pamoja na hayo kuna vigezo vya mtu kutokuwa na mzazi au wazazi lakini lazima awe amefaulu!

Mimi nakuomba Mamndenyi nenda TCU ufanye appeal kama nilivyo kwambia kuna mtoto wa ndugu yangu nae kakosa japo hana mzazi mmoja na alipata 2 na wamemwambia afanye appeal wata mzingatia kuna makosa yamefanyika!

Nakuomba uende bodi watakusikiliza!

Mkuu wa kazi kama mzazi mmoja mie ni mzazi mmoja. Kama tcu kozi aliyoomba ina priorty. Kama bodi nimeenda . Pale bodi wapo juu juu wamesema kama.pesa imeisha tufanyeje. Wamewalipa vijana wao wana fanya kutia watoto waliojaa pale moyo kana kwamba ni waathirika wa janga la mikopo.

Niambie niende wapi kwingine zaidi ya jf.
Sikutaka ila imelazimu nifanye hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Nenda physically pale HESLB waeleze kinagaubaga ikiwezekana ukate rufaa ningekua karibu ningekusaidia maana ni haki yake huyo dogo

Nimeenda mkuu.
Jibu wanakuambia soma ulivyoandikiwa. Yaanj wanaibariki budget exhausted.
 
Kilichosababisha mkose mkopo ni necta, wamepasisha mpaka vilaza sasa saivi wote wanahitaji kuingia chuoni, haya sasa. Tanzania mfumo wa elimu ni mbovu

Hivi mtoto wa kike kakwepa mangapi hadi fom six tena.shule za nyerere na kapata a.
Ananyimwa mkopo bila sababu.
Serikali itoe tamko kuhusu shule zake . Vingjnevyo tuseme sisi.
 
NGOJA NIWAITE HAWA MAKADA WA CHAMA HIKI CHA KIPUUZI WAJE WAMSAIDIE Mamndenyi

Cc. Ritz, Simiyu Yetu., Laki si Pesa, Le Mutuz, Nape Mwandosya, Mwanadiwani, Wingu,Faiza Foxy, Juliana wa Kufyonzwa, Msalani, Vuta ni Kuvute... et al Lumumba tema njooni mmsaidie kuandama Mamndenyi


Wako kwenye harusi ya dada.
 
Back
Top Bottom