Serikali yakanusha Dkt. Kigoda kufariki dunia

Serikali yakanusha Dkt. Kigoda kufariki dunia

Status
Not open for further replies.
Tunamwombea apate afya njema kiongozi wetu arejee ktk taifa letu aendeleze ujenzi wa taifa
 
Ndugu zangu watanzania, mimi si msemaji wa Dr. Kigoda wala familia yake wala serikali. Lakini, nataka kudokeza ninachokijua. Ni kweli kuwa Dr. Kigoda yuko nchini India kwa matibabu. Kwa siku za hivi karibuni,amekuwa akilazwa ICU.

Anasumbuliwa na matatizo makubwa ya figo na ini. Tuzipuuze habari za kifo ingawa zaweza kuthibitishwa na wahusika kama ni za kweli kwa wakati na namna inayopasa. Nijuavyo, Dr. Kigoda anaendelea na matibabu ingawa hali yake si njema. Tumuombee Dr. Kigoda apate nafuu na aungane nasi kujenga Tanzania yetu.

Get well soon Comrade Abdallah Kigoda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
======

Updates:

sasa wewe tuambie ukweli
 
Wakikanusha la Kombani ila akafa kweli.....
Leo wamekanusha la Kigoda ila kama ni Kufa atakufa..
Mwamunyange walikanusha ila hawajakanusha kwanini hajaja Tanzania
 
Wakikanusha la Kombani ila akafa kweli.....
Leo wamekanusha la Kigoda ila kama ni Kufa atakufa..
Mwamunyange walikanusha ila hawajakanusha kwanini hajaja Tanzania

Mkuu wa majeshi wanasema yupo hai, kuna press imetolewa bonge la onyo
 
Mkuu wa majeshi wanasema yupo hai, kuna press imetolewa bonge la onyo

Mbona hawamuoneshi hata huko alipo maana walisema alienda Italy kwa wiki sasa wiki imepita hatumuoni hata yeye mwenyewe kukanusha
 
Mbona hawamuoneshi hata huko alipo maana walisema alienda Italy kwa wiki sasa wiki imepita hatumuoni hata yeye mwenyewe kukanusha

Kuna ulakini sana kwenye taarifa zao, hata huko Italy I dont think ni kweli,
Siingii ndani zaidi
Taarifa kutoka JWTZ kuhusu jenerali David Mwamunyange
WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, imewataka watu waliosambaza uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, kuwa amelazwa nje ya nchi kwa ugonjwa, kuomba radhi mapema la sivyo watachukuliwa hatua.

Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali Juma Sipe, imeweka wazi kuwa Jeshi na Wizara kwa kushirikiana na mamlaka husika, wanachunguza watu hao na kuwataka waombe radhi mapema kabla ya hatua hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jenerali Mwamunyange ni mzima wa afya na aliondoka nchini Jumanne iliyopita Septemba 22, 2015, saa 10.45 jioni kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda Rome, Italia kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Jenerali Claudio Graziano.

“Tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa Jenerali Mwamunyange pamoja na ujumbe wake wanaendelea na ziara hiyo kama ilivyopangwa na amesikitishwa na uvumi huo,” alisema Sipe.

Sipe alisema uvumi huo ni matumizi mabaya ya uhuru wa habari na kuupotosha umma na umeleta usumbufu kwa familia ya Jenerali Mwamunyange, Jeshi na Taifa kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa watu walisambaza uzushi huo kwamba Jenerali Mwamunyange amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya, huku wengine wakidai kuwa yuko nchini India kwa matibabu, kumuomba radhi kwa kutambua kuteleza kwao.

“Taarifa hizo ni uongo wenye kila dalili ya kutengenezwa kwa lengo la kuwatia hofu Watanzania juu ya usalama wa kiongozi huyu wa juu wa majeshi yetu, Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi, ni mzima wa afya na hayupo nchini Kenya wala sio India kama ilivyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari,” alisema Sipe.

Sipe alionya kwamba kuacha kuomba radhi, itatafsirika kuwa ni kukiri kueneza uzushi huo kwa makusudi na kwa dhamira fulani na hivyo kushawishi hatua zaidi kuchukuliwa. Alisema wizara hiyo imesikitishwa na tabia hiyo ya uzushi inayopingana na weledi na kanuni za uandishi wa habari.
 
Kuna ulakini sana kwenye taarifa zao, hata huko Italy I dont think ni kweli,
Siingii ndani zaidi

Sisi tutawaaminije kuwa hizo picha zilikuwa za kipindi hiko, watoe hata kavideo....
Viginevyo tutaamini kile ambachi hawataki tuamini
 
Sisi tutawaaminije kuwa hizo picha zilikuwa za kipindi hiko, watoe hata kavideo....
Viginevyo tutaamini kile ambachi hawataki tuamini

Mkuu wa majeshi siyo mteremko,he looks soft but very tough guy
 
Mkuu wa majeshi siyo mteremko,he looks soft but very tough guy

Inaonesha aliwakatalia kile walichotaka awafanyie wakaamua kumfanyizia, sasa kama nchi inakaa bila mkuu wa majeshi na Raisi kwa wiki nzima hiyo nchi ikoje
 
Wasemaje wa JWTZ waache vitisho, watu tuna mapenzi na wapiganaji wetu na viongozi wake hivyo taarifa kama hizo zinapovumishwa wanapaswa kuzipangua kwa vielelezo kuna shida gani kuonyesha hata clip ya mkuu wetu wa majeshi akiwa huko Italy. watu wana mapenzi hivyo ni lazima wahoji a kusambaza hizo fununu. badala ya kumaliza fununu na wao wanatoa taarifa kwa mtindo wa fununu. mambo gani haya? unadhani angekua bosi wa polisi watu wangepoteza muda na hizo fununu? ni kwakuwa watu wana imani na mapenzi na JWTZ ndiyo maana fununu zinasambaa kwa kasi na kutukisa watu.
 
Inaonesha aliwakatalia kile walichotaka awafanyie wakaamua kumfanyizia, sasa kama nchi inakaa bila mkuu wa majeshi na Raisi kwa wiki nzima hiyo nchi ikoje

nadhani Chief of staff ni kibogoyo shimbo style! Loop hole hilooooooo
 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.

Taarifa Rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho ameendeleaa kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.

Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.

Imetolewa na Assah Mwambene, Msemaji Mkuu wa serikali.

Kweli Idara ya Habari - Maelezo a.k.a Msemaji wa Serikali anashindwa kuandika barua rasmi ambayo ni headed and signed !!!
 
nadhani Chief of staff ni kibogoyo shimbo style! Loop hole hilooooooo

Nashangaa waliweka kile kisheria chao cha mtandao bila ya kuwa na watu watakaoweza trace source ya habari, kazi vitisho wangejua watanzania hawatishiwi kihivyo hata wasingethubutu...
Sheria ya mtandao ni butu
 
Sisi tutawaaminije kuwa hizo picha zilikuwa za kipindi hiko, watoe hata kavideo....
Viginevyo tutaamini kile ambachi hawataki tuamini

Kwa hiyo unamaanisha kuwa Mkuu wa Majeshi amefariki ?
 
Mkuu wa majeshi siyo mteremko,he looks soft but very tough guy

Nashangaa kwanini watu wana amoni hisia na uvumi tu, mpaka kufikiwa na kufanyiziwa kama wanavyodhani ni ngumu.

Intelijensia ya kule ni matata, na ndio iliyosimama zaidi ya zote. Na ukiangalia influence yake kwa vikosi, na walivyo loyal kwake. Hawawezi mfanyia cheap and reckless move kama hiyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom