Serikali yamwekea pingamizi Mbowe kesi aliyofungua dhidi ya DPP, AG na IGP

Kama anajiamini yeye sio Gaidi siaache kesi isikilizwe na ushahidi utolewe kwa nn anarukaruka?! anakimbilia mahakama kuu eti kupinga kuwa utaratibu haukufuatwa/haukuzingatiwa wakati anashitakiwa hivyo anaomba afutiwe kesi!! haaa!! utulie uovu wake wote uanikwe mbele ya pilato.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu yote kwa yote lkn suala la UGAIDI, daah, sikilizia kwa mwenzio!
 
Mfa maji haishi kutapatapa.
aache kesi ya msingi ingurume kama kweli yeye sio Gaidi, kwa nn anataka kesi ifutwe hata kabla ngoma haijachezwa?! anafahamu uovu wake wote utawekwa hadharani ni wananchi wataijua tabia yake ovu dhidi ya nchi hii.
Ninakuombea uhai ili uje kushuhudia ushindi wa HAKI dhidi ya udhalimu.
Ninaamini kuwa baada ya hapo Mungu atakufungulia ili umuache shetani na mambo yake yote na uwe mwema, mpenda haki sio kwako tu bali na kwa wengine.
 
Dar es Salaam.

Serikali imemwekea pingamizi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, katika kesi yake kikatiba, ikitaja sababu nne na kudai kuwa kesi hiyo ni batili kwa kuwa ina upungufu wa kisheria.

Hivyo Serikali inaiomba mahakama hiyo iifute kesi hiyo bila kuisikiliza hoja za msingi.

Mbowe alifungua kesi hiyo ya kikatiba Julai 30 mwaka huu, Mahakama Kuu dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi hiyo namba 21 ya mwaka 2021, Mbowe anapinga utaratubu uliotumika kumkamata, kumweka kizuizini na hatimaye kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi.

Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji John Mgetta, akishirikiana na Jaji Leila Mgonya na Jaji Stephen Magoiga, ilitajwa kwa mara ya kwanza Agosti 9, mwaka huu ambapo waidai waliomba siku 14 kuwasilisha majibu yao dhidi ya madai ya Mbowe.

Leo Agosti 30, kiongozi wa jopo la wadaiwa, wakili wa Serikali Mkuu Hangi Chang’a amekanusha madai ya Mbowe.
Wakili Kibatala kwa upande wake aliieleza mahakama kuwa baada ya kurejea mambo mbalimbali kuhusiana na kesi hiyo wameona kwamba hakuna haja ya kuwasilisha kiapo cha ziada.

Kutokana na pingamizi hilo la awali, kama ilivyo kawaida, mahakama imelazimika kusimamisha kwanza mwenendo wa kesi ya msingi na badala yake itasikiliza na kuamua kwanza pingamizi la Serikali.

Ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za pingamizi la Serikali, basi itaitupilia mbali kesi hiyo na hicho ndicho kitakuwa kifo chake.

Lakini kama mahakama itupilia mbali hoja za pingamizi la Serikali basi kesi hiyo itakwenda katika hatua ya pili ambayo ni usikilizwaji wa hoja za Mbowe katika kesi ya msingi pamoja na hoja za Serikali kuhusiana na madaia ya Mbowe na kisha itatoa uamuzi.

Katika usikilizwaji wa pingamizi hilo la awali, Wakili Chang’a aliomba ufanyike kwa njia ya maandishi maombi ambayo mahakama imekubaliana nayo baada ya mawakili wa Mbowe kueleza kuwa hawana pingamizi dhidi ya maombi ya Serikali ya kusikiliza pingamizi hilo kwa njia ya maandishi.

Jaji Mgetta ambaye atasikiliza na kuama pingamizi hilo aliwataka Serikali kuwasilisha hoja zake za maandishi Septemba 6 na Mbowe kuwasilisha majibu yake ya hoja za pingamizi la Serikali Septemba 9 mwaka huu.

Pia Jaji Mgetta aliiamuru Serikali kama itakuwa na hoja za nyongeza kuhusu majibu ya Mbowe, kuziwasilisha mahakamani Septemba 13 na akapanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo Septemba 23, mwaka huu, saa Nane Mchana.

View attachment 1917285

Chanzo: Mwananchi
Haki itashinda milele. Mungu mlinde Freeman.
 
Wewe mwenye nia njema umeifanyia nini nchi hii?!!....watu walitumia damu na fedha kutafuta Uhuru wako Leo unaona wana tabia ovu?!!..uliwahi kusoma hata history kidogo?!!..
Ndugu,
Tatizo kubwa sana la nchi hii ni kizazi cha hao vijana wanaoshinda vijiweni lumumba wakilishwa ujinga ambao pia wanauamini mzimamzima.
 
Ninakuombea uhai ili uje kushuhudia ushindi wa HAKI dhidi ya udhalimu.
Ninaamini kuwa baada ya hapo Mungu atakufungulia ili umuache shetani na mambo yake yote na uwe mwema, mpenda haki sio kwako tu bali na kwa wengine.
Jifunzeni kuheshimu mamlaka kwanza.
Acheni Jeuri na kujifanya wajuaji.
mtaumia bure kwa upumbavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifunzeni kuheshimu mamlaka kwanza.
Acheni Jeuri na kujifanya wajuaji.
mtaumia bure kwa upumbavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
1630412557784.png

Hawa wangetii wakoloni, mamlaka dhalimu, sijui WEWE ungekuwa wapi?
Amen
 
Mbowe anafahamu uovu wake alio kuwa anutenda kwa kificho sasa anataka ajinasue kwa njia ya mkato ili uovu wake usitambuliwe na watu wengine. anaona aibu na fedha kwa kiongozi kama yu kufanya hayo aliyo kuwa akiyafanya dhidi ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Moja ya kosa lake ni kumtkmba mamayako ndio ukawa unakiherhere kama demu mwenye mimba ya ndugai.
 
Back
Top Bottom