Serikali yakanusha Dkt. Kigoda kufariki dunia

Serikali yakanusha Dkt. Kigoda kufariki dunia

Status
Not open for further replies.
Kama aliwahi kushiriki dhambi ya kumkashifu Lowassa hizi tetesi zitakuwa za kweli.
 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.

Taarifa Rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho ameendeleaa kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.

Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.
Ni vizuri watu wangekuwa na uhakika na habari kabla ya kuzisambaz
 
Eti serikali inasema anaendelea kupata matibabu. Mbona hawasemi hali yake ikoje? Matibabuuuuu matibabuuu!!!!! Serikali kila siku inavionya vyombo vya habari, lakini baada ya siku kadhaa yaliyo semwa kwamba ni uzushi yanakuwa kweli

Hili nalo ni janga.
 
VUTA-NKUVUTE kwani yeye hakuwahi kumtukana Lowasa kuhusu afya yake?? Niliomba kujua hilo tu!!!!!!!! Ili niweze kuangalia itakuwaje!!!
mzee wa push up nae kaambia asipende kupanda helicopter si unajua tena pacemaker haipendi sana altitude ndio maana inabidi ateseke sana na 4 wheel drive- mpaka kufika uchaguzi naona breaking news zitakuwa nyingi sana
 
mungu haingiliwi kwenye kazi yake

kumbe magamba ni magonjwa kupita maelezo
 
Huu mtindo wa kila anae ugua kupelekwa INDIA utamalizika lini, wengine wanapelekwa huko huku wakiwa katika hatua za
mwisho , baada ya siku mbili utasikia kiongozi fulani kafariki india au Africa kusini haya ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi ambao wakienda hospitalini wanapewa prescription na maelezo wakanunue dawa duka fulani. MADAKTARI muhimbili wana kazi gani ?.Na deni la serikali katika hospitali ya Apollo huko India kila siku LINAONGEZEKA
 
Tatizo la serikali huwa haitoi taarifa kwa umma kuwa kiöngozi fjn anaumwa hadi vyombo vya hbr vianze kuripoti. Mbaya zaidi hbr zikitoka srkli hukanusha na baadaye ndipo hukubali. Mfano hai ni Mwl JK Nyerere, hv krbn C. Kombani n.k. Huu usiri wa serikali ni kwa faida ya nani?
 
Mie nimeona taarifa inasambazwa kutoka kwenye blog ya William Malechela ,sasa sijui ya kutengenezwa ngoja tumsubiri Le Mutuz
 
tunawatambua wagonjwa mmoja baada ya mwingne.wazma wanaitwa wagonjwa,na wagonjwa wanita wazma.hii ndiyo tz.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom